Friday, May 23, 2008

IJUMAA SHOWBIZ!

Choki:Nawakubali Wakongo, wako juu
Mwanamuziki na kiongozi wa TOT Respect, Ally Choki amesema na ShowBiz kwamba, binafsi anakubali kuwa Wakongo wapo juu kimuziki ndiyo maana akafunga safari mpaka kwao na kunyakua wanenguaji kadhaa pamoja na repa, Mariam Mndeme alipiga naye stori.

Ndani ya safu hii, Ally alitamka kuwa muziki wa dansi asili yake ni Kongo na kwamba kama Wabongo tukitaka kufanya vizuri kunako tasnia hiyo lazima tutafute chimbuko lake.

“Wengi walinilaumu nilipowaleta Wakongo, wakidai kuwa sasa najimaliza, najua nafanya nini wala siwaogopi, zaidi nitajifunza mengi kutoka kwao, ukisingatia kwamba nina kipaji lakini nikiwa peke yangu sitaweza”.

Aidha, Choki aliwatoa wasiwasi wapenzi wake kwa kuongeza kuwa anaamini kuwa atafanya maajabu akiwa na timu hiyo ya Wakongo, hasa siku ya utambulisho wa Bendi hiyo. “Najua hivi sasa Wabongo wanataka nini, wasikose kuja kushuhudia”.

**************************************************************
TMK Wanaume Wamaliza ubishi Mwanza
Makundi mawili yenye uhasama wa kutosha, TMK Wanaume Halisi na Family kutoka Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita yalimaliza ubishi wa nani mkali katika shoo mbili zilizopigwa mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa mwana ShowBiz wetu aliyopo Kanda ya Ziwa, TMK Family walipata shangwe nyingi zaidi kupitia ngoma yao, Dar Mpaka Moro. “Shoo ya kwanza ilipigwa ndani ya Ukumbi wa City Cabana, kisha mpambano ukamaliziwa kunako Uwanja wa CCM Kirumba,” alisema.

Mpambano huo ulikujia kupitia Prime Time Promosheni, chini ya udhamini wa Kampuni ya Simu za Mkononi Tigo.
*****************************************************************

TUZO ZA VINARA WA FILAMU TANZANIA (TANZANIA FILM VINARA AWARDS) 2007 – 2008

Muigizaji Chipukizi wa Kike (Up coming actress)

1. Irene James – Miss Bongo II

2. Irene Uwoya – Diversion Of Love

3. Fatuma Makame – Karibu Paradiso

4. Jennifer Mwaipaja – Silent Killer

5. Grace Michael – Malipo ya Usaliti

Muigizaji Mwandamizi wa Kike (Best Actress in a Supporting Role)

1. Irene Uwoya - Diversion Of Love

2. Mama Frank – Yolanda

3. Irene James – Miss Bongo II

4. Susan Lewis – Behind the Scene

5. Tecla Mjata – Macho Mekundu

Irine Uwoya

Muigizaji Bora wa Kike (Best Actress)

1. Lucy Komba - Diversion Of Love

2. Grace Michael – Malipo ya Usaliti

3. Halima Yahya – The Stranger

4. Elizabeth Chijumba – Copy

5. Riyama Ally – Fungu la Kukosa


Muongozaji Bora wa Filamu (Best Film Director)

1. Gervas Kasiga – Fake Pastors

2. Jimmy Mponda – Misukosuko II

3. Kulwa Kikumba – Macho Mekundu

4. Haji Adam – The Stranger

5. Halfan Ahmed – Copy

Mtunza Sauti Bora (Best Soundman of The Year)

1. Adam Wazir – Fungu la Kukosa

2. Cleophance Ng’atingwa – Kolelo

3. David Sagala – Copy

4. Camillius Kanuli – Fake Pastors

5. Swalehe Juma – Fungu la Kukosa


Jacob Steven (JB)

Mpiga picha Bora wa Filamu ( Best Cameraperson of The Year)

1. Mbalikwe Kasekwa – Misukosuko II

2. Sylon Malalo – Kolelo

3. Rashid Mrutu – Copy

4. Nicholaus Mtengwa – Kilio moyoni

5. Sylon Malalo – Simu ya Kifo


Adui Bora wa Filamu (Best Film Villain)

1. Mohamed Aziz – The Body Guard

2. Irene Uwoya - Diversion Of Love

3. Sebastian Mwanangulo – Misukosuko II

4. Ahmed Ulotu – Silent Killer

5. Elizabeth Chijumba – Copy


Mhariri Bora wa Filamu (Best Film Editor)

1. Moses Mwanyilu – Misukosuko II

2. John Kalage – Miss Bongo I

3. Rashid Mrutu – Copy

4. Hassan Mbangwe – Malipo ya Usaliti

5. Sylon Malalo – Kolelo

Mwandishi Bora wa Filamu (Best Script Writer)

1. Seleman Mkangara – Malipo ya Usaliti

2. Hammie Rajab – Kolelo

3. Kulwa Kikumba - Diversion Of Love

4. Lucy Komba – Utata

5. Elizabeth Chijumba – Copy

Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kiume (Best Actor in a Supporting Role)

1. Aliko Tshmwala – Segito

2. Single Mtambalike – The Stranger

3. Adam Kuambiana – Fake Pastors

4. Halfan Ahmed – Copy

5. Emmanuel Muyamba – Fake Pastors


Adam Kuambiana

Muigizaji Chipukizi Bora wa Kiume (Best New And Upcoming Actor)

1. Emmanuel Muyamba – Fake Pastors

2. Laurent Anthony – Karibu Paradiso

3. Hassan Nguleni – Body Guard

4. Yussuf Mlela - Diversion Of Love

5. Uswege – Malipo ya Usaliti

Muigizaji Bora wa Kiume (Best Actor)

1. Single Mtambalike – Agano la Urithi

2. Nurdin Mohamed – Utata

3. Jacob Steven – Copy

4. Haji Adam – Miss Bongo

5. Yussuf Mlela - Diversion Of Love

Mapambo na Maleba Bora (Best Costume And Makeup of The Year)

1. Misukosuko II

2. Macho Mekundu

3. Kolelo

4. Utata

5. Copy


Mtunzi Bora wa Filamu (Best Creater of The Year)

1. Lucy Komba – Utata

2. Nicholaus Mtitu - Diversion Of Love

3. Single Mtambalike – The Stranger

4. Halfan Ahmed – Copy

5. Hammie Rajab – Kolelo

Filamu Bora ya Mwaka (Best Movie of The Year)

1. Behind the Scene

2. The Stranger

3. Diversion Of Love

4. Macho Mekundu

5. Misukosuko II

6. Simu ya Kifo

7. Copy

8. My Sister

9. Silent Killer

10. Miss Bongo I

11. Agano la Urithi

12. Malipo ya Usaliti

13. Utata

14. Kilio Moyoni (Crying Silently)

15. Fake Pastors

Wednesday, May 21, 2008

Samaki Mkunje Angali Mbichi!





UTATA WA KIFO CHA BALALI!

Katika kupigana 'scoop', gazeti la Tanzania Daima limeweka historia ya pekee kwa kuweza kuchapa habari nzito kama hii na kuwa gazeti pekee lenye habari hiyo leo asubuhi, hivyo kulifanya liuzike kama 'njugu'. Si Serikali wala Benki Kuu waliokuwa na taarifa juu ya suala hili. Hata hivyo kuna maswali mazito na utata mtupu umegubika kifo cha Balali.
Baadhi ya maswali magumu:
KWA NINI KIFO CHAKE KIMEKUWA SIRI KWA MUDA WA SIKU TANO?
NI KWELI SERIKALI ILIKUWA HAINA TAARIFA YA KIFO CHAKE?
NA KAMA WALIJUA, KWA NINI WALIAMUA KUFANYA SIRI?
BAADA YA KUCHELEWA NA HATIMAYE KUTOA TAARIFA YA KUTHIBITISHA KWELI BALALI KAFA, BOT HAWAKUWA NA TAARIFA ZAIDI YA KUSEMA WANAUNGANA NA NDUGU NA JAMAA KATIKA MSIBA HUU, WHY?!!!!
Tanzania Daima wanastahili pongezi, Uhuru wa Media nchini unafanyakazi yake! HAKUNA SIRI!

Tuesday, May 20, 2008

WABONGO SASA SAUZI NOMA!





Nchini Afrika Kusini (Sauzi) kumezuka mapigano makali, wenyeji wanawauwa na kuwachomea nyumba zao 'wageni' ambao ni weusi wenzao kwa madai kuwa 'wanawamalizia' kazi. Sheshe hili, linaripotiwa kuanza Jumatatu wiki hii na walioathirika sana ni Wazimbabwe ambao wanakimbia soo lililoko kwao hivi sasa! Watu 22 washavuta na zaidi ya 200 wameshajeruhiwa vibaya katika vitongoji vya Jo'Burg! kifupi hali ni mbaya kama picha zinavyojionesha na hatujui kama Wabongo wenzetu walioko huko wanaweza kusalimika!

HATUKUUMWA ILI TUUGUWE -2

You Are What You Eat!
Wiki iliyopita tulianza makala haya kuhusu ukweli kwamba binadamu ameumbwa ili aishi bila kuandamwa na maradhi. Tunaelezwa kwamba kuugua, ugonjwa wowote, huwa kunatokana na kukiuka kwa sheria za mwili (physical laws) zilizowekwa na Mungu mwenyewe….endelea..

UTAKAPOUGUA UFANYE NINI?

Naweza kusema kuwa tatizo kubwa tulilonalo ambalo linatusumbua ni kutokujua jinsi ya kutibu miili yetu pale tunapougua. Katika suala la ugonjwa, kabla ya kupata tiba, chanzo cha ugonjwa lazima kieleweke. Mazingira machafu yabadilishwe, ulaji usio sahihi uachwe kisha mwili usadiwe kujisafisha wenyewe kwa kuondoa sumu mwilini kwa kutumia dawa zisizo na madhara zikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na vyakula sahihi.

Unapopatwa na ugonjwa, ikiwa ni matokeo ya ukiukwaji wa zile kanuni za mwili, swali la kwanza kujiuliza ni nini kimesababisha ugonjwa huo, kwa sababu hakuna ugonjwa usiokuwa na chanzo. Jiulize; ‘nimefanya nini mpaka nimeugua’? Mwanzoni swali hilo linaweza kuwa gumu na usipate jibu, lakini ukizoea na ukiwa makini na vitu unavyokula kila siku, jibu hupatikana kirahisi.

Baada ya kujua nini kimesababisha ugonjwa wako, ondoa sababau hiyo na acha kula au kufanya jambo hilo kisha anza kujitibu kwa kutumia dawa asilia ambazo zitakusaidia kuondoa sumu iliyoko mwilini na bila kukuletea madhara mengine. Jambo la kuzingatia hapa ni kuepuka matumizi ya dawa zisizo sahihi kutibu ugonjwa ulionao, kwani badala ya kutibu unaweza kuwa unajiongezea maradhi mengine zaidi.

Baada ya kuelezea kwa kirefu kanuni za mwili, tuangalie vitu muhimu vitatu anavyopaswa kuvitumia binadamu kila siku kutokana na umuhimu wake katika kufikia lengo la kuwa na afya bora:

1. MAJI

Sumu hurundikana mwilini tunapokuwa hatuna maji ya kutosha. Mtoto mchanga aliyezaliwa leo, asilimia 80 ya mwili wake huwa maji. Kiwango cha maji kwenye tishu hupungua kadri mwili unavyoongezeka hadi kufikia asilimia 60 kwa mtu mzima.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, binadamu aneweza kuishi hadi siku 81 bila kula, lakini hufa anapokosa maji kwa muda wa siku 5 tu! Mtu anapopoteza asilimia 5 ya maji mwilini, hubadilika na hueza kuanza kuweweseka, misuli kushikana na kukosa mwelekeo na akipoteza maji kwa asilimia hadi 15 maisha yake huwa hatarini na kupoteza maji kwa zaidi ya asilimia 15 mtu huweza kufa!

Katika suala hili la maji, naomba nisherehesha vya kutosha, kwani ni jambo muhimu na nyeti sana ambalo watu wengi hulipuuza na hawajui kuwa ndiyo chanzo cha matatizo mengi ya kiafya. Kwa kawaida mwili huwa hauweki akiba ya maji, hivyo huhitaji maji wakati wote na yanapokosekana athari zake huonekana upesi.

Watu wengi wamezoea kunywa maji pale wanaposikia kiu, hawana utaratibu wa kunywa kiwango cha maji kinachopendekezwa na wataalam wa afya cha lita moja na nusu hadi tatu kila siku. Unapofikia hatua ya kusikia kiu ni dadlili kwamba tayari mwili wako umepungukiwa maji. Mwili wa binadamu ni sawa na gari ambalo likiishiwa maji huweza kusababisha injini kufa!

Ili kujua umuhimu wa maji, unapaswa kuzijua dalili zinazojitokeza mwili unapopungukiwa maji. Sehemu za mwanzo kuathirika na upungufu huo ni zile zisizokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mzunguruko wa mishipa (Vascular circulation) kama vile magoti, viongio vya vidole na uti wa mgongo.

Maumivu yanayojitokeza sehemu hizo, ambayo huja na kuondoka, huwa ni matokeo ya mwili kuwa na upungufu sugu wa maji. Unapokabiliwa na hali kama hiyo, wazo la kwanza kukuingia akilini liwe “mwili wangu una tatizo sugu la maji”.

Kwa bahati mbaya sana, watu wanaokabiliwa na matatizo kama hayo katika hatua za awali huzipuuzia, ama kwa kutokujua au kwa kutojali, badala yake hukumbilia hospitali ambako huandikiwa dawa za kupunguza maumivu na kuacha tatizo la msingi likiendelea kujiiimarisha mwilini na hatimaye kuharibu mifupa ya sehemu hizo.

Kwa majibu wa Dk. Fereydoon Batmanghelidj, upungufu wa maji mwilini unaweza kusababisha maradhi mengine na kukauka kwa midomo siyo dalili pekee za kuishiwa maji mwilini, mtu kusubiri mpaka usikie kiu ndiyo unywe maji si sahihi.

Maumivu ya ndani ya viungo mara nyingi huwa ni kilio cha mwili ukiomba maji, mwili hujaribu kukufikishia ujumbe kuwa “nimeishiwa maji” na hupaswi kusikia kiu ndiyo unywe maji, bali kiu inapaswa kuzuiwa isitokee. Mwili unapokuwa haupokei maji ya kutosha lazima utasikia maumivu ya viungo.

“Maumivu ya mwili, ambayo hayawezi kuelezewa na mgonjwa kama yanatokana na kuumia au maambukizo ya ugonjwa, yaelezwe kama ni upungufu wa maji katika sehemu zenye maumivu, hivyo si vyeme mgonjwa kupewa dawa ambazo zitafanya tatizo kukua,” anaeleza zaidi Dk. Batmanghelidj.
ITAENDELEA WIKI IJAYO

Monday, May 19, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Hot Corner with YP
Kutoka ndani ya kundi la TMk Wanaume Family, Hot Corner imembamba Yessaya Ambilikile ‘YP’, ambaye hukamua na swahiba wake, Y-Dash na wameshadondoka na albamu yenye jina la Mapengo Matatu yenye kazi kibao. Twende chini, tucheki na YP.
Hot Corner: Inakuwaje YP?
YP: Fresh, Mungu anasaidia.
Hot Corner: Unajisikiaje kuwa maarufu?
YP: Yaani mzuka, ‘nafil’ sana.
Hot Corner: Nani muhimu zaidi katika maisha yako?
YP: Ni mwanangu Ambilikile.
Hot Corner: Mbali na muziki, kitu gani kingine unapenda?
YP: Kufanya biashara.
Hot Corner: Mke mwenye sifa zipi utamweka ndani?
YP: Msikivu na mtulivu.
Hot Corner: Unapenda kuwa kama nani wa Tanzania?
YP: Kama Bakhresa.
Hot Corner: Unautumia vipi muda wako wa mapumziko?
YP: Kulala ili kutuliza akili yangu.
Hot Corner: Aksante kwa ushirikiano wako mtu wangu.
YP: Haina kwele, tuko pamoja.



**********************************************
Mzee Benz, Akudo Impact walivyofunika Bongo



Vijana wa masauti

Sunday, May 18, 2008

KIPIMA MACHO!

Hapa ni ndani ya ukumbi wa Diambond Jubilee kama kulivyotayarishwa juzi kwa ajili ya VIP ili kuona onesho la Akudo Impact. Ni picha inayoonesha ubunifu wa kutumia 'angle' na kupiga picha. kwa wale wapiga picha, mnaweza kujua mpigaji alitumia 'settings' gani na ali 'position' wapi camera kupata picha kama hii? Ni kipima macho tu!