Saturday, June 6, 2009

Suala la kupima UKIMWI linasemwa sana.

Tunaambiwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana, kwa kupima.

Inakuwa kama kujua afya yako ni jambo la maana sana.

Ukiangalia athari za kujua afya yako kulinganisha na faida, utaona
jinsi ambavyo tendo hilo la kupima halina msaada mkubwa kama
inavyosikika.

Kuishi maisha ya kutokuwa na hakika na uwapo wa wadudu hao mwilini,
hakuwezi kukuathiri kama pale unapokuwa unajua ubomoaji wa seli
unaendelea mwilini. Ni rahisi kuanza kuugua kabla ya wakati, kitu
ambacho
kisingekuwapo kama ungesingejua.
Faida iko wapi?

Kujua kwamba tayari unaumwa, kunakushawishi kujinyanyapaa mwenyewe, na
kuanza kuhisi kufakufa, jambo ambalo haliwezi kuelezeka kama faida.

Ni kama unapokunywa maji yasiyochemshwa bila taarifa.
Huumwi tumbo.

Suala la kupima kimsingi halina maana zaidi ya kukusanya takwimu za
wagonjwa nchini.

(Maoni ya Daktari mwanafunzi, Muhimbili. Asante sana!)

2 comments:

Anonymous said...

Huyu hapashwi kuwa daktari atapotosha jamii nzima.

1. Kwa leo tuna dawa zinzosaidia kurefusha maisha. Kuna watu wanaishi na ukimwi kwa zaidi ya miaka 20. Cha muhimu ni kuugundua ugonjwa ukiwa katika stage changa + mabadiliko ya life style. Cha muhimu ni jitihada ya kuwa na strategy ya kuhakikisha kuwa kila anayehitaji dawa anapata, pia kuwaelimisha ni vipi wanaweza kuishi na ugonjwa huu. Cha muhimu dawa ziwe za bure, wasio kuwa na uwezo wapewe misaada zaidi.

Kupima ndiyo kunasaidia takwimu (kitu ambacho ni muhimu),lakini pia kunasaidia kutoambukiza wengine. Najua kuna watu wanaojigundua kuwa wamehadhirika na wanaanza kuwahadhiri wengine maksudi. Hii ni matter ya kuwaelimisha watu ili wabadilishe hii tabia na pia kuacha tabia za kuwatenga waliohadhirika.

Mfano wa wamama wajawazito, ni vizuri wakipima mapema ili waanze treatment ya kuwakinga watoto wao kuambukizwa. New patners wanafaidika wakipima kuhakikisha kuwa wote wako safi.

Je watu wasipomima na wakaendelea kuambukizana na kufa si jamii yote itakwisha?????+

Anonymous said...

Hata mimi sioni sababu ya kwenda kupima maana nikisha jua ndio nitakuwa ho bin taaban kwanza sintalala usingizi. Kwahiyo dawa ni kujilinda usitembee ovyo ovyo bila mpango. Pia kuna tatizo lingine kwa sisi wana ndoa mimi naweza kuwa nalinda lakini mwenzangu ndio kwanza kumekucha kwahiyo hilo gonjwa ni balaa tupu. Kuna watu hata ukimpigia ngoma ni bure tu anakuona kama wewe hayawani. Kwahiyo nikuomba Mungu atunusuru.