Thursday, February 14, 2008

YOU ARE WHAT YOU EAT!


Ijue nguvu ya kuponya ya vyakula

Hapo zamani za kale kabla wanasayansi hawajavumbua dawa za kisasa kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali yanayomkabili binadamu, mababu zetu walikuwa wakitumia mitishamba na vyakula kutibu magonjwa ya aina yote yaliyokuwa yakiwakabili. Kwa maelfu ya miaka, chakula kimehesabika kama tiba ya matatizo mengi ya kiafya, hilo halina ubishi hadi leo.

Lakini katika karne iliyopita, dawa nyingi za kisasa zimevumbuliwa na kuchukua nafasi ya vyakula, hasa kutokana na uwezo wake wa kutibu ugonjwa haraka. Lakini madhara yatokanayo na matumizi ya muda mrefu ya dawa hizo, yameanza pia kuwafanya watumiaji wake kukimbilia tiba mbadala za mitishamba na vyakula ambavyo havina madhara katika afya ya binadamu na hutibu kwa uhakika.

Katika makala ya leo tutaangalia baadhi ya vyakula na nguvu ilivyonavyo katika kuzuia na kutibu magonjwa mbalimbali kama ilivyothibitishwa na tafiti mpya za kisayansi juu ya suala hili na kuelezwa na mwandishi Tanushree Podder katika kitabu chake cha You Are What You Eat:

APPLE (Tufaha)

Dawa nzuri ya ugonjwa wa moyo

Hushusha kolestro

Hushusha shinikizo la damu

Huimarisha kiwango cha sukari katika damu

Huongeza hamu ya kula

Linakemikali yenye uwezo wa kuzuia saratani

Juisi yake inaua virusi vinavyoambukiza magonjwa

BANANA (NDIZI MBIVU)

Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo

Hushusha kolestrol katika damu

BEANS (MAHARAGE YA AINA ZOTE)

Hupunguza aina mbaya ya mafuta mwilini

Hudhibiti kemikali mbaya za saratani

Hudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu

Hushusha shinikizo la damu

Hurekebisha mwenendo wa utumbo mkubwa

Huzuia na kutibu ukosefu wa choo

Huzuia kutokwa damu kwenye haja kubwa (haemorrhoids) na matatizo mengine ya tumbo

CABBAGE (KABICHI)

Hupunguza hatari ya kupata saratani, hasa ya utumbo

Huzuia na kutibu vidonda vya tumbo (hasa juisi yake)

Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili

Huua bakteria na virusi mwilini

Huharakisha ukuaji wa mwili

CARROT (KAROTI)

Inaaminika kuzuia saratani, hasa zitokanazo na uvutaji sigara, ikiwemo saratani ya mapafu.

Hushusha kolestro katika damu

Huzuia ukosefu wa choo (Constipation)

COFFEE (KAHAWA)

Kahawa si kinywaji cha mtu kupenda sana kutumia, lakini kinapotumiwa kwa kiasi kidogo na kwa tahadhari, kina faida zake:

Huboresha utendaji kazi wa ubongo

Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa asma (asthma)

Hutoa ahueni kwa wenye homa

Huongeza nishati ya mwili

Huzuia meno kuoza

Ina kemikali ambayo huzuia saratani kwa wanyama

Hutoa uchangamfu

CORN (NAFAKA- MAHINDI, MCHELE, N.K)

Zina aina fulani ya kemikali ambazo huzuia saratani

Hupunguza hatari ya kupatwa na aina fulani za saratani, magonjwa ya moyo na kuoza kwa meno

Mafuta yake hushusha kolestro mbaya mwilini

Itaendelea wiki ijayo..

1 comment:

Anonymous said...

jamani kaka sasa unatuboa sana sisi wapenzi wa blog yako kwani kila tukifungua mambo ni yale yale wiki hata tatu mfululizo tunachoka kurudiarudia kusoma tupe mambo mamya kila tarehe ibadilikapo sio picha unaweka mweni mzima maana yake nini ?unatuopoa wapenzi wa hii blog.