Friday, September 3, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Tabia Batamwanya: “Navutiwa zaidi na wanaume weusi, wenye nguvu”
Kutoka ndani ya mradi wa muvi Bongo, mwanzoni mwa wiki hii ShowBiz ilipata chansi ya kugonga stori mbili tatu na staa wa game hiyo ambaye pia aliwahi kutwaa mataji kadhaa ya urembo nchini , Tabia Batamwanya ambaye alifunguka kwamba anawahusudu sana wanaume weusi na wenye nguvu.

Tabia aliiambia safu hii kwamba wanaume kibao wamekuwa wakimtokea kila kukicha lakini amekuwa akiwaonesha msimamo wake kwamba yeye siyo ‘demu’ wa kumkubali kila ‘men’ anayekuja usoni kwake ukizingatia kwamba tayari anaye ampendae.

“Wengi wakiniona kwenye muvi au kwenye muziki wanadhani wanaweza kunidanganya nikakubali, mimi siko kiihivyo japo siku zote nimekuwa nikivutiwa na wanaume weusi, ambao wako ‘strong’, siyo legelege,” alisema.

Kwa upande wa game ya muvi tayari mwanadada huyu ameshapiga filamu tatu, huku moja yenye jina la Babla ikiwa kitaani. “Kwa upande wa muziki pia bado naendelea kulisongesha, lengo ni kufika mbali zaidi katika sanaa na kujiongezea kipato, sitaki kuwa msanii wa kuuza sura bila mafanikio,” alisema Tabia.


“Babu Tale amuogope Mungu, Mwezi Mtukufu”
Kama tulivyokuahidi kwenye gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda kupitia safu yake Abby Cool & MC George Over the weekend kwamba tutamtafuta mwanadada Khadija Shaban ‘K-Sher’ na kupiga naye stori mbili tatu kuhusiana na ishu yake na uongozi wa familia ya Tip Top Connection ambao ulidai kwamba umemsimamisha msanii huyo.

Akipiga stori na ShowBiz, K-Sher alisema kwamba ameshangazwa na meneja wake, Babu Tale kudai kwamba amemsimamisha kundini wakati huo siyo ukweli na kumtaka kiongozi huyo aweke wazi ishu nzima ilivyo na siyo kama anavyodai.

“Kuhusu hilo mimi siwezi kulizungumzia sana, wala sikutaka kuzunguka kwenye media na kuongea na vyombo vya habari kama walivyofanya wasanii wengine waliojitoa, isipokuwa nataka kumwambia Tale kwamba amuogope Mungu mwezi huu mtukufu, aseme ukweli kuhusu kilichotokea na siyo kunisimamisha. Kama nimesimamishwa mbona matangazo ya shoo zao yananitaja mi pia nitakuwepo?”Akihoji K-Sher.

Bifu? Wape ushauri Mlela, Hemed
Walianza kama utani, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda hali inazidi kuwa mbaya kwani hivi sasa wamefikia hatua ya kuchanana laivu kupitia baadhi ya vyombo vya habari, kibaya zaidi kila mmoja akionesha nia ya kutaka kuzichapa na mwenzie. Je mwisho wake utakuwa nini?

Nawazungumzia vijana wawili walioingia kwenye mradi wa muvi Bongo hivi karibuni, Yusuf Mlela na Hemed ambao wanazidi kuwaacha mashabiki wao njia panda bila kujua kama bifu lao lina ukweli wowote au la!

Sisi kama wadau wa burudani tumeamua kuingilia kati tukikutaka wewe msomaji na mdau wa filamu Bongo uwape ushauri wasanii hawa kupitia hapa ili urafiki wao urudi kama zamani, ikiwezekana waendelee kufanye kazi pamoja. Tuandikie SMS kupitia 0712-078264 au email: mcgeorge2008@gmail.com.



Extra Bongo wazindua na majonzi
Bendi ya muziki wa dansi nchini, Extra Bongo mwishoni mwa wiki iliyopita ilitambulisha nyimbo pamoja na wanamuziki wapya huku ikiwa na majonzi baada ya mpiga gitaa wake, Isaac Gregoli kufiwa na mkewe, Richard Bukos alikuwepo.

Akipiga stori na safu hii, baada ya uzinduzi huo uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Advantage uliopo pande za Sinza Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki alisema kwamba licha ya kuwa na majonzi walihakikisha mashabiki wao wanafurahia shoo hiyo.

Mke wa mcharaza nyuzi huyo alifariki dunia Alhamisi iliyopita wakati mumewe akiwa kwenye mishemishe za kujiandaa na utambulisho huo lakini alishindwa kutokea ukumbini baada ya msiba huo huku pengo lake likizibwa na Ephrahim Joshua aliyetua hivi karibuni akitokea Muscat.

Ngwasuma: Swaga za utambulisho wao zinakuja
Bendi ya muziki wa Dansi nchini ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ Hatimae imekamilisha nyimbo kumi na mbili zitakazo beba albamu yao mpya inayokwenda kwa jina la Vuta Nikuvute Mathematics, Musa Mateja alisema nao.

Ndani ya ShowBiz ‘Prezi daa’ wa bendi hiyo, Nyoshi El Sadat alisema kwamba kitakachofuata baada ya hapo ni swaga za utambulisho wa albamu hiyo utakaofanyika siku ya Idd Mosi ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee.

“Ndani ya albamu hiyo kutakuwa na historia fupi ya bendi yetu tangu ilipoanzishwa hadi hapo ilipo leo, baadhi ya nyimbo zilizomo ni pamoja na Vuta Nikuvute, Heshima kwa Wanawake, Fadhila kwa mama, Angalia shida yangu, Mwili wangu, Jasmini, Entro Mathematics, Mgeni,Usiku wa Jumatano, Moyisi Katumbi na nyingine ambazo zitakuwa ni ‘sapraizi’ kwa mashabiki wetu siku ya uzinduzi,” alisema.
Katika utambulisho huo msanii Nameles kutoka Kenya atatoa sapoti ya kutosha.


KIDUMU

LINEX
Mama Halima ni ngoma yangu siyo ya Kidumu wa Kenya
Stori iliyopo kitaani hivi sasa ni kuhusu ngoma ya msanii Sunday Mangu a.k.a Linex inayokwenda kwa jina la ‘Mama Halima’ ambayo imekuwa ikiwachanganya mashabiki wengi wakidhani ni wimbo wa Kidumu wa Kenya, kisa sauti zinarandana.

Akiangusha stori na ShowBiz juzi kati, Linex alisema kwamba ngoma hiyo ambayo hivi sasa iko juu imekuwa ikimpa wakati mgumu na kumfanya aonekane mwenye majonzi kwani baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiiomba redioni kwa jina la Kidumu.

“Napenda kuwaambia kwamba ‘Mama Halima’ ni ngoma yangu, ili kuepusha utata uliojitokeza tayari nimepiga kideo ambacho kitaanza kuonekana siku kadhaa zijazo. Ngoma hiyo pia imebeba jina la albamu yangu ambayo itadondoka kitaa hivi karibuni ikiwa na nyimbo 13,” alisema.

Mchizi pia aliwataja ‘maproducer’ waliohusika kuwa ni Villy wa 24/7 Records, Prof. Ludigo, Tuddy, Solomoni Lamba, Jala Man, Dunga na Lamar, pia amewapa shavu wakali kibao wa Bongo Flava.


Oprah “Natamani kufanya shoo kwenye uwanja wa soka”
Chicago, Marekani
Presenter maaraufu huko pande za ‘mbelembele’, Oprah Winfrey ‘ame-expressed’ hamu yake ya kufanya shoo yake ya runinga ijulikanayo kama the Oprah Winfrey Show ndani ya dimba (uwanja) kubwa la soka kabla ya kuachana na kazi hiyo.

Mbele ya wadau wa mtandao wa TV Guide, Oprah alichana kuwa yuko kwenye mipango maalum ya kutekeleza azma yake hiyo ya kufanya shoo kwenye uwanja unaomilikiwa na timu ya Chicago Bears wenye uwezo wa kuchukua watazamaji zaidi ya 61,000 kabla ya tarehe ya mwisho ya kufunga kipindi chake hicho kilichoruka kwa miaka 25 ndani ya runinga ya US TV .

“I don’t know if that’s going to happen, lakini nina hamu ya kufanya hilo mbele ya watazamaji 61,000 kabla sijastaafu rasmi kazi hii mwezi septemba mwaka ujao,” alisema Oprah.

Compiled by mc george/ijumaa

No comments: