Huu ni mfululizo wa mwisho wa makala haya yaliyokuwa na lengo la kujua sababu za watu kuugua mara kwa mara. Tulianza kwa kuona kuwa mwili una kanuni zake ambazo ni lazima zifuatwe na zisipofuatwa huleta maradhi. Vile vile tumeona kuwa maradhi hayaji ghafla, bali huanza kwa kutoa ishara ambazo watu wengi, ama hawazijui au huzipuuzia, tunahitaji kuwa na elimu ya kutosha kuhusu ulaji wa vyakula vya aina mbalimbali vinavyokinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali… Endelea kusoma sehemu hii ya mwisho.
Mafuta, Sukari, Ice Cream, Pipi
Hili ni kundi la mwisho la vyakula ambalo limepewa nafasi ndogo sana katika orodha ya vyakula muhimu mwilini. Ni vyakula au vitafunwa ambavyo hutumika kuongeza ladha ya chakula.
Unapopika chakula, kama wali, nyama, maharage, n.k unahitaji kutia mafuta ili kupata ladha nzuri ya chakula hicho. Kuna aina mbalimbali za mafuta, yapo yatokanayo na nafaka na yale yatokanayo na mimea na wanyama.
Hivyo, linapokuja suala la kutumia mafuta katika vyakula vyetu, tunatakiwa kuweka kiasi kidogo cha mafuta, tupendelee mafuta yaliyotengenezwa kutokana na mimea au mbegu ili kupata faida ya mafuta.
Watu wengi hupenda sana vyakula vyenye mafuta mengi. Kuna imani potofu imejengeka miongoni mwa watu kuwa kula vyakula bila kutia mafuta (chukuchuku) ni dalili ya umaskini au upungufu wa kipato.
Imeonekana kuwa mtu anayekula vyakula vinono vilivyopikwa kwa mafuta mengi ndiye anayekula vizuri, wakati kumbe wanaopenda ulaji wa vyakula hivyo, mwisho wao huwa mbaya, kwani huishia kupatwa na shinikizo la damu na magonjwa mengine ya moyo na hatimaye kupatwa na kiharusi au kupoteza maisha kabisa.
Halikadhalika kwenye sukari, ni kiasi kidogo sana kinahitajika mwilini. Vyakula vingi vya asili, vya jamii ya mboga na matunda, vina sukari yake ya asili ambayo inakidhi mahitaji ya mwili. Kupenda kula vyakula vya kawaida vyenye sukari nyingi nako ni hatari kwa afya yako.
Kwa ujumla, vyakula vyote vya kundi hili, mtu anaruhusiwa kuvila lakini kwa uchache sana. Pale unapolazimika kula moja kati ya vyakula hivi, huna budi kuwa mchaguzi na kutafuta mbadala. Tumia asali pale unapohitaji sukari, tumia mafuta yatokanayo na mimea au mbegu, kama vile mafuta ya alizeti, ufuta pale unapolazimika kutumia mafuta.
Kwa mpangilio wa chakula ambao tumeueleza tangu mwanzo wa makala haya, jipeleleze mwenyewe na Ujiulize ni vyakula gani unakula vingi kwa siku na katika maisha yako kwa ujumla. Je, unafuata mwongozo huu kwa kiasi gani? Utafiti unaonesha kuwa mwongozo huo wa vyakula umegeuzwa na umekuwa ‘kichwa chini, miguu juu’.
Mwongozo wa vyakula (Food Pyramid) unaonesha ugali wa dona, mikate ya rangi nyeusi, maharage matunda, mchicha, kabichi, kisamvu, ndiyo vyakula vya kuliwa kwa wingi kila siku, wakati chips kuku wa kukaanga, mayai, pilau, ma ‘bugger’, keki, ice cream, ni vyakula vyakula kidogo sana.
Lakini hali halisi haiko hivyo. Chips mayai, kuku, buggers, keki, ice cream, nyama choma ndiyo vyakula vinavyoliwa kwa wingi kila siku. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za ulaji. Ulaji huu unaunyima mwili kinga yake ya asili dhidi ya maradhi yote, hivyo unapoanza kuugua, ugonjwa mmoja hadi mwingine, usishangae, kwani hali hiyo inakuwa umeijenga mwenyewe!
MWISHO.

3 comments:
mmh kaka hapo kwenye ice cream duh!! asante sana.
swali langu ni vipi mtu akiamua kutokula mafuta kabisa? akihitaji mafuta anakula nyama yenye mafuta au nafaka zile zenye mafuta basi.
anaweza akapata upungufu wowote?
kaka hii ni kweli kabisa, kwani toka niwe nampeleka mama yangu katika clinic ya sukari, nimekuwa nikipika mchemsho kama wake na hali yangu ya afya ni nzuri sana, ila hapo katika ice cream ni mtihani kidogo.
vipi nikila ice cream kwa wiki mara mbili tu, na biskuti mara mbili kwa wiki? itaharibu utaratibu? chips hizo sina shida nakula mara chache sana.
Je ulaji wa Ice Cream hauna faida kabisa Ni hasara tu?

Post a Comment