Sunday, May 11, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Jitta Man Sasa ni ‘Nzagamba Mamba’
Kutoka mkoani Mwanza, mchizi aliyepata kutingisha miaka ya nyuma kunako game ya muziki wa kizazi kipya kupitia ‘kategori’ ya ragga, Jitta Man amerudi tena akiwa na a.k.a mpya.

Ndani ya safu hii, Jitta ambaye aliikacha game kwa muda baada ya baadhi ya wadau wa sanaa hiyo kumtia ndani mkwanja wake, amesema na safu hii kwamba amerudi tena na sasa anatambulika kama ‘Nzagamba Mamba’, huku kazi yake yenye jina la ‘Maisha’ ikifanya vyema hewani.

“Hasira zilinifanya niachane na muziki, baada ya jamaa (hakuwataja jina) kunizingua, lakini nimeamua kurudi kwasababbu muziki ndiyo kazi yangu, kinachofuata hivi sasa ni ngoma juu ya ngoma, baada ya kazi hiyo natarajia kuachia video hivi karibuni, kisha nitaachia wimbo mwingine wenye jina la ‘Mimi ni wako,” alisema Jitta au Nzagamba Mamba.
Kapt. Komba Awakoromea Misambano, Hegga
Mkurugenzi wa T-RESPECT (T.O.T), Kapteni John Komba, mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka mbogo na kutaka kuwalamba vibao wanamuziki wake, Rogart Hegga na Abdul Missambano ambao walishindwa kusimamia vizuri mazoezi ya bendi yao, yaliyokuwa yakifanyika ndani ya Ukumbi wa Dar West Park, Tabata, Dar es Salaam.

“Nononooo, hebu njoooni hapa, bado sijaridhika na safu ya unenguaji, kuna sehemu wanakosea, nataka warudie kucheza na makosa kama hayo nisiyaone tena,” alisikika akifoka Kapteni Komba.

Pamoja na makosa hayo madogo madogo, bendi hiyo kwa sasa inakuja juu katika sanaa ya dansi na tayari imeshaonesha kuwakuna mashabiki kibao wanajitokeza mazoezini.

No comments: