Wednesday, May 21, 2008

UTATA WA KIFO CHA BALALI!

Katika kupigana 'scoop', gazeti la Tanzania Daima limeweka historia ya pekee kwa kuweza kuchapa habari nzito kama hii na kuwa gazeti pekee lenye habari hiyo leo asubuhi, hivyo kulifanya liuzike kama 'njugu'. Si Serikali wala Benki Kuu waliokuwa na taarifa juu ya suala hili. Hata hivyo kuna maswali mazito na utata mtupu umegubika kifo cha Balali.
Baadhi ya maswali magumu:
KWA NINI KIFO CHAKE KIMEKUWA SIRI KWA MUDA WA SIKU TANO?
NI KWELI SERIKALI ILIKUWA HAINA TAARIFA YA KIFO CHAKE?
NA KAMA WALIJUA, KWA NINI WALIAMUA KUFANYA SIRI?
BAADA YA KUCHELEWA NA HATIMAYE KUTOA TAARIFA YA KUTHIBITISHA KWELI BALALI KAFA, BOT HAWAKUWA NA TAARIFA ZAIDI YA KUSEMA WANAUNGANA NA NDUGU NA JAMAA KATIKA MSIBA HUU, WHY?!!!!
Tanzania Daima wanastahili pongezi, Uhuru wa Media nchini unafanyakazi yake! HAKUNA SIRI!

1 comment:

Anonymous said...

Ni kweli kabisa, hata mimi naungana na wewe kwa asilimia mia moja. Hii serikali sijui vipi, mi nawasiwasi nchi imeshauzwa lakini tumnafichwa tu!
Si waseme kama wameuza watugaie pesa zetu? Nchi hii bwana ah!!!
Mdau wa kudumu