Tuesday, August 14, 2007

EDITOR WA RISASI AJIBU

DEAR CHAHALI,

Tumefuatilia critisism zako na maoni ya wachangajiaji waliokuwa wakifuatilia mjadala wa habari ya Risasi uliyoishutumu kuwa ina ujanja ujanja ndani yake, kwa takribani siku saba na leo tunaamua kuhitimisha kwa kusema mambo mawili makubwa yafuatayo:-

1: Hatukukurupuka kuchapisha habari ile wala hatukuwa na nia ya ‘kuwadanganya wasomaji wetu’ (deceiving our readers, as you put it) kwani tulipewa ‘tip’ na msomaji wetu ambayo tulifuatilia na kukuta profile za akina dada watatu akiwemo huyo dada aliyejiita Melanie ambaye alijitambulisha kuwa ni Mtanzania anayefanya kazi katika miji ya Miami na Dar es Salaam.

Hivyo hoja hapa ingekuwa ‘tumedanganywa’ na huyo mtoa habari wetu na huyo dada aliyeamua kutumia picha ya mtu mwingine (kama ni kweli), kwani hii si mara ya kwanza kukuta picha za watanzania kwenye mtandao wa Hi 5 na kuziandika (rejea stori na picha ya Mtangazaji mmoja wa Redio Clouds) ambazo ni ya kweli.

Kwetu sisi isingekuwa stori kama tungejua picha zile ni za Mmarekani, kwani stori hapo ilikuwa ni kukuta jina la Mtanzania akiwa amepiga picha ambazo kwa mila na utamaduni wetu bado ni kitu kigeni ambacho kinalaaniwa.

Na kama Bw. Chahali ulisoma vizuri ‘profile’ ya huyo binti utabaini kuwa, kuna sehemu anaeleza bayana nia yake ya kumnasa mwanamuziki wa hapa nchini Rehema Chalamila ‘Ray C’ anayesifika kwa kujua kutumia kiuno chake awapo jukwaani.

Pia kuonekana Miami ni jambo ambalo hata kwenye profile yake ndivyo alivyosema na Mtanzania kuwa Porn Star Marekani haliwezi kuwa jambo geni ikiwa tayari tunao warembo wa fani tofauti ambao ni watanzania wanaoishi huko na baadhi yao wanajihusisha na vitendo vya kifuska.

2: Bw. Chahali unadai kuwa sisi ni waumini wa msemo “offence is the best form of defence” (matusi ndo njia bora ya kujilinda) kwa kuwa hoja zetu tulizozitoa tangu tuisome makala yako zimekuwa zikiegemea kujadili upeo wako wa kupambanua mambo pamoja na elimu yako, tunasema hilo kwa kuwa ulianza mwenyewe!

Kimsingi tunaamini kuwa mtu aliyesoma, akawa na tabia ya kujisomea na kuongeza maarifa kichwani mwake hufanikiwa maishani, lakini yule anayependa kutumia masikio zaidi kupata taarifa kuna uwezekano mkubwa akakosa taarifa sahihi katika wakati sahihi hivyo hujikuta anakosa maarifa.

Aidha, tunaamini mtu anayesoma vitabu huongeza maarifa, akili na hupanua uelewa wake katika mambo ya dunia. Hivyo, ni ukweli ulio wazi kuwa watu wanaopenda kusoma sana vitabu au waliosoma sana wana uwezo mkubwa wa kuchambua mambo kuliko watu wasiopenda kusoma!

Elimu humsaidia mwanadamu kupanua uwezo wa kufanya maamuzi sahihi. Hivyo tulilazimika kujenga hoja zetu kwa kuchambua uwezo wako kwa kuwa katika makala yako ulionesha kujenga hoja kwa misingi ya dharau na kebehi huku ukionesha kutokuwa tayari kufungua milango ya taarifa kuingia kwenye ubongo wako.

Katika dunia tunayoishi, ambayo sayansi na tekinologia inakua kwa kasi, kuna vyanzo vingi vya habari, hivyo kutegemea masikio peke yake kuweza kupata habari ni sawa na kuachwa na wakati, nasi hatuko tayari kwa hilo, tunahitaji kusonga mbele ndio maana tunafanya kila tunaloweza kwenda sambamba na kasi ya dunia kwa kutumia vema vyanzo vyote vya habari (hiki ndicho tulichokifanya katika habari ile inayotuhumiwa).

Mwisho, Chahali tunashukuru kwa chang’amoto uliyotupatia na bila shaka umetujua ni watu wa aina gani. Sisi si watu tusiotaka kujifunza vitu vipya na kujifanya tunajua kila kitu. Hivyo tutafanyia kazi yakinifu mambo yote yaliyochangiwa katika mjadala wote unaoihusu habari ile ili tusije achwa na wakati.

Tunawaheshimu watanzania na kamwe hatutawapa taarifa potofu katika misingi ya kutaka kupata faida na tunapokosolewa, heshima iwekwe mbele!

Asanteni kwa kunisoma,
Sub-Editor, Risasi Newspaper,
Tulizo Kilaga
+255 0715 888887

11 comments:

Anonymous said...

Nyie watu wa Risasi nadhani kama hamjui lugha msiitumie. Mnakera sana. Yaani unataka kuuhadaa umma unaosoma habari hii kuwa tafsiri ya “offence is the best form of defence” ni 'matusi ndo njia bora ya kujilinda?' Kama JK anavyosema, "hii haikubaliki!!!" Tafahali kama hamjui lugha tafuteni mtaalamu awatafsirie. Kiswahili hamjui vizuri, jifunzeni kabla ya kukurupukia lugha za watu. Hii inadhihirisha wazi kama tu Naibu Mhariri ni kilaza namna hii, wafanyakazi wengine mkoje?

Pili msitake kudanganya watu, kama hamna habari za udaku (mwaziita pendwa) kutoka nje ya Tanzania wekeni utaratibu wa kuzipata badala ya kuunganisha habari zisizokuwa na kichwa wala miguu. Chahali alichosema na anachosema ni ukweli mtupu. Ametumia uwezo na utaalamu wake kuwaeleza. Kumbukeni kukiri kosa si kujiumbua bali ni kujiimarisha katika fani. Mlichemsha, jirekebisheni ikiwezekana ombeni msamaha.

Naamini ndugu Mrisho utakuwa jasiri wa kukubali hoja yangu na za wenzangu na kuzimuvuzisha ndani ya blugu yako.

adagio

Anonymous said...

KWELI NYIE MNA UGONJWA WA UBISHI,OR IS IT?YAANI LEO MNATAKA KUTUAMBIA KUWA HUYO LORI ALEXIA ANAWEZA KUWA MTANZANIA?HIVI KAMA MNASAIDIA JAMII NDIO INAKUWA EXCUSE YA KUKOPI NA KUPASTI PICHA FROM THE NET?

Anonymous said...

Bro ,nadhani wewe ni muungwana hata kama mmekataa kumwomba radhi chahali kama wengi walivyosuggest lakini majibu yako yamenionesha kuwa wewe ni mtu mzima na unajua taaluma yako.Lakini huyo Mrisho bado anaandika pumba tuu ,ndugu mtake msitake zile habari zina walakin mi si mwandishi wa habari lakini nadhani kichwa changu kinauelewa mkubwa.Yaani umejibu kwa uungwana naona wadau wengi wataanza kuwasemehe kwa mchemsho uliotokea,Sasa huyu Mrisho anavyoleta hizo stori za watu mliowasaidia jamani au the first.Akianza Mengi kuelezea wake na yeye mtayaweza,sitaki kuandika comment kwa huyo mrisho anakera lakini mpe ujumbe.Anabore sana nadhani yeye ndo shule yake inawalakin.Kaka hii comment ukitoa usitoe message sent au sio.wasaalam

Anonymous said...

aaah!hata mimi nashangaa sana kuona huyu jamaa anakuja na habari zake tu za alinacha!sasa sisi watu wa kampuni uliowasaidia humu yameingiaje!?kujionyesha kuwa mna hela za kutosha ama??yaani katika watu sifuri huyu jamaa ni mmoja wapo!manake kutoka mwanzo wa hoja hakuna cha maana chochote ambacho ameongea!namsifu Editor wa Risasi walau yeye ameonyesha muelekeo!lakini wewe jamaa yangu mwingine ndo umechemsha kabisa na ndo haya tulikuwa tunaongea mwanzo kuwa kuna watu wana ugonjwa wa ubishi!kama wewe jamaa alikukera kwa maneno ambayo hukuyapenda kwanini usingekuja na njia mbadala ambapo jamii pia ingekuona mtu wa maana sana!ndugu yangu umesahau ule usemi wa kuwa ukimkimbiza kichaa ambae kakuibia nguo zako wewe ndo utaonekana kichaa!kama suala zima liliwakera basi mngetumia busara zenu!kiko sasa!kwani sasa nyie ndo mnaonekana ndo mmechemka kabisa!si hamuoni sasa mnakubali kuwa mlikosea kuandika ile habari!kweli kama nyie ndo watu wa kuambiwa habari na mtu basi mkaandika tu kwa vile mmeambiwa bila kufanya uchambuzi yakinifu wa habari hamuoni kwamba nyie ndo mlipotea kabisa!ukweli daima utasimama mbele!na pia msikae kupangia watu jinsi ya kuongea!Chahali ametoa lile ambalo lilikuwa moyoni mwake ambapo wengi pia tunaweza kuwa nayo sema tu ni kwa vile hatujapata wasaa wa kufanya hivyo!manake nyie inaonekana kabisa mnataka hata kupangia watu jinsi ya kuwakosoa!kwani nyie mmekuwa nani??kamwe haitakuwa hivyo na kuanzia sasa tutakuwa sambamba sana na nyie kwani mmeshaonyesha udhaifu wenu ulipo!kumbe mambo ya mtandao nyie ni wageni!hahahahah!muachie basi wale wanaoyajua na muwe warahisi kuelewa pale mnapopewa shule!mjadala hope now utakuwa umekwisha na kukubali kuwa aliyewapa habari ndio aliwaongopea ila na nyie mkawa wafupi wa mawazo labda ni kwa ugeni wenu katika masuala ya mtandao na mkaamua kubandika hivyo hivyo!na kwa Chahali ni kwa vile aliwakebehi ndo maana mkaona kuwa mumdhalilishe!ila tungewaona wa maana sana kama mngekuja na hoja za msingi kama mlizoleta sasa walau tungeweza kuwaelewa lakini tungewalaumu kwa kuandika habari ambayo hamkuifanyia uchambuzi na kujua ni ya kweli ama feki!

Anonymous said...

..Bado nakushangaa wewe Editor unasema kuwa eti unasema "Kwetu sisi isingekuwa stori kama tungejua picha zile ni za Mmarekani" Sasa unakubaliana na umma kuwa nyie ndo mmekuwa wafupi wa mawazo kwa kushindwa kufuatilia na kupata ukweli kuwa zile picha ni za mmarekani????sasa huko kama sio kukurupuka ni nini??halafu umesema pia kuwa "Kwetu sisi isingekuwa stori kama tungejua picha zile ni za Mmarekani, kwani stori hapo ilikuwa ni kukuta jina la Mtanzania" hapo bado nazi kuwapima tu akili zenu!yaani kweli kuna jina la Mtanzania na Mmarekani???waungwana hebu nisaidie na nyinyi!eti wamekuta jina la Mtanzania!ukiachilia hayo yote wewe mwenyewe binafsi UNA UHAKIKA GANI NI JINA LA MTANZANIA???au nyie ndo wale wa bendera hufuata upepo??poleni sana kwa hilo!manake kiukweli ni KUWA MMESHINDWA KUTHIBITISHA KUWA HAO WADADA NI WATANZANIA!
Pia Editor naomba uelewe hapa kuwa suala linaloongelewa ni kuwa PICHA SIO ZA WATANZANIA ila Profile inaweza kuwa imendikwa na Mtanzania na amini usiamini anaweza kuwa hata ni mwanaume kandika hayo maneno au vile vile anaweza kuwa ni mwanamke!hivyo Ray C kutajwa pale kwenye profile binafsi naona sio point ya msingi sana katika kupelekea umma kuamini kuwa picha ni za Mtanzania!
Mwisho naomba kunukuu haya yatuatayo "Mwisho, Chahali tunashukuru kwa chang’amoto uliyotupatia na bila shaka umetujua ni watu wa aina gani. Sisi si watu tusiotaka kujifunza vitu vipya na kujifanya tunajua kila kitu. Hivyo tutafanyia kazi yakinifu mambo yote yaliyochangiwa katika mjadala wote unaoihusu habari ile ili tusije achwa na wakati." Big up Editor kwa comment nzuri!

Anonymous said...

Yaani mimi nilitegemea kuwa ungekanusha na kujibu hoja ya Chahali kwa hoja. Nafikiri na wewe unakiri kuwa hizo picha aliyewapa hiyo story alidanganya na wewe mwenyewe hukutumia source nyingine kuihakikisha hiyo story ukweli wake, hivyo Chahali alilolisema, ni ukweli mtupu.

Nafikiri next time jaribu kuwa makini, sababu story mliyoandika kuwa Chahali anaropoka kumbe ni nyie ndo mnaropoka kwa kudanganya watu. Kumbuka siku hizi sio enzi za ujima kwani kuna source nyingi za info. na free hakuna urasimu kabisa.

Cha mwisho, kumsaidia mtu si lazima wewe mwenyewe ujitangaze kuwa nimemsaidia fulani, Bw. Mrisho itabidi ututake radhi wasomaji wa blogu yako kwani umeonyesha wewe ubinadamu ni kidogo kwako kwani haikuwepo haja ya kuweka watu ambao mmeshawasaidia. Ulichotakiwa hapa ni kumwomba CHAHALI radhi period

Anonymous said...

kwa RISASI,
nadhani mngefanya jambo la maana kumuomba CHAHALI radhi.
mkitaka msitake, habari yenu ilikuwa FEKI. mlimponda chahali kuwa kapata taarifa kutoka kwa rafiki na hakuifuatilia!! kumbe aliifuatilia kwa kina ana akaja na zaidi ya website 5 za kuwaonyesha kuwa wale si watanzania!
cha kusikitisha ni kuwa nyie source yenu ni Hi5 ambayo hata humo mmoja tu ya hao warembo amejiandika ni MTz na mwengine kusema ni MGANDA. sioni kimisingi ipi nyie mlimuamini huyo alowapa TIP wakati mnajua kuwa Hi5 watu hutumia picha ambazo si zao kama mfano mliouweka.
inaonyesha hamna credibility kwenye source zenu na uchambuzi wa mambo.
lasty haina maana kama mna nia ya kusaidia jamii ndio tuamini kama hamuuzi habari FEKI kwa jamii ili kupata faida zaidi.
kuwatoa watu ulokuwa umewasadia inaonyesha element za kusumbulia na element za kuwa umesaidia ili upate sifa na sio vyenginevyo.
kabla hujaandika .....fikiria sana unachotakak ukiandika.
wasalaa,

Anonymous said...

Sasa mtaomba msamaha au mtaanza kuleta nakala ndefuuuu ambazo mnataka kujikosha tuwaone kuwa ni wa kweli? penye ukweli uongo unajitenga, Siku zoote tulikuwa tunasikia watu wakidharau magazeti ya udaku na huwa wanayasoma tu kupoteza muda na hawajayapa umuhimu kama baadhi ya magezi mengine, na ndoo maana hata maofisini (ofis zenye kujiheshimu) hamna bill za magazeti ya udaku, hayo usomwa hasa uswahilini.

Angalia hii paragraph then nani alaumiwe CHAHALI AU NYINYI WATU WA RISASI?

Kimsingi tunaamini kuwa mtu aliyesoma, akawa na tabia ya kujisomea na kuongeza maarifa kichwani mwake hufanikiwa maishani, lakini yule anayependa kutumia masikio zaidi kupata taarifa kuna uwezekano mkubwa akakosa taarifa sahihi katika wakati sahihi hivyo hujikuta anakosa maarifa.

SOMA NA HII....
Hivyo hoja hapa ingekuwa �tumedanganywa� na huyo mtoa habari wetu na huyo dada aliyeamua kutumia picha ya mtu mwingine (kama ni kweli), kwani hii si mara ya kwanza kukuta picha za watanzania kwenye mtandao wa Hi 5 na kuziandika (rejea stori na picha ya Mtangazaji mmoja wa Redio Clouds) ambazo ni ya kweli.

SASA NYINYI NA CHALALI NANI ANAEPENDA KUTUMIA MASIKIO? KWAHIYO NYINYI NDO MMEKOSA MAARIFA !!!!

Chahali alitumia masikio wakati wa uchunguzi ili kukusanya kitu kinachoeleweka? na chenye uhakika sidhani kama huyo rafiki yake chahali alikurupuka tu na kumpa hizo link CHAHALI itakuwa katika upepelezi chahali aliuliza ndo akapewa hizo link ni kwamba tangu anasoma alipata wasiwasi wa hiyo habari kwahiyo hakutumia masikio kwa kupata uhakika!!! Cha kushanganza nyie ambao mnawahabarisha watu umma wa Tanzania (uswahilini) mmeshindwa kuzifanyia utafitizi hizi habari na kuziweka kwenye magazeti na msituambie kuna mamiss wanafanya ufska huko ughaibuni tunahitaji vithibitisho sababu sasa hivi IMANI imeshotutoka zaidi na haya magazeti ya UDAKU.

Kama ni wastaarabu mnapaswa kumuomba radhi CHAHALI KWA KUSEMA KUWA AMEKURUPUKA, KUMBE NYINYI NDO MMEKURUPUKA, NA PIA MUWAOMBE RADHI WATANZANIA WOOTE KWA KUTUDHALILISHA YAANI HAMNA HATA UCHUNGU NA NCHI YENU MNAIPAKAZIA MABAYA KIASI HICHO????

NA NDIO MAANA MLIKOSA HATA POINT ZA KUONGEA MKAANZA KUINGILIA MAISHA BINAFSI YA CHAHALI KUWA HAFANYI VIZURI SHULE, OOH ATAMPONZA MENGI!! TATIZO NYINYI NI WACHONGANISHI WA KUBWA NA WAKUZAJI WA MAMBO.

Kwetu sisi isingekuwa stori kama tungejua picha zile ni za Mmarekani, kwani stori hapo ilikuwa ni kukuta jina la Mtanzania akiwa amepiga picha ambazo kwa mila na utamaduni wetu bado ni kitu kigeni ambacho kinalaaniwa

Hivi katika hii tanzania ni gazeti gani ambalo linasemwa na kuongoza kwa kutoa picha za uchi kama sio magazeti yenu ya UDAKU? Magazeti yenu mnapiga picha watu uchi mnawaweka kwenye gazeti ambalo huko uswahilini linasoma na baba na mbele ya watoto sasa nyinyi na hao wa kwenye mtandao ni nani anaekiuka maadili? habari za UZINIFU MNAZIPA KICHWA KIKUBWA CHA HABARI MNAHARIBU WATOTO NA MUNGU ATAWALIPA HAPA HAPA, MNASHINDWA KWENDA KUSAKA SHIDA WANAZOPATA WATU VIJIJINI HUKO MKALETA KWENYE MAGAZETI.

HONGERA SANAA KAKA CHAHALI KWA KUTUFUMBUA MACHO!!! KEEP IT UP.

Anonymous said...

Mrisho, eeeeh

Kuna msemo wa kiswahili usemao kuwa kuna watu wa aina nyingi katika dhana ya kujua.

1. Kuna yule ambaye hajui, na hajui kwamba hajui,huyu ni .....
2. Kuna yule ambaye hajui, na anajua kuwa hajua, huyu ni......
3. Kuna anayejua na hajui kua anajua, huyu ni.......
4. Kuna wale ambao hawajui, lakini wanajifanya wanajua. Wao ni ......

Sasa kwa mustakabali huu, wewe nakuweka kwenye kundi la nne, wewe haujui chochote kwenye hili jambo, ila unataka kutuonyesha kuwa unajua. Kwa maana nyingine unataka kutupotosha. Pia nakuweka kwenye kundi la kwanza, inawezekana kabisa wewe haujui na haujui kuwa hauji. Maana kwa mtu mwenye akili yake hawezi kumshambulia Chahali tena kwenye personal issues, eti hafanyi vizuri huko kwenye masomo yake, kumbuka Chahali anafanya PhD, ikimaanisha kafanya digrii ya kwanza safi, akaenda ya pili safi, sasa anatafuta PhD. Haya mwenzetu wewe uliye kipanga, umemaliza digrii ngapi hapo ulipo. Maana wakati mwingine inaudhi kumshambulia mtu kumbe wewe inawezekana umemaliza form 4 au form 6 na kufanya kozi, tena sio digrii. Tupe profile yako, tueleze ulikuwa unafanya vipi shule na tupatie grade zako, sio kuleta tu longo longo zako hapa. Mimi nimemaliza digrii ya kwanza, na nilikuwa na Upper division second class. Wewe jeeeeeeeeee.

Ukitundika hii comment, itakuwa kheir, ukii moderate, ujumbe utakuwa umeupata. Na kwa sie waislam hatutakiwi kuwa wanafiki, ukiimoderate tu ni unafiki

Anonymous said...

Ni ukweli usiopingika kwamba magazeti yenu sometimes huwa yana beba news za udaku na matokeo yake watu makini kama Chahali huamua kufanya uchunguzi wa stori na kugundua kwamba kuna utata au ni udaku per se! Nimepitia kwa makini mjadala mzima na nimesikia hoja za pande zote mbili, pia nimepitia tena stori zenu ambazo nilikuwa ninazitilia mashaka. Kwa mtazamo wangu Chahali hana kosa lolote japokuwa mmeendelea kumlaumu, kosa lake ni kuwakosoa na kusema stori yenu haikuwa na uhakika.

Mhariri wa Risasi umemlaumu Mhariri wa Kulikoni kwamba aliweka headline ya kuhusu gazeti lenu wakati contents za news zilikuwa 95% zinahusu mambo ya ughaibuni, and only 5% ndiyo zinahusu gazeti lenu (Risasi). Matatizo hayo pia mnayo kwenye news za kwenu. Gazeti la 2/8 mliweka picha za Mastaa 10 kwenye ukurasa wa mbele na kusema 3 kati ya hao wana ngoma. Baada ya kusoma hiyo habari hakukuwa na link yoyote ya kuwahusu hao mastaa 10 mliowaweka picha zao kwenye ukurasa wa mbele. Mbaya zaidi kwenye habari mlikiri kwamba wasanii wengi (mastaa) wamekuwa wakikwepa kwenda kupima ngoma, na mkasema inawezekana kati ya hao 10 hakuna mwenye ngoma (huo kama siyo udaku ni nini?). Mtu akisoma headline impression anayoipata ni kwamba watatu kati ya hao mastaa wana ngoma, but ndani ya stori hakuna kitu kama hicho! Na stori inayowagusa hao mastaa ni less than 5%!

Tuje kwenye stori husika ambayo ilipelekea malumbano haya: Headline inasema kwamba “Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu … zasambazwa mitaani, baadhi yao ni washiriki wa mashindano ya kusaka mataji ya u-miss!” Ndani ya stori umetoa namba za simu za mkononi za Bongo na ukadai una picha za wahusika ambazo zina msg nyuma ya picha, impliedly you had hard copies of photographs, lakini ukashindwa kuzilinganisha picha ulizo nazo na zile ulizozikuta kwenye website ya hi5 na yet ukajiridhisha kwamba ni news ya ukweli kiasi cha kukubali kuichapa kwenye gazeti lako. Responsibility yako kama Mhariri iko wapi? Sina hakika kama mtu anaweza kushindwa kutofautisha picha za hard copies na zile za kwenye mtandao kama ni picha ya mtu yule yule ama mtu mwingine. The bottom line ni kwamba mlichemka na huwa mnachemka mara kwa mara kwenye stori ambazo hazina uhakika unless kama mmepiga picha ninyi wenyewe na hakuna mtu ambaye alishawahi kuwalaumu pale ambapo mna evidence ya tukio. Lakini kwa issue ya hizo picha za warembo ule ulikuwa ni mkorogo na mchemsho wa nguvu. Kibaya zaidi mkawaunganisha na mabinti wanaogombea u-miss, stori kama hiyo ina implication gani kwa jamii? Unadhani jamii itawachukuliaje watu wanaogombea u-miss kama siyo kuwaona ni Malaya?

Kwa maoni yangu Chahali was right lakini kwa kuwa amewagusa mahali pabaya (kuharibu maslahi yenu kwa kuwafungua macho watanzania) ndiyo maana mmejikuta mkikosa hoja na kuanza kupapasa huku na kule mpaka mkaingilia maendeleo yake ya kimasomo. Hiyo ni kasoro kubwa sana katika kujitetea. Siku zote, hoja hujibiwa kwa hoja na siyo personal issues za mhusika. Bado ninasimama pale pale kwamba Chahali ana-deserve kuombwa msamaha maana tayari mmejiweka mahali ambapo mmeji-expose na kuonyesha wazi alichokisema ni cha kweli na nyie hamkufanya kazi yenu. Asante sana Chahali kwa kuwafungua macho watanzania angalau itawafanya waandishi wa magazeti haya wawe wanafuatilia kwa karibu stori wanazoandika!

No offense, nilikuwa ninatoa maoni yangu kwa kutazama pande zote za shilingi!

Anonymous said...

How much does it cost kufungua hi5 account?
Mrisho fungua kichwa hiyo na ujifunze,au ni makusudi tu ili muonekane kama hamna kosa, by the way nahisi hata hiyo whatever juice ya hi5 mmefungua wenyewe hiyo account.
Next time be careful bro'