Monday, August 4, 2008

Bushoke: albamu yangu inafanyiwa maujanja zaidi China

Kutoka pande za Dom, tunamshusha kwenu Ruta Maximilian Bushoke, mchizi huyo siku chache zijazo atadondosha Bongo ‘nyu aidia’ ambayo baadae inaweza ikawa changamoto nyingine kwa wasanii waliojiajiri kupitia sanaa ya muziki wa Bongo Flava.

Akipiga stori na safu hii juzi, Bushoke alitamka kwamba, albamu yake mpya ambayo tayari imeshakamilika ikiwa na jina la ‘Dunia njia’ ipo nchini China kwa ajili ya kuifanyia maujanja zaidi ikiwemo kurudufu kopi za mauzo.

“Albamu ina kazi zaidi ya kumi zikiwemo Chupa ya koka, Nimeshafika, Nimekuchagua, Angel, Dodoma, Kama, Hallo na nyingine kibao. Nataka kufanya kitu ambacho kinaweza kikawa mkombozi wetu, yaani kutengeneza kopi mwenyewe na kuzisambaza sokoni, badala ya kuwatengemea wahindi kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Bushoke.
Albamu hiyo inatarajiwa kudondoka kitaani mapema mwezi ujao.

No comments: