Wednesday, June 10, 2009

HEBU SOMENI NA HII NAYO...

Kwanza pole sana.
Hii habari nimeikubali kwa asilimia mia moja, kwani nami nina katukio nilichosimuliwa na ndugu yangu mmoja kidogo kinafanania na tukio hili.
Mwezi uliopita yaani May kuna ndugu yangu mmoja (msichana) katika familia alikuwa akitokea Dubai kuja Bongo.
Tazama jinsi hawa wezi wasivyo hata na chembe ya aibu.... akiwa katika safari yake hiyo kwa kutumia shirika la ndege la Kenya Airways aliketi katika seat ya abiria watatu akiwa peke yake na seat ya nyuma yake aliketi mzee wa makamo na kutokana na mavazi ya huyo mzee mara moja alimtambua kuwa ni raia au mtu mwenye asili ya kinaijeria.
Alimsabahi wakati anaketi na mara wakati ndege inataka kuruka ndugu yangu huyo alitoa simu zake mbili katika mkoba ili azi switch off(si unajua tena sheria za urukaji wa ndege)
Cha ajabu wakati anafanya hivyo (kuzima simu) aligeuka nyuma na kumuona yule mnaijeria akimpungia mkono (waving) na ghafla akajihisi kupata usingizi wa ghafla na kupoteza nguvu kabisa. Binti huyu ni mtu wa dini kidogo na alipohisi hali ile alianza kuomba na kusali kwani alihisi lile tukio halikuwa la kawaida.
Na kweli baada ya kama dakika 3 alizinduka toka katika ule usingizi wa ajabu na katika hali ya kushangaza hakuwa na simu hata moja mkononi.
Aliomba msaada kwa air hostess na kueleza tatizo lake na walipochungulia chini ya seat hakukuwa na dalili ya simu kudondoka kwani mkoba wake bado alikuwa ameushikilia mkononi.
Binti alikuja juu na kutaka habari ile ajulishwe pilot ili hatua za kufanya searching zichukue mkondo wake. "Inauma kwa kweli simu mbili tena Nokia N96 na Nokia Express Music 5800 touch screen, zipotee katika mazingira ya kutatanisha lazima ipigwe search" binti alilalama
Sasa kabla habari haijafika kwa pilot, kumbuka simu zilitazamwa chini ya seat hazikuwepo eti yule mbaba wa Kinaijeria tena bila hata woga wala wasiwasi akasimama na kusema kwa sauti " Here look , whose phones are these?? i just found them passing by my feet" !!!
Ndugu yangu hakuwa na comment alisema tu ahsante mzee wangu.
Ila kwa kweli yale yalikwa ni mauzauza na kama hakuwa ameamka vizuri siku ile basi ilikuwa inakula kwake, simu zingekwenda kweli hivyo!!!
Tuji

(
Dingituka Toboatobo)

No comments: