Maunda
tulia nyumbani ulee mtoto”
Huku kichanga chake kikiwa na takribani miezi mitatu tangu kilipoingia duniani, Bongo fleva Diva, Maunda Zorro, amezua viulizo na kutoa ‘chansi’ kwa wadau wa burudani nchini kumpa ushauri wa bure wakimtaka atulie nyumbani na kulea mtoto.
Jamaa hao walifikia hatua hiyo baada ya Maunda kuonekana akijirusha ile mbaya ndani ya klabu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar juzikati ambapo kulikuwa na ‘afta pati’ ya tuzo za Kill 2009.
Wadau hao waliamua kumtolea uvivu walidai kwamba, ni mapema mno kwa Maunda kujiachia na kwamba mtoto alimwachia nani hivyo kumtaka atulie nyumbani ili kulea mtoto hadi atakapofikia ‘eji’ ya kufanya hivyo.
“Hebu muone Maunda anavyojiachia, mtoto atakuwa amemwachia nani? Maunda anatakiwa atulie nyumbani alee mtoto hadi akiwa na umri wa kumwacha ndiyo afanye haya anayoyafanya,” alisema mmoja wa wadau hao.

******************************************
MKALI WA NYONGA TEKETEKE
Kuisapoti Bahati Nasibu ya Shinda Gari Awamu ya Pili
Mpango mzima wa shindano la kumsaka mkali wa kucheza muziki wa taarab a.k.a Mkali wa ‘Nyonga Teketeke’ unaogongwa na Kundi la Jahazi Modern Taarab unatarajiwa ku-take place ndani ya Ukumbi wa Vatican City Sinza, Dar es Salaam usiku wa Mei 22, mwaka huu.
Tifu hilo ambalo litawahusu wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, litakuwa pia likiinadi Promosheni ya Shinda Gari Awamu ya Pili inayodondoshwa kwa wasomaji wa magazeti yanayotolewa na Kampuni ya Global Publishers.
“Kama wewe unadhani una kipaji na umri wa kunzia miaka 18, jitokeze ili uweze kushiriki kwenye mpambano huo, utuoneshe uwezo wako wa kukata nyonga stejini kupitia burudani kutoka kwa washindi wa tuzo kibao, Jahazi Modern Taarab, chini ya Mzee Yusuf,” alisema Sarah Felix ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Raha Entertainment waandaaji wa shughuli hiyo.
Kunako fainali hizo, mshindi ataondoka na zawadi ya mkwanja taslimu huku watakaofuatia wakiambulia vifuta jasho vya ‘ukweli’. Shindano hilo linaletwa kwenu chini ya udhamini wa gazeti hili, Kampuni ya simu za mkononi Tigo, Allana Tours na SASSY Foot and Nails Spa.

*******************************************
Afande, Ditto
Kutoka pande za Kinondoni, Dar es Salaam ulipo mjengo wa kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wa Kibongo, THT tumedondoshewa ishu kwamba, msanii Benedictor Lameck a.k.a Ditto aliyewahi kupiga kazi na Afande Sele kupitia kundi la Watu Pori kabla ya kuzinguana na kutengana, amesimama tena na Mfalme huyo wa Moro na kupiga kolabo moja kupitia ngoma yenye jina la ‘Ukimuona’ iliyofanyika ndani ya Studio za Soundcrafters chini ya Prodyuza Enrico. Big up ndugu kwa kumaliza tofauti zenu.
*****************************************
Diamond:
Siyo uchawi ni baraka za mama’angu
Dogo aliyejikusanyia tuzo tatu kupitia Kili Music Awards 2009-10 zilizotolewa mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar, Nassib Abdul a.k.a Diamond amechana na ShowBiz juzi kati kwamba kila kitu anachokifanya ndani ya game ya muziki wake huwa kina baraka za mama yake mzazi ndiyo maana anafanikiwa.
Mchizi ambaye hivi sasa anasikika na ngoma yenye jina la Mbagala alisema kuwa ameamua kuweka wazi kuhusu hilo ili kuupoteza uvumi ulioenea town kwamba mafanikio yake kimuziki ikiwemo kulamba tuzo tatu kwa mpigo yanatokana na mishemishe zake za kwenda kupuliza kwa ‘wichi dokta’ pande za Tanga a.k.a TA.
********************************
Makhirikhiri Live Bongo
Wakati tunaelekea mtamboni tulidondoshewa ishu mpya kwamba, lile kundi maarufu la muziki wa asili kutoka pande za Botswana linaloongozwa na Moses Malapela a.k.a Shumba Ratshega, linalojulikana zaidi kama Makhirikhiri linatarajiwa kudondoka Bongo Mei 27, mwaka huu kwa ajili ya shoo kadhaa. Zaidi endelea kufuatilia katika Magazeti ya Global Publishers.
compiled by mc george/ijumaa newspaper
1 comment:
Love Diamond much.
Post a Comment