Kila mtu anakula chakula kulingana na mahitaji ya mwili wake. Mbeba zege, hawezi kula sawa na anayefanyakazi ya kukaa ofisini, kula kiasi ambacho kinalingana na mahitaji ya mwili wako. Kanunni ya kula inasema acha kula wakati bado hujashiba vizuri. Kwa kawaida, mahitaji ya chakula ya mwili ni kiasi cha ‘kalori’ 2000 kwa siku, ikitegemeana na umri, jinsia, urefu, uzito na kazi anazozifanya mtu.
KULA VYAKULA MCHANGANYIKO
Ulaji sahihi ni ule wa kula vyakula mchanganyiko vya aina tofauti, hasa mboga za majani, matunda, vyakula vya nafaka ambavyo huwa huvili mra kwa mara. Kwa kula vyakula mchanganyiko utapata faida ya kuwa na virutubisho tofauti mwilini na kuondoa upungufu wowote wa vitamini unaweza kuwepo mwilini bila wewe kujijua.
KULA
Ni kawaida ya watu wengi kutokula matunda kabisa katika staili
Hivyo hakikisha siku haipiti bila kula matunda na mboga. Kiwango kinachopendekezwa na Shirika la Afya Duniani, ni kwa mtu mmoja kula milo ya matunda na mboga mboga kati ya 4 – 6 kwa siku, mlo mmoja unaweza kuwa sawa na ujazo wa kisahani cha chai.
KUNYWA MAJI MENGI
Imeelezwa na wataalamu wetu kuwa asilimia 75 ya mwili wa binadamu ni maji. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku nayo ni sehemu ya ulaji sahihi. Maji ndiyo yanayosaidia kusafisha mifumo ya mwili na kutoa nje uchafu na sumu, hasa kwenye kibofu cha mkojo na figo. Watu wanaopatwa na matatizo ya viungo hivyo ni wale wenye tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.
Iwapo utazingatia ulaji sahihi, bila shaka utakuwa huru kula mara moja moja vyakula vingi, hata vya kukaanga bila kupata matatizo yoyote. Kwani chakula ni chanzo kizuri cha furaha na mtu mwenye furaha hujiepusha na magonjwa ya moyo pia. Hivyo zingatia ulaji sahihi ili uwe huru wa kula vyakula vya aina vyote katika kiwango kinachokubalika.
JISHUGHULISHE
Mwisho, ili lishe yako au ulaji wako sahihi ufanyekazi yake vizuri na kukupa afya njema, lazima ufanye mazoezi au ujishughulishe na kazi mbalimbali za kila siku. Kula vizuri bila kuushughulisha mwili, hakuwezi kuwa na faida kiafya. Aihda katika hili, mambo 3 hayana budi yazingatiwe, nayo ni Lishe Bora, Mazoezi na kupumzika.
No comments:
Post a Comment