Wateule
Mack 2B: Wakati washikaji wanaingiza voko za ‘Msela’ nilikuwa Milembe
Kutokana na maswali yaliyojaa vichwani mwa wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya pamoja na wasomaji wa ShowBiz kuhusiana na kukosekana kwa sauti ya Mark 2B au Simba kwenye ngoma mpya ya Wateule, ‘Msela’ huku akiwa ni memba wa kundi hilo, safu hii ilijaribu kumtafuta na kupiga naye stori mbili tatu kuhusiana na hilo.
Mchizi ambaye jina lake kamili ni Malick Ahmed Mohamed anayegonga mzigo ndani ya studio za Bacyard Records hivi sasa, alisema kuwa wakati washkaji wanaingiza voko kwenye ngoma hiyo ambayo iko mstari wa mbele ikiwarudisha vyema yeye alikuwa katika Hospitali ya Milembe, Mkoani Dodoma akimalizia matibabu.
“Najua wengi watahoji kwanini sijasikika kwenye kazi hiyo wakati na mimi ni ‘Mteule’, lakini huu ndiyo ukweli. Tangu Aprili mwaka jana nilipatwa na ugonjwa wa akili nikawa natibiwa Milembe Dodoma, nashukuru Mungu baada ya miezi kama sita nikarudi katika hali yangu ya kawaida, niliporudi Dar nikakuta jamaa wapo kwenye harakati za kukamilisha ngoma hiyo.
“Nilichofanya nilitulia kwanza, siku kadhaa baadae nikaanza kazi ndani ya studio za Backyard kama unavyoniona na tayari katika kuchangia albamu ya Wateule ambayo itadondoka kitaani hivi karibuni nimeshafanya kazi moja na Jay Moe yenye jina la ‘Ashura,” alisema Mark 2B ambaye kabla ya kuugua alikuwa akipiga mzigo ndani ya studio za Soundcrafters.
Kwa upande wa Jafarai ambaye pia ni memba wa kundi hilo alisema kwamba kazi hiyo ya wateule ambayo ilifanyiwa ‘mix’ katika studio za Fish Crab kwa Ramah imefanywa na Mox, Jay Moe, yeye mwenyewe na Solo Thang ambaye yupo Uingereza ambaye alitumiwa ‘bit’ akaingiza voko kisha kazi ikarudishwa Bongo na kufanyiwa mix. Mbali na wasanii hao kufanya vyema kwenye ngoma hiyo, kwa niaba ya wasomaji ShowBiz inahoji kwamba, wako wapi wasanii wengine wa kundi hilo, Lady Lou na Kelvin?
Pamoja na kuviambia baadhi ya vyombo ya habari kwamba, siku chache zijazo ataipiga chini ajira yake ya muziki na kuendelea na ishu nyingine, msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na ngoma mpya yenye jina la ‘Nipe Love’ akishirikiana na kichwa kimoja kutoka ndani ya kundi la Rackaz, Quick Racka, Zubagy Akilimia anashuka nayo.
ShowBiz imepewa ishu kwamba, goma hilo ambalo tayari limeanza kusumbua kunako anga ya muziki wa kizazi kipya limegongwa ndani ya Studio za MJ chini ya mtayarishaji Maco Chali ambaye ‘staa’ yake ilianza kung’aa tangu alipokuwa akipiga kazi Kama Kawa Records.
Kama wewe ni mdau wa ukweli kunako ‘bizinesi’ hii ya muziki wa kizazi kipya utagundua kwamba, ‘Ray C’ akishirikiana na mchizi huyo wamefanya mapinduzi mengine katika muziki huo kwani ngoma hiyo ipo katika staili na levo nyingine. Kula ‘gwara’ mwanadada kwa kuonesha kuwa ‘still u can do’.
Kingwendu ni mmoja wa wachekeshaji wa Kibongo waliopata kupiga stori na ShowBiz wiki hii na kudodosha ishu kwamba, japo tayari ameshafanikiwa kupata watoto watatu huku ‘waifu’ wake bado yupo kwenye mishe mishe za kutafuta mtoto wa nne kwa kuwa anaamini anaweza kulamba dume kwani alio nao wote ni wa kike.
Mchizi ambaye jina lake kamili ni Rashidi Mwinshehe Said alisema kuwa hata kama ikitokea akapata mtoto wa kike tena siyo mbaya kwani itakuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu. Lakini mbali na yote hiyo siyo ishu sana zaidi yupo kwenye mazoezi makali ya kujiandaa na mpambano wake na Dickson Makwaya ‘Bambo’ utakaopigwa ndani ya Ukumbi wa Dar West uliopo Tabata, Dar es Salaam.
“Wasanii hao watapambana katika ziara tuliyoipa jina la ‘Nani mkali’ kati ya wasanii hao, shoo ya kwanza itapigwa Juni 19, mwaka huu na siku itakayofuata yaani Juni 20 itakuwa katika Ukumbi wa Kontena, Kibaha, mkoani Pwani,” alisema Braton wa Backyard Records ambao ndiyo waandaaji.
Aidha Braton alisema kwamba, wasanii kibao kama Q-Jay, Mkoloni, Dk. Kumpeneka na wengine watatoa sapoti kwa wachekeshaji hao, huku mshindi akiondoka na zawadi ya gari.
Mack 2B: Wakati washikaji wanaingiza voko za ‘Msela’ nilikuwa Milembe
Kutokana na maswali yaliyojaa vichwani mwa wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya pamoja na wasomaji wa ShowBiz kuhusiana na kukosekana kwa sauti ya Mark 2B au Simba kwenye ngoma mpya ya Wateule, ‘Msela’ huku akiwa ni memba wa kundi hilo, safu hii ilijaribu kumtafuta na kupiga naye stori mbili tatu kuhusiana na hilo.
Mchizi ambaye jina lake kamili ni Malick Ahmed Mohamed anayegonga mzigo ndani ya studio za Bacyard Records hivi sasa, alisema kuwa wakati washkaji wanaingiza voko kwenye ngoma hiyo ambayo iko mstari wa mbele ikiwarudisha vyema yeye alikuwa katika Hospitali ya Milembe, Mkoani Dodoma akimalizia matibabu.
“Najua wengi watahoji kwanini sijasikika kwenye kazi hiyo wakati na mimi ni ‘Mteule’, lakini huu ndiyo ukweli. Tangu Aprili mwaka jana nilipatwa na ugonjwa wa akili nikawa natibiwa Milembe Dodoma, nashukuru Mungu baada ya miezi kama sita nikarudi katika hali yangu ya kawaida, niliporudi Dar nikakuta jamaa wapo kwenye harakati za kukamilisha ngoma hiyo.
“Nilichofanya nilitulia kwanza, siku kadhaa baadae nikaanza kazi ndani ya studio za Backyard kama unavyoniona na tayari katika kuchangia albamu ya Wateule ambayo itadondoka kitaani hivi karibuni nimeshafanya kazi moja na Jay Moe yenye jina la ‘Ashura,” alisema Mark 2B ambaye kabla ya kuugua alikuwa akipiga mzigo ndani ya studio za Soundcrafters.
Kwa upande wa Jafarai ambaye pia ni memba wa kundi hilo alisema kwamba kazi hiyo ya wateule ambayo ilifanyiwa ‘mix’ katika studio za Fish Crab kwa Ramah imefanywa na Mox, Jay Moe, yeye mwenyewe na Solo Thang ambaye yupo Uingereza ambaye alitumiwa ‘bit’ akaingiza voko kisha kazi ikarudishwa Bongo na kufanyiwa mix. Mbali na wasanii hao kufanya vyema kwenye ngoma hiyo, kwa niaba ya wasomaji ShowBiz inahoji kwamba, wako wapi wasanii wengine wa kundi hilo, Lady Lou na Kelvin?
********** **********************
Ray C, Quick, Racka ndani ya Nipe mimiPamoja na kuviambia baadhi ya vyombo ya habari kwamba, siku chache zijazo ataipiga chini ajira yake ya muziki na kuendelea na ishu nyingine, msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na ngoma mpya yenye jina la ‘Nipe Love’ akishirikiana na kichwa kimoja kutoka ndani ya kundi la Rackaz, Quick Racka, Zubagy Akilimia anashuka nayo.
ShowBiz imepewa ishu kwamba, goma hilo ambalo tayari limeanza kusumbua kunako anga ya muziki wa kizazi kipya limegongwa ndani ya Studio za MJ chini ya mtayarishaji Maco Chali ambaye ‘staa’ yake ilianza kung’aa tangu alipokuwa akipiga kazi Kama Kawa Records.
Kama wewe ni mdau wa ukweli kunako ‘bizinesi’ hii ya muziki wa kizazi kipya utagundua kwamba, ‘Ray C’ akishirikiana na mchizi huyo wamefanya mapinduzi mengine katika muziki huo kwani ngoma hiyo ipo katika staili na levo nyingine. Kula ‘gwara’ mwanadada kwa kuonesha kuwa ‘still u can do’.
************
Kingwendu atafuta mtoto wa nneKingwendu ni mmoja wa wachekeshaji wa Kibongo waliopata kupiga stori na ShowBiz wiki hii na kudodosha ishu kwamba, japo tayari ameshafanikiwa kupata watoto watatu huku ‘waifu’ wake bado yupo kwenye mishe mishe za kutafuta mtoto wa nne kwa kuwa anaamini anaweza kulamba dume kwani alio nao wote ni wa kike.
Mchizi ambaye jina lake kamili ni Rashidi Mwinshehe Said alisema kuwa hata kama ikitokea akapata mtoto wa kike tena siyo mbaya kwani itakuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu. Lakini mbali na yote hiyo siyo ishu sana zaidi yupo kwenye mazoezi makali ya kujiandaa na mpambano wake na Dickson Makwaya ‘Bambo’ utakaopigwa ndani ya Ukumbi wa Dar West uliopo Tabata, Dar es Salaam.
“Wasanii hao watapambana katika ziara tuliyoipa jina la ‘Nani mkali’ kati ya wasanii hao, shoo ya kwanza itapigwa Juni 19, mwaka huu na siku itakayofuata yaani Juni 20 itakuwa katika Ukumbi wa Kontena, Kibaha, mkoani Pwani,” alisema Braton wa Backyard Records ambao ndiyo waandaaji.
Aidha Braton alisema kwamba, wasanii kibao kama Q-Jay, Mkoloni, Dk. Kumpeneka na wengine watatoa sapoti kwa wachekeshaji hao, huku mshindi akiondoka na zawadi ya gari.
**********
Zanzibar wapewa shavu Tollywood
Baada ya wasanii wengi kujitokeza Dar es Salaa, Tanga, Morogoro, Arusha kwa ajili ya kuchukua fomu za kushiriki kunako filamu mpya, ‘Tears on Valentine Day’ inayoandaliwa na Kampuni ya Tollywood Movies, Zanzibar nayo imepewa shavu hilo kwa kutumiwa fomu kibao.
Mkurugenzi wa Filamu za Tollywood, Hamie Rajab amesema na ShowBiz kwamba wameamua kuongeza wasanii wa Zanzibar baada ya kupata maombi ya wakazi wengi kutoka visiwani humo na kwamba fomu tayari zinapatikana Masomo Bookshop kwa Farouk Kharim.
“Tulipokea maombi mengi kutoka kwa wasanii wa Zanzibar pia walihitaji kushiriki kwenye filamu zetu, tukaona ni vyema kuwashirikisha kwa kuwa tunaamini nao wana vipaji kama ilivyo sehemu nyingine nchini,” alisema Hamie.
Aidha Hamie alisema kwamba, wale watakaohitaji fomu hizo kwa upande za Zanzibar wanaweza kuwasiliana na Farouk kwa simu namba 0766-464748, 0785-533533 na 0777-464748 au wanaweza kufika ofisini kwake Masomo Book Shop.
“Fomu hizo pia bado zinaendelea kutolewa kwa shilingi 5, 000 katika mikaoa ya Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam katika ofisi zetu zilizopo Sinza, Bamaga, unaweza kuwasiliana nasi kwa simu zetu ambazo ni 0784 211107 au 0784211108. Wasanii chipukizi watakaofanikiwa kupita katika usaili watashiriki kwenye filamu yetu, ‘Tears on Valentine Day’ ambayo imeandikwa na Eric Shigongo, inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwaka huu,” alisema.
Compiled by mc georgeBaada ya wasanii wengi kujitokeza Dar es Salaa, Tanga, Morogoro, Arusha kwa ajili ya kuchukua fomu za kushiriki kunako filamu mpya, ‘Tears on Valentine Day’ inayoandaliwa na Kampuni ya Tollywood Movies, Zanzibar nayo imepewa shavu hilo kwa kutumiwa fomu kibao.
Mkurugenzi wa Filamu za Tollywood, Hamie Rajab amesema na ShowBiz kwamba wameamua kuongeza wasanii wa Zanzibar baada ya kupata maombi ya wakazi wengi kutoka visiwani humo na kwamba fomu tayari zinapatikana Masomo Bookshop kwa Farouk Kharim.
“Tulipokea maombi mengi kutoka kwa wasanii wa Zanzibar pia walihitaji kushiriki kwenye filamu zetu, tukaona ni vyema kuwashirikisha kwa kuwa tunaamini nao wana vipaji kama ilivyo sehemu nyingine nchini,” alisema Hamie.
Aidha Hamie alisema kwamba, wale watakaohitaji fomu hizo kwa upande za Zanzibar wanaweza kuwasiliana na Farouk kwa simu namba 0766-464748, 0785-533533 na 0777-464748 au wanaweza kufika ofisini kwake Masomo Book Shop.
“Fomu hizo pia bado zinaendelea kutolewa kwa shilingi 5, 000 katika mikaoa ya Arusha, Tanga, Morogoro na Dar es Salaam katika ofisi zetu zilizopo Sinza, Bamaga, unaweza kuwasiliana nasi kwa simu zetu ambazo ni 0784 211107 au 0784211108. Wasanii chipukizi watakaofanikiwa kupita katika usaili watashiriki kwenye filamu yetu, ‘Tears on Valentine Day’ ambayo imeandikwa na Eric Shigongo, inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwaka huu,” alisema.
No comments:
Post a Comment