IRENE UWOYA: Umisi nilirogwa, filamu siwezekani
MISS Tanzania namba tano 2006-07, Irene Uwoya amesema kuwa wakati akishiriki fainali hizo za urembo mwaka juzi, alirogwa na kujikuta akianguka jukwaani kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kusisitiza kwamba sasa hivi amejizatiti kumkabili mwanga yeyote atakayemuingilia katika filamu.
Irene, alimtonya mdau wa Abby Cool & MC George Over The Weekend, Issa Mnally kuwa hakuna mwanga yeyote atakayemroga kwenye filamu kwakuwa ni fani anayoipenda na kwamba hakuna atakayemkamata kwenye anga zake.
“Sasa hivi nipo ‘serious’, mchawi yeyote nitamdhibiti. Kama vipi ajitusu kwenye filamu yangu mpya ya Yolanda aone. Filamu sasa hivi ndiyo maisha yangu ndiyo maana nasema nipo tayari kupambana ili niendelee kuwepo,” alisema Irene.
Jahazi kutoa shoo ya bibi, mwana na wajukuu
TAMASHA la kuadhimisha mwaka mmoja wa Kikundi cha Jahazi Modern Taarab, litapambwa shoo iliyokwenda shule kutoka kwa bibi, mwana na wajukuu, Shufaa Lyimo anakupa ndogondogo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya QSSP Group Ltd (inayoratibu onesho hilo), Bahati Singh aliifafanulia safu hii kuwa bibi ni Fatma Baraka Hamis ‘Bi Kidude’, mwana ni Mwajuma Mzee na wajukuu ni Mzee Yusuf na Khadija Yusuf.
“Mwajuma kiukoo ni mtoto wa Bi. Kidude, pia Mwajuma ndiye mama yao mzazi Mzee Yusuf na Hadija Yusuf, kwa kweli familia yao ni ya vipaji kwasababu wote hao ni waimbaji nyota na siku hiyo wamepanga kufanya shoo bomba ya bibi, mwana na wajukuu,” alisema Singh.
Aidha, meneja huyo alitaja siku ya tamasha hilo kuwa ni Februari 29, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kwamba shoo hiyo itawakutanisha wapenzi wote wa Jahazi katika nyumba moja.

No comments:
Post a Comment