Monday, May 17, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

(click picha kusoma tex)
Kili Music Awards 2009 Live Bwana Misosi amng'ata sikio Sean Kingston
Mshindi wa Tuzo ya Wimbo Bora wa Ragga, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’, alitumia fursa adimu ya kuwa karibu na staa wa Reggae Dancehall duniani, Sean Kingston. Misosi alikabidhiwa tuzo yake na Sean Kingston lakini mkali huyo wa Nitoke Vipi, alijinyoosha hadi kwenye sikio la mchizi anayeminya nchini Marekani na kumnong’oneza kitu fulani.

“Yeah, nilimuomba kuzungumza naye akasema tutafanya hivyo kesho (Jumamosi), nina mambo ya msingi ya kuzungumza naye kuhusu muziki, huu ndiyo wakati wa kutoka,” Misosi alisema nasi Ijumaa iliyopita baada ya kushuka jukwaani na kukabidhiwa mzigo wake.
***********************************************************
Chuji akung'uta 'fulanaz', achafua viwango
Tuzo za Kili 2009/2010, ziliandaliwa kwa viwango vinavyotosheleza, kila kitu kilipelekwa ki-5star, lakini kiungo wa Klabu ya Yanga, Athuman Idd Chuji alivuruga color baada ya kunyuka fulanaz na trak jukwaa kuu.

Chuji alialikwa kama mgeni wa heshima na alipanda kukabidhi Tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae ambayo ilidondoka kwa Ambwene Yesaya ‘AY’. Kutokana na hilo, Chuji alipotezwa vibaya na AY ambaye alikuwa smart, huku wadau wakiponda muonekano wa mwanasoka huyo kwamba mandhari ya eneo la tukio, yalimfanya aonekane mchafu.
********************************************
Gadner awa mwenyeji, ageuka mgeni
Ni kionjo tu! Gardner G Habash alikuwa mshereheshaji wa Usiku wa Kili lakini sauti yake ikawa inasikika kutoka Backstage, kwahiyo alikuwa mwenyeji, lakini baadaye akabadilika mgeni pale alipopanda jukwaani kupokea Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike ambayo alishinda mkewe, Judith Wambura Habash ‘Lady Jaydee’, ambaye alikuwa ameshaondoka kwenda 'kiwanjai chake kutumbuiza mashabiki waliokuwa wakimsubiri.
****************************************

Diamond: Afanya wonderful
Mbagala Icon, Diamond a.k.a Wa Kutoswa, amefanya wonders baada ya kudaka tuzo tatu katika vipengele vitatu kati ya vinne ambavyo alishindanishwa mwaka 2009-2010. Diamond ambaye ni dogo anayechipukia, aliwapiga mwereka mastaa kibao, akadaka ya Wimbo Bora wa R&B kupitia ngoma yake Kamwambie ambayo ilishinda category ya Wimbo Bora wa Mwaka, pia akawafunika underground wenzake kwa kubeba Tuzo ya Msanii Bora Anayechipukia.

Ni category moja tu ambayo alishindanishwa na kushindwa ambayo ni Video Bora ya Muziki ya Mwaka ambayo ilitua kwa mkali Cpwaa! Baada ya kukabidhiwa tuzo ya Msanii Bora Chipukizi, Diamond aliteka hisia za watu, pale alipofanya freestyle ambapo aliweka maneno kwamba ugumu wa maisha ndiyo uliofanya ajue kutunga nyimbo.
********************************************************
Mange ampa mateso mtoto tumboni
Miongoni mwa mastaa waliokanyaga red carpet kwenye Usiku wa Kili Ijumaa iliyopita, Diamond Jubilee, Dar ni Mange Kimambi lakini kama ulikuwa haunyaki ni kwamba mdada huyo kwa sasa ni mjamzito, tumbo ndiii, halijifichi! Hata hivyo kivazi alichonyuka ni kama mateso kwa mtoto tumboni, kwani alitinga kiwalo cha kubana ambacho hakikumtoa poa hasa pale kwenyewe! Kitaalamu, inashauriwa kwamba mwanamke akiwa mjamzito, anatakiwa awe anavaa nguo pana ambazo zitamuwezesha awe na nafasi na kumuweka huru zaidi yeye na kichanga chake tumboni.

compiled by mc george/ijumaa wikienda

3 comments:

Anonymous said...

huyu mtoto akizaliwa na matatizo, the mummy she will be the one to be blamed! lets watch this space

Unknown said...

kuna wakati na wakati, watu wamesahau hata maadili ya dini zao jamani.

Anonymous said...

Uyu malay. hanatia kichefu chefu