Monday, May 26, 2008

Aliyevunja ndoa yake Shania Twain ajulikana!

Marie-Anne (kulia) na Shania Twain mwaka 2006
Eebwana ee! Kikulacho kweli kinguoni mwako. Hatimaye imebainika kwamba, kuvunjika kwa ndoa ya staa wa pop, Shania Twain, wiki iliyopita kumesababishwa na rafiki yake wa damu!

Ishu hiyo ilidondoshwa na Jarida la People mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa, rafiki wa Twain aitwaye Marie-Anne Thiebaud, ndiye aliyekatisha ‘uhai’ wa ndoa ya Shain Twain na mtayarishaji muziki, Robert ‘Matt’ Lange, iliyodumu kwa miaka 14.

Baadhi ya watu wa karibu na mwanamziki huyo mwenye asili ya Canada, walilitonya jarida hilo kuwa, familia za watu hao wawili wakati mwingine huwa zina ‘spendi’ pamoja katika kufurahia maisha wakati wa likizo.

‘Twain alimchukulia Marie- Anne mmoja kati ya marafiki zake wakubwa’ kilisema chanzo cha habari kwa jarida hilo. Ishu hiyo imemfanya Twain akimbilie kwao Canada kupoza machungu ya kuvunjika kwa ndoa yake na siyo ya kusalitiwa na mume wake tu, bali pia na rafiki yake kipenzi.


No comments: