Friday, January 23, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

TOP 3: Rose Ndauka nje!

Hatimaye warembo watatu wamefanikiwa kuingia kwenye hatua ya tatu bora (Top 3),kunako shindano la Ijumaa Sexiest Girl baada ya mshiriki mmoja, Rose Ndauka, kutupwa nje ya mpambano, sababu ikiwa ni kupata kura chache kutoka kwa majaji ambao ni wasomaji.

Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye hatua hii muhimu ni Irene Uwoya, Hadija Sure na Wema Sepetu. Mmoja kati ya warembo hawa anawania taji la staa wa kike mwenye mvuto wa kimapenzi ‘Ijumaa Sexiest Girl’ ambalo hivi sasa linashikiliwa na Jokate Mwegelo.

Mratibu wa shindano hili, Oscar Ndauka alisema kwamba, anawashukuru wasomaji ambao bado wanaendelea kutoa sapoti kwa kutuma maoni yao katika mpambano huu tangu ulipoanza. “Tunawaomba waendelee kutuma kura zao kwa kuandika ujumbe mfupi (SMS) wakimtaja mshiriki ambaye wanadhani anastahili kuibuka na ushindi, kisha watume kwenda simu namba +255 784-275 714,” alisema.
Ngwea Yuko pande za Uganda, kupiga kazi na Chameleone

Akiwa Kampala, nchini Uganda, msanii Albert Mangwea ‘Ngwea’ alipiga stori na ShowBiz kwa njia ya simu juzi na kutamka kwamba yupo nchini humo kwa ajili ya kurekodi ngoma kadhaa ili kujiweka fiti mwaka 2009.

Ngwea alisema kwamba tayari amesharekodi kazi kadhaa, imebaki moja yenye jina la ‘weekend’ ambayo itamshirikisha Joseph Mayanja ‘Chameleone’ ambaye hivi karibuni alipata ajali ya gari.

“Siku yoyote kuanzia leo tutafanya kazi kwasababu Chameleone hivi sasa amepata nafuu, anaweza hadi kuendesha gari, hatembelei magongo tena kama ilivyokuwa wakati ameumia. Vile vile tayari nimeshafanya video za nyimbo zangu mbili, ‘Nipe Dili’ na ‘120’ kupitia Kampuni ya Visualab, zitatoka pamoja wiki hii.”

Ndani ya ngoma yake hiyo mpya, 120 aliyompa shavu Chid Benz, Ngwea ‘amewachana’ baadhi ya wasanii walioshindwa kufanya kazi na kuamua kuwasema wenzao vibaya. Ndani ya kazi hiyo mchizi ameonesha uwezo mkubwa wa kucheza na sauti.
*******
Soggy aibukia kwa Mwana FA

Baada ya kupotea kunako game ya muziki kwa muda sasa, mchizi kutoka ndani ya Familia ya Hot Port, Hanselem Tryphone Ngaiza, ‘Soggy Dog’ (pichani chini) ameibukia kwenye video ya wimbo mpya wa msanii Hamis Mwinjuma ‘Mwanafalsafa’ unaokwenda kwa jina la ‘Msiache kuongea’, uliyomshirikisha Judith Wambura ‘Lady Jaydee’.

Showbiz ambayo ilikuwepo kwenye zoezi la upigaji picha za video hiyo ambalo lilifanyika maeneo ya Msasani, Dar es Salaam ilimshuhudia Soggy pamoja na mastaa wengine kibao wakijiachia mbele ya kamera za Adam Juma wa Kampuni ya Visualab aliyefanya kazi hiyo.

Kwa mujibu wa ‘FA’, video hiyo itadondoka kideoni siku chache zijazo, ikiufuatia wimbo huo ambao tayari umeanza kusikika kupitia vituo kadhaa vya redio, ukiitambulisha albamu yake mpya, Mabibi na Mabwana itakayokuwa na ngoma zaidi ya tisa.

********
compiled by: mc george

No comments: