Thursday, June 11, 2009

Mike Tyson Aoa Kwa Mara ya Tatu Wiki Mbili Baada ya Binti Yake Kufariki


Thursday, June 11, 2009 5:25 AM
Bingwa wa zamani wa ndondi za uzito wa juu Mike Tyson ameoa kwa mara ya tatu wiki mbili tu baada ya kifo cha mtoto wake. Mike Tyson alifunga ndoa na mpenzi wake Lakiha Spicer jijini Las Vegas ikiwa ni wiki mbili tu baada ya mtoto wa kike kufariki baada ya shingo yake kunasa kwenye nyanya za mashine ya kufanyia mazoezi ya kukimbia.

Tyson alifunga ndoa katika jumba la kufungia ndoa la Spicer La Bella na ndoa hiyo ilifanyika bila kuwepo mgeni mualikwa yoyote, alisema mmiliki wa jengo hilo Shawn Absher.

"Kulikuwa hakuna mgeni yoyote aliyealikwa, ni bwana harusi na bi harusi pekee, Tyson alionekana mwenye furaha sana" alisema Absher.

Tyson hivi sasa ana umri wa miaka 42 wakati mke wake mpya ana umri wa miaka 32.

Wiki mbili zilizopita mtoto wa kike wa Tyson mwenye umri wa miaka minne aliyekuwa akiitwa Exodus alifariki baada shingo yake kunasa kwenye nyanya za mashine ya kufanyia mazoezi ya kukimbia nyumbani kwa mama yake Sol Xochiti ambaye alikuwa mpenzi wa Tyson kabla ya Spicer.

Waya huo ulikuwa umezungushwa kama fundo la duara na kuwekwa uking'inia nyuma ya mashine hiyo.

Haikujulikana wazi kama mtoto huyo aliteleza na kichwa chake kuingia kwenye fundo la nyaya hizo au kama alikiingiza mwenyewe halafu akashindwa kujinasua.

Exodus alikuwa ndiye mtoto wa mwisho wa Tyson kati ya watoto wake sita aliozaa na wake zake wa zamani ukijumlisha na mahawara zake.

Wakati tukio hilo likitokea Tyson alikuwa nje ya mji kwenye shughuli zake za kikazi.

Ndoa ya Tyson na Spicer imekuwa ni mara ya tatu kwa Tyson kufunga pingu ya maisha baada ya kuwaacha wake zake wa zamani.
(kwa hisani kubwa ya nifahamishe.com)

No comments: