Friday, September 25, 2009

IJUMAA SHOWBIZ!


D’banj Kudondoka Bongo
Katika kusheheresha tuzo za MTV Afrika zinazotarajiwa kutolewa mwezi ujao pande za Kenya, mchizi anayefanya vyema na ngoma kadhaa hivi sasa, ikiwemo Falling In Love, Dapo Daniel Oyebanjo a.k.a D’Banj (pichani juu) kutoka Nigeria anatarajiwa kudondoka Bongo hivi karibuni kama mgeni mwalikwa kunako shoo yenye jina la Road to MTV Africa Music Awards (MAMA) itakayopigwa ndani ya Ukumbi wa Bilicanas Oktoba 3, mwaka huu.

Kwa mujibu wa mratibu wa ishu hiyo, Christine Mosha ‘Seven’ ,shoo hiyo ambayo hufanyika kila mwaka na sehemu tofauti yakiwa ni maandalizi ya kuelekea kunako tuzo hizo, safari hii itafanyika Bongo ambapo mbali na mkali huyo kutoka Nigeria pia wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania ‘awadi’ hizo Ambwene Yesaya ‘A.Y’ na Sara Kaisi ‘Shaa’ wataangusha burudani ya ukweli.

“Pia msanii kama Profesa Jay ambaye atakuwa ni mgeni mwalikwa katika tuzo hizo tutakuwa naye katika shoo hiyo ya Bilicanas ambayo itaanza saa tatu usiku na kuendelea kwa kiingilio cha shilingi 15, 000 kila mtu. Kwa ishu zaidi watu wanaweza kutembelea website yetu ambayo ni www.mama.mtvbase.com,” alisema Seven.

Pia mratibu huyo amewaomba Watanzania na wapenzi wa burudani kwa ujumla kuendelea kuwapigia kura A.Y na Shaa ili waweze kuleta heshima Bongo kwa kuibuka na tuzo hizo. “Kumpigia kura A.Y andika neno BHH AY kisha unatuma kwenda namba 0789 777 333. Ili kumuwezesha Shaa ambaye anawania tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia andika neno BNA SHAA kisha tuma kwenda namba 0789 777 333.”
****************************



DJ Choka ala shavu Zizzou Entertainment
Siku kadhaa baada ya kuacha kupiga kazi na Prof. Jay, Dj maarufu kunako game ya Muziki wa Kizazi Kipya, Hugoline Mtambachuo Martin a.k.a Dj Choka au Mr. Apetite amekula shavu ndani ya Kampuni ya Zizzou Entertainment kama dj wa wasanii waliyopo chini ya lebo hiyo.

“Baada ya kuachana na Prof. Jay ambaye nilikuwa kama Dj wake na mambo mengine yanayohusu muziki, hivi sasa nipo na Kampuni ya Zizzou Entertainment kama dj wa wasanii waliopo chini ya kampuni hiyo na kazi nyingine za entertainment pia najishughulisha nazo na hivi sasa nipo kwenye tour ya Fiesta kama dj wa Ngwea na Blue.

“Najisikia faraja sana kwasababu nimeyaanza maisha yangu upya kabisa tangu nilipoondoka kwa Bro Jay, pia najishughulisha kusambaza habari za wasanii wote wa Bongo kupitia Blog yangu inayoitwa www.djchoka.blogspot.com,” alisema Choka alipopiga stori na ShowBiz.
****************************

A.Y ndani ya Malaysia
Msanii Ambwene Yesaya A.Y ambaye alikwea pipa mwishoni mwa wiki iliyopita kuelekea Malaysia tayari ameshadondoka pande hizo na jana Alhamisi aligonga shoo ya funiko kunako Jiji la Kuala Lumpur.

Akipiga stori na ShowBiz kwa njia ya simu kutoka pande hizo jamaa alisema kwamba kila kitu kuhusu ziara yake hiyo kimekwenda fresh na kwamba anatarajia kurudi Bongo Jumapili ya wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wa kuwania tuzo za MTV Afrika kama Msanii Bora wa Hip Hop akichuana na mastaa kama Jay-Z na Kanye West.

Ili kumuwezesha kuibuka na ushindi cheki katika stori ya D’Banj hapo juu.
**********************************

Fiesta One Love Dom wiki hii
Baadhi ya wasanii waliokuwa ndani ya bifu za hapa na pale wanatarajia kumaliza tofauti zao kupitia Tamasha kubwa ambalo hupigwa kila mwaka mara moja, Fiesta ambalo safari hii litaanzia pande za Dom (Dodoma) kesho Jumamosi.

Ndani ya ShowBiz, Mratibu wa burudani hiyo, Godfrey Kusaga alisema kwamba mbali na kuwapatanisha wale waliowahi kuzinguana, Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya ‘One Love’ pia litaenda sambamba na kutafuta vipaji vya watangazaji ambao watakula shavu kunako Clouds TV ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni.

“Tumetoa kauli mbiu hiyo ya ‘One Love’ kuunganisha wasanii wote na mashabiki katika kuinua sanaa yetu ya Tanzania, ndiyo sababu pia ya kutafuta watangazaji na waandaaji wa vipindi katika Fiesta ya mwaka huu, zoezi hilo litakuwa likiendelea katika mikoa mingine kwa staili hiyo, tunaomba wenye vipaji wajitokeze,” alisema Kusaga.

Baadhi ya wasanii wanaotarajia kuangusha burudani pande za Dodoma kesho ni pamoja na Marlaw, Ngwea, Chid Benz, Sir Nature, Madee, TMK Wanaume Family na wengine wengi. Fiesta ya mwisho itafanyika Dar es Salaam, Octobar 31, mwaka huu.
**************************

IJUMAA SEXIEST BACHELOR: Ay, Chid, Black, Mwisho wasimama pabaya
Hali imechafuka, mastaa Chid Benz, Mwisho Mwampamba, Black Rhino, Tundaman na AY wamekaa kwenye mstari wa hatari na kama kura yako haitofanyakazi basi watapotea kwenye shindano.

Wiki ijayo watatoka watatu, kwahiyo kama mmoja kati yao ndiye staa wako basi mchague ili aendelee kwenye shindano.

Kimsingi mastaa hao ndiyo wapo mguu ndani mwingine nje na waliosalia wanakula bata a.k.a shushu kwa sababu kura zao zinatosha kuwafanya wapumue.

Unachotakiwa kufanya ni kuandika ujumbe mfupi wa maneno, SMS kupitia simu yako ya mkononi, unaandika neno IJUMAA unaacha nafasi, halafu unaandika namba ya mshiriki kisha unaituma kwenda namba 15551.

Mfano; IJUMAA 00 halafu unaituma kwenda namba 15551. Kumbumbuka, wiki ijayo watatu wanaenda BIG OUT.
****************************
Compiled by mc george

No comments: