Friday, July 24, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!

Irene Uwoya: Ndoa kwanza, zawadi za Sexiest Girl baadaye
Miss Tanzania namba tano 2006-07, Irene Uwoya Ndikumana hakuweza kuchukua zawadi zake baada ya kuibuka mshindi wa taji la Ijumaa Sexiest Girl 2008-09. Irene a.k.a Shemeji wa Wanyarwanda alipokuwa nchini, mara kwa mara alipanga appointment na mmoja wa waratibu wa shindano hilo lakini mambo hayakuweza kwenda kama inavyotakiwa kwa sababu muda mwingi alikuwa kwenye pilika za ndoa.

Mrembo huyo ambaye hivi sasa ameibukia kuwa muigizaji funika bovu nchini, mpaka anafunga ndoa na kuondoka nchini kuelekea Cyprus bado alikuwa hajakamata stahiki yake ya ushindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2008-09 ambayo ni shopping ya nguvu.

Kwa mashabiki wa Ijumaa Sexiest Girl, taratibu za mawasiliano kati ya waratibu na Irene zinaendelea, itakapofikia wakati wa makabidhiano kila kitu kitafanyika katika picha.
******
Hey! Babu hajafulia
Supastaa mwenye ‘eji’ ya kutosha Bongo Flava, Horoun Kahena ‘Inspector’ ameachia dude jipya linalokwenda kwa jina la Sijafulia.

Inspector a.k.a Babu alilonga na Showbiz kwa njia ya waya na kuiambia kuwa sababu ya kuiweka hewani Sijafulia ni kutaka kuwadhihirishia mashabiki wake kwamba mambo yake ni supa.

“Yap watu wanaongea, wengine wanafikiria nimeishiwa lakini mimi nipo mzuka sana. Zaidi ya yote nina familia ambayo inanikip bize,” alisema mfalme huyo wa Rap Katuni.

Apart of that, Babu alisema kuwa hivi sasa yupo chimbo kwenye studio za Bongo Records chini prodyuza, Paul Matthias ‘P. Funky’ akiunda dude lingine ambalo amekamua pamoja na Hamis Mnjuma ‘Mwana FA’.
Hey, si ilielezwa Babu ana bifu na FA? Stay tuned 4 da song!
********

JANET JACKSON KUZIBA MAPENGO YA THE JACKO
Janet Jackson tayari ameshatangaza kwamba atakuwa tayari kuwalea watoto watatu wa marehemu kaka yake, Michael Jackson ‘The Jacko’.

Aliweka wazi kuwa ataambatana na memba waliobaki wa Kundi la Jackson 5 ili kutoa shoo 50 za London, England ambazo zilitakiwa zitekelezwe na King MJ lakini kwa bahati mbaya Mungu akawa amemchukua mapema.

Kutokana na moyo huo wa upendo ambao Janet anauonesha, wadau mbalimbali wamekuwa wakimminia pongezi kwa maelezo kuwa anaonesha mapenzi yake ya wazi kwa kaka yake.

Kutokana na kukubali kwake kushiriki ziara ya London 02, mratibu wa shoo hizo alisema kuwa anaamini kwamba Janet, 43, atafunika vibaya.

Aidha, inaelezwa kwamba watoto wa Michael, Prince I, Paris na Prince II wanamuona Janet ndiyo chaguo lao kwa sababu hawafikirii mtu mwingine anayeweza kuwalea kwa mapenzi makubwa kama shangazi yao huyo.
********
Ijumaa Sexiest Barchelor. whoz next?
Steven Charles Kanumba ‘The Great’ ndiye aliyebeba taji mwaka 2007, alimpiga mweleka Golikipa wa Simba, Juma Kaseja Juma (PICHANI KULIA) ambaye aliambulia nafasi ya pili.
Tangu wakati huo, mambo yalipoa lakini mwaka huu shindano hilo linakuja kivingine, nani ataibuka kidedea? Ni suala la kusubiri muda, everything gona be mwake.

Ni Kanumba tena? Je anaruhusiwa kutetea taji? Piga simu utoe maoni yako kama The Great aendelee kutetea nafasi yake au apumzishwe na asiingie kabisa kwenye shindano.

Tuma sms utaje jina la staa wa kiume unayedhani anatosha kuwa Ijumaa Sexiest Bachelor 2009-2010. Kumbuka Kaseja alifunga ndoa mwaka jana na mtoto wa Kitanga, Nasra Nassor, hivyo haruhusiwi.
********
kazi kwenu ladies, changamkieni mchongo huo!!!

No comments: