Monday, September 21, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Moe Q: Nataka kumaliza bifu na Ray C
Artist wa Bongo Flava anayesimama, Mohamed Chalamila ‘Moe Q’ amesema kuwa hivi sasa anajiandaa kuzindua albamu yake ya kwanza na katika kuhakikisha hilo linakwenda kwa mapenzi ya Mungu, anajiweka sawa kumaliza bifu na dada yake, Rehema Chalamila ‘Ray C’.

Akipiga stori na mwandishi wa Wikienda Showbiz, Chausiku Omar, Moe Q alisema kuwa amekaa na kufikiri, hivyo akagundua kwamba haipendezi yeye na dada yake kukaa bila maelewano.

“Kimsingi mimi sijui hasa kilichofanya mimi na sister tutofautiane hadi kufikia bifu lililopo, kwahiyo nitafurahi sana tukimaliza tofauti zetu. Nitamfuata na kumuuliza nimemkosea nini mpaka tukawa hivi kisha nitamwomba msamaha,” alisema Moe Q.

Moe Q alitibuana na Ray C baada ya brazameni huyo kumchana laivu sister wake kwamba hapendi mambo yake na anavyojichoresha kwenye vyombo vya habari, kitu ambacho kilisababisha dada Rehema amkane ndugu yake kwamba hamtambui.

Mbali na hilo, Moe Q amesema kuwa albamu yake itakwea kitaani kwa jina la Machozi na kusema kwamba ataizindua Oktoba 4, 2009 kwenye Ukumbi wa Travertine, Migomigo, Dar ambapo shoo kali itakayolihusisha Kundi la Jahazi Modern Taarab itachukua nafasi pana.
*****************************

AY: Kura ndiyo mambo yote
The Commercial Rapper, Ambwene Yesaya ‘AY’ amewataka Watanzania kuungana kupiga kura ili kumwezesha kuibuka shujaa kwenye kinyang’anyiro cha Best Hip Hop Artist Award on MTV Africa Music Awards (MAMA).

Ambwene aliiambia Abby Cool & MC George over the weekend kwamba kura ndiyo itakayowezesha kila kitu, hivyo akawaomba Watanzania kadiri wanavyoweza kupiga kura ili kumwezesha.

Alisema: “Kitu ambacho MAMA wanakiangalia ni category, hawaangalii wasanii waliopo. Wao wanaamini kuwa wasanii waliopo kwenye category moja wanalingana uwezo kwahiyo mwenye kura nyingi ndiye atashinda.”

Mbali na hilo, Ambwene alisema kuwa anaamini Tuzo za MTV Africa zitamtoa kwa sababu siku ya event ameteuliwa kuwa mmoja wa wasanii watakaosimama on stage na kutoa shoo kwa awamu mbili tofauti.

Apart of MAMA issues, Ambwene amekwea pipa jana Jumapili kuelekea Malaysia ambako Alhamisi ya wiki hii (Septemba 24), ataangusha shoo ya funiko kunako Jiji la Kuala Lumpur na Septemba 27, 2009 atadondoka Bongo kujiandaa na tuzo hizo.

Katika issue ya MAMA, Mtanzania mwingine ambaye amekuwa nominated kuwania tuzo hizo ni Sara Kaisi ambaye anapigania Awadi ya Msanii Bora Anayechipukia.

Bongo inaweza kuwa na heshima ikiwa tu hautobana kuwapigia kura, kumchagua AY andika neno BHH AY kwenda namba 0789 777 333 na Shaa unaandika BNA SHAA kwenda namba 0789 777 333. Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo.
*************************

Cameron Diaz: Kumbe kajichetua kitandani na midume 21!
Modo Cameron Diaz ndiye staa anayesomeka kwenye stage ya Ebwana Dah! Orodha ya wanaume aliowahi kucharuka nayo inakuja katika aya zinazofuata.

Kwa mujibu wa mtandao unaodili na issues za staa gani kajichenga faragha na nani, Cameron amewahi kupumzika na watu maafurufu kama Ashton Kutcher, Robbie Williams, Tom Cruise na Carlos de La Torre katika kipindi ambacho hakiwekwi wazi.

Cameron pia anaelezewa kufanya karamu on the bed na Matt Dillon kati ya mwaka 996 – 98, Edward Norton, 1998 – 99, Vince Vaughn, 1998, Jared Leto, 1999 – 03, Leonardo DiCaprio, 2001 – 09 na Justin Timberlake, 2003 – 06.

Wengine ni Djimon Hounsou, 2007, Kelly Slater, 2007, Criss Angel, 2007, John Mayer, 2007, Bradley Cooper, 2007, Scott Speedman, 2008, Gerard Butler, 2008, Kevin Connolly, 2008, Paul Sculfor, 2008 – 09, Adam Levine, 2009 na Jude Law, 2009.

Kwa jumla, inaonesha kuwa Cameron amewahi kujikunja kimahaba na wanaume 21 lakini katika muda wote huo, inaonesha kwamba mwaka 2007 ndiyo alichangamsha damu na wanaume wengi zaidi.

Jina lake kamili ni Cameron Michelle Diaz na a.k.a yake ni Cam, alizaliwa San Diego, California, Agosti 30, 1972 na umri wake ni miaka 37 na ana urefu wa futi 5.8. Ni Mmarekani mwenye asili ya Hispania.
**********************************
compiled by mc george

No comments: