Sunday, February 24, 2008

YOU ARE WHAT YOU EAT


Ijue nguvu ya kuponya ya vyakula-2

Wiki iliyopita tuliona nguvu ya baadhi ya vyakula katika kuzuia na kuponya baadhi ya magonjwa. Vyakula tulivyoangalia vilikuwa ni pamoja na tufaha (apples), ndizi mbivu, maharage, kabichi, karoti, kahawa na nafaka, wiki hii tunaendelea kuangalia orodha hiyo ya vyakula vyenye uwezo wa kutuepusha dhidi ya magaonjwa mengi hatari kama ifuatavyo:

SAMAKI (FISH)

Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi

Huilinda mishipa ya damu isiharibike

Huzuia damu kuganda

Hushusha shinikizo la damu

Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi

Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso

Husaidia kuzuia uvumbe mwilini

Huendesha mfumo wa kinga ya mwili

Huzuia saratani

Hutoa ahueni kwa wenye pumu

Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo

Huongeza nishati ya ubongo

KITUNGUU SAUMU (GARLIC)

Hupambana na maambukizi

Ina kemikali zenye uwezo wa kudhibiti saratani

Hufanya damu kuwa nyepesi

Hupunguza shinikizo la damu na kolestro

Huamsha mfumo wa kinga ya mwili

Huzuia na kutoa ahueni kwa kikohozi kilaini.

Huweza kutumika kama dawa ya kifua

TANGAWIZI (GINGER)

Huzuia ugonjwa wa kutetemeka

Hufanya damu kuwa nyepesi

ZABIBU (GRAPE)

Ina uwezo wa kufanya virusi visifanyekazi

Huzuia meno kuoza

Ina mchanganyiko wenye uwezo wa kuzuia saratani

PILIPILI HOHO (GREEN CHILLIES)

Dawa nzuri ya mapafu

Hutumika kama dawa ya kifua

Huzuia na kuponya kikohozi kikali

Husaidia kuyeyusha mabonge ya damu

Hutoa maumivu

Huweza kumfanya mtu kuwa na furaha

ASALI (HONEY)

Huua vijidudu (bacteria)

Huondoa wadudu kwenye vidonda na malengelenge

Huondoa dalili za maumivu

Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa pumu

Hutuliza maumivu ya vidonda vya koo

Hutuliza mishipa ya damu, humpatia mtu usingizi

Hutoa ahueni kwa mtu anayeharisha

MAZIWA (MILK)

Huzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis)

Hupambana na maambukizi, hasa kuharisha

Hurekebisha kuchafuka kwa tumbo

Huzuia vidonda vya tumbo

Huzuia kuoza kwa meno

Huzuia mtu kupatwa na kikohozi

Huongeza nishati ya ubongo

Hushusha shinikizo la damu

Hushusha kiwango cha kolestro mwilini

Hudhibiti baadhi ya saratani

UYOGA (MUSHROOM)

Hufanya damu kuwa nyepesi

Huzuia saratani

Hushusha kiwango cha kolestro

Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili

Hudhoofisha virusi

SHAYIRI (OATS)

Dawa bora ya moyo

Hushusha kolestro mwilini

Hurekebisha sukari kwenye damu

Ina mchanganyiko wa virutubisho unaodhibiti saratani

Hupambana na kuvimba kwa ngozi

Ina uwezo sawa na dawa ya kumpatia mtu choo

KITUNGUU MAJI (ONION)

Dawa kubwa ya magonjwa ya moyo

Huimarisha kolestro nzuri (HDL)

Huifanya damu kuwa nyepesi

Hushusha kiwango cha kolestro mbaya

Huzuia damu kuganda

Hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu

Huua vijidudu

Huzuia saratani

Itaendelea wiki ijayo...

No comments: