Friday, August 1, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Mrembo wa mtandao wa Global kujulikana kesho

Mrembo mwenye mvuto atakayepata kura nyingi za wasomaji kwenye tovuti ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, kati ya washiriki 27 wa Vodacom Miss Tanzania 2008, atajulikana kesho.

Miss www.globalpublisherstz.com atatangazwa jukwaani kesho kabla ya jaji mkuu kutaja jina la Miss Tanzania 2008-09. Hiyo inamaanisha kuwa kura zitafungwa muda mchache kabla ya kwenda jukwaani kushuhudia tukio la Fainali ya Miss Tanzania mwaka huu.

Mshindi wa Miss www.globalpublisherstz.com, atajinyakulia kitita cha shilingi 500,000. Miss www.globalpublisherstz.com ni shindano ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Global Publishers ambayo ni wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani, Championi na hili la Ijumaa kwa lengo la kuipa sapoti Kampuni ya Mtandao wa Simu za Mkononi ya Vodacom ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa Miss Tanzania.

JINSI YA KUSHIRIKI NENDA HAPA: www.globalpublisherstz

Kanumba apiga kolabo na mtu mzima Richard
Baada ya kutesa nchini Nigeria katika filamu ya Player No 1, mshindi wa Big Brother II, Richard Bezuidenhout, ameibukia medani ya muvi nchini na hivi sasa anakuja na bonge la picha akiwa amepiga kolabo na Steven Kanumba.

Muvi hiyo, ambayo iko kunako hatua za mwisho kukamilika itakwenda kwa jina la Bad Intention na ikiwa ni ‘production’ ya kampuni ya Game 1st Quality, Kanumba na Richard ndio wahusika wakuu (sterling) wa filamu hiyo.

Akipiga stori na Showbiz mapema wiki hii, Kanumba alisema kwamba, ndani ya muvi hiyo atakuwemo pia Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ambaye alionesha uwezo na kipaji cha kutosha ndani ya filamu yenye jina la Point Of No Return ambayo inafanya vyema sokoni hivi sasa.

Bad Intention itakuwa ni falamu ya kwanza kwa Richard kucheza nchini tangu alipotwaa taji la Big Brother Africa II mapema mwaka jana na kujishindia mkwanja wa kitita cha dola za Kimarekani 100.000.

Kwa upande mwingine, hii itakuwa ni muvi yake ya pili kucheza baada ya ile aliyokwenda kucheza nchini Nigeria mara baada ya kulitwaa taji hilo.

No comments: