mwanzo mpya ya tht inabamba mbaya
Taasisi ya kukuza na kuendeleza Vipaji vya wasanii wachanga, Tanzania House of Talent ‘THT’, tayari imeangusha kitaani filamu yao mpya inayokwenda kwa jina la Mwanzo mpya, ambayo imewashirikisha mastaa kibao wakiwemo wasanii wenye uwezo wa kutosha.
Ikiwa imefanyika kupitia Kampuni ya Bani Vision, muvi hiyo ambayo inafanya vyema sokoni tangu ilipodondoka siku chache zilizopita imewashirikisha wasanii kama Banana Zorro, H. Baba na Dj ambaye pia ni mtangazaji maarufu wa Redio Clouds FM, Mully B.
Mratibu wa Maonesho na Masoko wa THT, Michael Nkya, alisema na safu hii kwamba, filamu hiyo pia imewashirikisha wasanii chipukizi wanaotisha kunako game hiyo ambao ni Islam Awadh, Kauye Dotto, Stephen Joseph (Jobiso) na Msami, ambao wameonesha maujuzi ya kutosha yakiwemo yale waliyofundishwa na waalimu wao.
“Maudhui ya filamu hiyo yanagusa maeneo mengi yakiwemo Mapenzi, Ushirikina, Umuhimu wa Urafiki, Usaliti na mambo mengi kibao, nawataka Watanzania waichungulie ili wajifunze mambo mengi zaidi, ikiwa ni pamoja na kupata burudani,” alisema.
Afande Sele kurudi kideoni
Kutoka pande za Moro, msanii Selemani Msindi ‘Afande Sele’ mapema wiki hii atadondosha hewani video ya ngoma yake yenye jina la ‘Mbele yako’ aliyomshirikisha kijana kutoka Mkuranga, Mkoani Pwani, Hamisi Kinzasa a.k.a 20%, Edna Katabalo alipiga naye stori.
Akipiga stori kwa njia ya simu na upande huu wa burudani, Afande alitamka kwamba vurugu hizo zote ni utambulisho wa albamu yake mpya ambayo hakupenda kuitaja jina kwa sasa kwakuwa bado anaweka sawa baadhi ya mambo.
“Kiukweli video imetulia, nimefanya kitu ambacho mashabiki wangu watakifurahia, kawaida yangu huwa sibahatishi hasa ninapofanya kazi na kampuni ya Empty Souz chini ya mtayarishaji Osama. Nafahamu mashabiki wangu wanataka nini,” alisema Afande.
Aidha, Afande aliimegea safu hii kwamba, pamoja na kuwa bize akiandaa video hiyo, pia yupo kwenye mishemishe za kukamilisha albamu ya kundi lao ambayo inatarajiwa kuwa kitaani ndani ya Sikukuu ya Pasaka
Chegge kuanika maisha ya kiumeni
Baada ya kufanya poa na kazi yake, ‘Goodbye’, msanii kiraka wa kutoka kundi la TMK Wanaume Family lenye maskani yake pande za Temeke, Dar es Salaa, Said Juma a.k.a Chegge Chibinda’ au Mtoto wa Mama Saidi’ anatarajia kuachia ngoma nyingine yenye jina la ‘Kiumeni’.
Chegge ameimegea safu hii kwamba ndani ya ‘pini’ hilo amefanya bonge la kolabo na ‘Cow Boy’ wa East Zoo, Arbert Mangwea a.k.a Mimi, pamoja prodyuza makini kutoka studio za 41, Ambrose Dunga ambaye ndiye aliyetengeneza kazi hiyo.
“Ndani ya kazi hiyo nimemueleza demu wangu maisha halisi ninayoishi Kiumeni na machizi wangu, masela wangu, ndugu zangu na jamaa zangu. Nataka mpenzi wangu huyu afahamu kichaa naishi vipi,” alisema Chegge na kuongeza kwamba siku yoyote wimbo huo utaanza kulindima hewani.
Wakati Chegge akijiandaa kuchomoka na kazi hiyo, kundi lake, TMK Wanaume Family pia linatarajia kuachia hewani wimbo mpya wenye jina la ‘Wanaume Kazini’ ili kuupotezea mwaka huu wa 2009.
Celine Dion: Miaka 41, wanaume wawili tu, bonge la mjanja!
Anayeuza leo ndani ya ‘Ebwana Dah’ ni mwanamuziki aliyepata kutingisha na ngoma kibao za R&B, ikiwemo Titanic, Celine Marie Claudette au Celine Dion ambaye kiukweli pamoja na kuwa na umri mkubwa wa miaka 41 hivi sasa na tangu ameukwaa ustaa amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wawili tu.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘intaneti’, Celine amewahi kujiachia na mchizi anayekwenda kwa jina la Peabo Bryson (anayeonekana katika picha ndogo hapo juu) na baada ya hapo alijiweka kwa mzee mzima, Rene Angelil ambaye ndiye mumewe wa ukweli hadi hii leo kama wanavyonekana kunako picha hiyo kubwa.
Celine ambaye alizaliwa Machi 30, 1968 Charlemagne nchini Canada, wazazi wake wakiwa ni Dion Adhemar ambaye ni baba, huku mama yake akiitwa Tanguay Therese, alifunga ndoa na Rene Desemba 17, 1994 huko Montreal, Quebec, Canada na hivi sasa wana mtoto mmoja mwenye jina la Angelil Rene-Charles.
Ebwana dah, inamuona staa huyo bonge la mjanja, kwani ni tofauti na mastaa wengine wa kike ambao wana listi ndefu ya wanaume waliyowahi kujiachia nao siku za nyuma. Tuambie, unataka kufahamu uhusiano wa kimapenzi wa staa gani na wanaume au wanawake wengine siku za nyuma? Tutumie ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu 0715-110 173.
compiled by: mc george

No comments:
Post a Comment