Saturday, August 28, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Tunda apokea pongezi za kutosha, ampa shavu Rose Ndauka, kuoa mwakani

Mkali wa ngoma za majonzi kutoka kruu ya Tip Top Connection, Khalid Ramadhani ‘Tundaman’ amesema na ShowBiz kwamba amepokea kwa mikono miwili pongezi anazopewa na baadhi ya mashabiki wake kuhusiana na ubora wa kazi zilizomo kwenye albamu yake mpya iitwayo ‘Hali yangu mbaya', inayosumbua sokoni kitaani hivi sasa, Hemed Kisanda anashuka nayo.

Akiangusha stori na safu hii juzi kati Tunda alisema kwamba amekuwa akipokea simu nyingi kutoka kwa mashabiki zinazompa ‘hala’ kwa utunzi bora wa nyimbo zake. “Albamu ya Hali yangu mbaya ni elimu tosha kwa jamii kwa jinsi nyimbo zake zilivyokuwa na mafundisho ya kutosha, ndiyo maana napata pongezi.

Pia katika albamu hiyo yenye nyimbo kumi kuna ngoma moja inakwenda kwa jina la ‘Uzuri wake’ ambayo nimemuimbia staa wa muvi Bongo, Rose Ndauka,” alisema. Pia msanii huyo aliweka kweupe kwamba kwa wale wenye maswali kuhusu ndoa yake anatarajia kufanya hivyo mapema Februari mwaka ujao. ***************************
“Chiller hajafulia, alipitia mitihani ya kimaisha tu, sasa yuko sawa”
Ule uvuni uliyonea kitaani kwamba mkali wa ‘game’ ya muziki wa Bongo Flava, Aboubakari Shaban Katwila ‘Q Chiller’ amefulia umekanushwa vikali na meneja wa msanii huyo.

Akisema na ShowBiz kwa njia ya simu, meneja huyo aliyejitambulisha kwa jina la Dida Fashion alitamka kwamba, wale wanaosema Chiller kafulia wanakosea kwakua msanii huyo alipitia mitihani midogo ya kimaisha na hivi sasa yuko poa akiendelea na muziki.

“Hivi ninavyokwambia siku chache zijazo tutaelekea Uingereza kwa ajili ya shoo kadhaa kabla ya kurudi Bongo kuendelea na ishu nyingine,” alisema meneja huyo ambaye alipoulizwa Q Chiller yuko wapi hadi anaongea kwa niaba yake, alisema yeye kama msimamizi wake ndiye anapaswa kuongea na vyombo vya habari kwa sasa.
**********************************************************
Dida Kumbeba Sister Fay
Mtangazaji wa kituo cha redio Times FM cha Dar es Salaam, Khadija Shaibu a.k.a Dida amejitolea kumbeba msanii wa muziki wa kizazi kipya, Faidha Omary aliyejipa jina la Sister Fey, Gladness Mallya alisema naye.

Akipiga stori na ShowBiz juzi kati Dida aliweka wazi kwamba, amejitoa kuwa meneja wa msanii huyo baada ya kupokea kazi yake mpya ambayo ipo katika mahadhi ya taarabu ikiwa na jina la Mjini. “Siku za nyuma Sister Fay aliwahi kuniletea CD yenye wimbo wake mpya ukiwa katika staili ya Bongo Fleva, nilipousikiliza nikamshauri ajaribu kufanya muziki wa taarabu, nafurahi ushauri wangu ameufanyia kazi na mimi kwa mikono miwili nimekubali kumsimamia kama meneja wake,” alisema Dida. ***************************************************
Wyclef Jean Akata rufaa kuwania urais Haiti
Mwanamuziki Wyclef Jean amesema kuwa atakata rufaa dhidi ya tume ya uchaguzi nchini Haiti ambayo imepinga hatua yake ya kushiriki kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika baadaye.

Akisema na shirika la habari la ‘Associated Press’ mwishoni mwa wiki iliyopita, Jean ambaye ni mkali katika staili tofauti za muziki aliweka wazi kuwa hataachana na nia yake hiyo, atamtuma mwanasheria wake Haiti kabla yeye pia hajaelekea nchini humo akitokea Marekani anakofanyia kazi zake za muziki.

“Nina hati ambayo inaonyesha kila kitu kiko sawa,” alisema Wycleaf na kuongeza kwamba kinachofanyika huko Haiti hivi sasa ni njama tu za kisiasa. Tume ya uchaguzi nchini humo ilitupilia mbali dhamira ya mwanamuziki huyo kwa madai kwamba hakukidhi masharti husika.
:::::::::::::::::::::::::
COMPILED BY MC GEORGE/IJUMAA

No comments: