Monday, June 22, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

M-Net yashuka na bonge la tamthilia
Mwaka unaelekea ukingoni, lakini burudani zinazidi kukumwagikia hapohapo kitaani kwako. Iko hivi, saiti yako inayoongoza kwa ishuz za Entertainment barani Afrika, M-Net ambayo inatokana na Kampuni ya Multi-Choice inakudondoshea bonge la tamthilia. Ukitaka kuichungulia tamthilia hiyo, basi siyo ishu sana kama unatumia king’amuzi (decoder) cha DStv.

Kama haujaunyaka mnuso huu ni kuwa itaoneshwa kwa mara ya kwanza Juni 23, 2009, hapo tunaizungumzia kesho na itarushwa saa 2:00 jioni. Tamthilia ipo kikenya zaidi, lakini ina stori bomba kuhusu mapenzi na ndoa kwa ujumla, pia ndani yake Kijana wa Kitanzania Adam Juma (wa pili kushoto walio simama) wa Visual Lab, ambaye ametumia jina la Minja Kabwe ameuza sura na kupoteza ile mbaya. Changamkia kideo chako, hii si ya kukosa kwani ipo hewani kila Jumanne.
*********************************

Posh: hajachezewa kiviiile, penzi lake ni ishu nzito
Kupitia kona hii, juma lililopita ulimcheki Sean John Combs a.k.a P. Diddy na ufundi wake wa kubadilisha wanyange, lakini hapa yuko kivingine zaidi. Anaongelewa Victoria Adams Beckham a.k.a Posh Spice. Mmama huyu ni fundi wa kubana na penzi lake ni ishu kulipata.

Washakunaku wengi mtoni kupitia mapaparazi wa magazeti na mitandao mbalimbali walikwishafanyakazi ya ziada kufunua ni akina nani waliowahi kufaidi penzi lake, au ikiwezekana wamnase mwanaume ambaye huwa anamega kisela nje ya ndoa, lakini wapi.

Baada ya kuambulia patupu, mtandao mmoja unaodili na maisha ya uhusiano wa mastaa mbalimbali huko mbele, umeeleza kuwa Posh amewahi kutoka na wanaume wawili tu tangu kuzaliwa kwake.

Umefafanua kuwa kati ya mwaka 1995 hadi 1996, Posh alikuwa anachizika kimahaba na janki mmoja hivi anayekwenda kwa jina la Corey Haim kabla ya 1997 kuangukia kwa mwanasoka wa kimataifa wa England, David Beckham ambaye amedumu naye mpaka leo kama mke na mume na kuzaa watoto watatu.

Unaweza kumwita Victoria Beckham au Victoria Adams lakini jina lake kwa kirefu ni Victoria Caroline Adams Beckham. Ni memba wa kundi marehemu la Spice Girls, alianza kupendeza kupitia muziki lakini sasa anafunika kwenye mitindo.

Alizaliwa Aprili 17, 1974 hivyo amekwishajikusanyia umri wa miaka 35. Ana urefu wa futi 5.6.
****************************************************
Bambo vs kingwendu
Wasanii Bambo (kushoto) na Kingwendu wakichuana kuchekesha kwenye mpambano uliofanyika juzi ndani ya Ukumbi wa Dar West Tabata (Picha na Ismail Mang’ola)
********************************


Miss Dar city centre is around the corner!, Jiandae kuona totoz zenye sifa na vigezo
Shindano lenye hadhi ya kipekee kwenye levo ya vitongoji kuelekea kanda kabla ya fainali za Miss Tanzania, tunazungumzia Miss Dar City Centre, ebwana eeeh, ngoma imeiva na sasa ipo vere vere around the corner.

Juni 26, 2009 hapo inatajwa Ijumaa hii kwenye Ukumbi wa Lamada Hotel, Ilala, Dar es Salaam ndipo fainali zitachukua nafasi ambapo watoto wa ukweli watapanda jukwaani kuonesha cat-walk za maana.

Wikiendi iliyopita, Abby Cool and MC George Over The Weekend ilitembelea kambi ya warembo hao, iliyopo Lamada Hotel na kushuhudia moto mkali wa warembo hao ambapo kila mmoja alikuwa ‘siriaz’ ile mbaya kuhakikisha ananyakua nafasi ya juu na kusonga mbele.

Safu hii ilipata fursa ya kuchonga mawili matatu na totoz wote ambao wapo kamili kwa ajili ya kufanya performance katika tarehe husika ambapo kila mmoja kwa staili yake ya kuchonga kimisi, alionesha hope kuwa Juni 26 yeye ndiye atakayeibuka mwenye taji.
Hata hivyo, safu hii ilikagua kuanzia kucha za miguu mpaka nywele kwa warembo wote na kubaini kuwa kila mmoja anavyo vigezo vyake vya kuwafanya majaji wamwagie kura za kutosha hivyo kuibuka mshindi.

Mkurugenzi wa Sisi Entertainment, John Dotto ambaye ndiye mratibu wa Miss Dar City Centre 2009 alisema nasi kwamba kila kitu kipo tayari kwa ajili ya fainali hizo mwaka huu na kuongeza kuwa amani itatawala, pia burudani za kipekee kutoka African Stars Band ‘Twanga Pepeta’, Haisa Mbyula ‘Bob Haisa’ na kadhalika zitakonga nyoyo.

Shindano limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers, Vayle Springs LTD, CXC Africa, Fredito Entertainment na Masoko Agency.


******************************************************************************
Jeezy Mabovu

Kalapina

Fid Q

Nick wa Pili

Tupac, Snoop na Suge Knight

The real kuhusu....hip hop
Ofkoz kuna watu wanavamia fani. Hawajui chimbuko la Hip Hop huko mtoni miaka hiyo lakini wanaingia kati na kuchana mistari, ukiwauliza niaje mazee, wanajibu: “Men tunafanya Hip Hop ya ukweli.”

Abby Cool and MC George over the weekend inataka tui la nazi lisiitwe maziwa. Tunavyoelewa sisi ni kwamba Hip Hop si kuchana vesi peke yake. Unaweza kuwa mzuri wa kuandika mistari lakini bado ukawa si mfuasi kamili. Si kila aliyesoma Biblia ni padri au mchungaji, yawezekana msahafu umelala kichwani lakini siyo shehe.

Get facts, Hip Hop ni imani, ina misingi yake. Hapa Bongo wengi wanajitapa kuwa ni wana-Hip Hop lakini hawana wanalojua kuhusu aina hiyo ya muziki.

Wana-Hip Hop wanavyospeek loudly kuhusu Hip Hop yao
Hatukutaka tuchonge sisi tu, tulitoa uwanja mpana kwa wana-Hip Hop wa ukweli katika himaya ya Jakaya ili waweke mambo kweupe. Tulipiga stori na Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Jeezy Mabovu, Nick wa Pili, Karama Masoud ‘Kalapina’ na wengineo.

Wote hawa waligongana katika meseji hii. Hip Hop ni muziki ulioanzia kitaani. Enzi hizo Wamarakeni weusi walipokuwa bize for liberation movements against ubaguzi wa rangi.

Hip Hop ilivyotake-off
Machizi wa mtoni baada ya kuona unyanyasaji ni too much, walianza kuchora mitaani na kueleza meseji zao waziwazi jinsi wasivyopendezewa na ubaguzi. Michoro hiyo ikapewa jina GRAPHITE, ngoma ikazidi kutambaa ikawa kwenye kwanja, DJ anakatiza muziki na kuchombeza mistari ya kudai haki ya mtu mweusi.

Chombezo za DJ ziliwadatisha machizi, kwahiyo mitaani wakawa wanafanya FREE STYLES, hivyo wanaharakati hasa vijana walipokutana kitaa ikawa ni full kubadilishana mistari, baada ya hapo mzuka ukahamia kwenye BLACKA DANCES, kwahiyo machizi wakawa wanamegeana vesi huku wanacheza kabla ya kuibuka MC kamili.

Hey! Let us put all things in one basket, unapozungumzia Hip Hop maana yake unaweka Graphite, DJ, Free Styles, Black Dances na MC pamoja.

Kauli ya wana-Hip Hop ni kuwa Hip Hop inamaanisha meseji, mavazi, pozi, kutembea na hata jinsi ya kulala. Haiwezekani brazamen kaweka wave kichwani halafu naye anajiita mfuasi. Ugumu ni nguzo, ubishololo ni mwiko.

Kuna wakereketwa wa siasa ambao wana uwezo mkubwa wa kuongea kuliko viongozi wao, lakini haimaanishi na wao ni wanasiasa. Inawezekana fulani ni mtaalamu wa kughani lakini kama hajui misingi ya Hip Hop atabaki kuwa shabiki. Jiandae kupata elimu kamili ya kupitia hapa!

Huu ni mjadala, unalo la kuweka? Tupatie neno lako kupitia namba 0715-110173, 0713-355717.
compiled by mc george

No comments: