Friday, October 1, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

P.Funk majani: Afunguka kuhusu kumchapa Afande
Siku kadhaa baada ya gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda kupitia safu yake ya Abby Cool & MC George Over the weekend kuripoti ishu ya prodyuza kiwango na Mkurugenzi wa Bongo Records, Paul Matthysse ‘P.Funk Majani’ kumchapa kibao na kumtishia kwa bastola msanii Selemani Msindi a.k.a Afande Sele, ShowBiz imetupiwa stori nyingine mpya kutoka kwa mtayarishaji huyo.

Akifunguka mbele ya safu hii ndani ya studio zake zilizopo pande za Mwenge Bamaga, Dar es Salaam, Majani alisema kwamba alilazimika kurusha kofi moja kwa Afande ili kumtuliza baada ya kuona hawaelewani Kiswahili na kukanusha ishu ya kumtolea bastola.

“Kweli nilimpiga Afande kofi moja tu, baada ya kuona hatuelewani. Mimi nilikuwa namuelewesha kwamba humu ndani nimeweka sheria mpya ya kutovuta sigara kubwa na yeye anafahamu hilo, kwanini alivunja sheria, badala ya kunijibu vizuri akawa anawaka huku akinifosi nimalizie kazi yake wakati kuna pesa nilikuwa bado namdai, pia kwa muda huo nilikuwa nimetoka usingizini, kwakuwa usiku mzima wa jana yake sikulala nikimalizia kazi za watu.

“Kuhusu ishu ya bastola hakuna kitu kama hicho, sikumtishia wala similiki hiyo silaha. Kama niliweza kumpiga kofi moja akatulia kwanini nimtishie bastola? Silaha kama hiyo wanatishiwa watu wenye miili mikubwa au majambazi, siyo Afande Sele,” alisema Majani.

Kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda, Afande Sele alidai kupigwa kofi na kutishiwa bastola na P.Funk ambapo alikwenda kufungua kesi katika Kituo cha Polisi Kijitonyama na kupewa RB iliyosomeka KJN/BR/6950/2010 Shambulio la mwili.
ShowBiz inawapongeza mastaa hao kwa kuimaliza ishu hiyo kiutu uzima na kuendelea kupiga kazi pamoja, wawe mfano kwa wengine kwakuwa bifu hazijengi.

**************************************
Gemu la Bongo sasa ni Swaga tu, Meseji zao leo ni kukopi na kupesti
Wakati Mwenyezi Mungu kupitia vitabu vyake anaagiza kuwa asiye fanya kazi na asile, binaadamu nao kwa upande wao wamelitii hili na kuingiza yao wakisema kwamba, baada ya kazi faraja. Wengi watajiuliza kwanini tumetoa mfano huu, ili kufahamu nini tunamaanisha shuka na Hemed Kisanda wa ShowBiz.

Unaweza kuuchukulia tofauti usemi huo lakini maana kubwa inayousimamisha ni kuwa baada ya majukumu ya kutwa nzima binadamu wengi hukutana sehemu mbalimbali za burudani ili angalau kupunguza uchovu na hata kupoteza mawazo.
Tunapoizungumzia burudani ni pamoja na muziki, filamu pamoja na nyingine ambazo zina wapenzi wengi ama watu hupenda kuburudika nazo baada ya kazi.

Sisi kama wadau wa burudani nambari ‘wani’ leo tunaitazama sanaa ya muziki hasa wa kizazi kipya ambao uko juu na unaendelea kupaa hewani huku ukiwatoa vijana wengi kwenye umasikini na kuwapatia ajira inayowasaidia kusukuma gurudumu la maisha na familia zao kwa ujumla.

Na unapoizungumzia game hiyo huwezi kukwepa kutaja jina hata moja la mshiriki wa sanaa hiyo, nazungumzia wasanii wake kama Fareed Kubanda a.k.a Fid Q, Sara Kais Shaa, Hamad Ally ‘Madee’ na wengine kibao ambao bado wanakomaa katika fani. Lakini je umewahi kujiuliza ni kwanini muziki huo bado unaendelea kuwa juu? Inawezekana kabisa si kwa sababu nyimbo za sasa zina ujumbe mzito au unaoelimisha zaidi lakini ukweli ni kwamba kazi nyingi katika muziki wa kizazi kipya zinabebwa na swaga (staili) tu za wasanii wa sasa.

Hakuna jipya katika nyimbo zao kwa maana ya ‘meseji’ wanazoimba leo zilishaimbwa toka miaka hiyo wanachokifanya ni kama ‘kukopi na kupesti’ tu lakini ni yale yale yaliyokuwa yakiimbwa na akina Marijani Rajabu.

Hili liko wazi kwani hakuna asiyejua nyimbo za kuwasifia wanawake ama kulilia mapenzi zilizokuwa zinaimbwa na Hayati Hemed Maneti, na ni kipya gani alichokiimba Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenye nyimbo zake za sasa .

Mwisho wa yote tunakuja kugundua kuwa utamu wa muziki wa leo unalindwa na Swaga tu za wasanii lakini bado hawajaimba kitu kipya. Kwa kusema hayo tusieleweke kuwa tunawapuuza, ni mtazamo tu .

*****************************************

Dully atibua shoo ya Akudo
Bongo Flava icon, Abdul Sykes a.k.a Dully Sykes, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya ‘madudu’ ya mwaka baada ya kuvamia steji na kumnyang’anya kipaza sauti ‘Prezdaa’ wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’, Christian Bella a.k.a Obama.

Dully ambaye pia anajulikana kwa jina la Mista Misifa, alifanya kioja hicho ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni Dar, wakati Bella alipokuwa stejini akitoa burudani kwa mashabiki wake, jambo lililoushangaza umati uliofurika ukumbini hapo na kumkodolea jicho ili kutaka kujua lengo lake.

Baada ya kukwapua kipaza sauti hicho Dully anayetamba na wimbo wa ‘Shikide’ alianza kuimba nyimbo za bendi hiyo huku akijikanyaga jambo lilowafanya kumzomea na kumtaka kushuka stejini hapo.

*****************************
Dudu, Kabago wazidi kutokomea Mwanza
Kutoka pande za Rock City (Mwanza) msanii Godfrey Tumaini a.k.a Dudubaya ambaye ameamua kupiga kambi mkoani humo ameendelea kutokomea ndani zaidi ili kuwafuata mashabiki wake walioko mbali.

Akipiga stori na ShowBiz kwa njia simu kutoka pande hizo, Dudu alisema kwamba ameamua kupiga kambi mkoani humo kwakuwa ni nyumbani kwao na kuendelea kutokomea kwenye vijiji vya mbali kwa ajili ya burudani kwa watu wake wa huko.

“Kwa mfano Ijumaa hii (leo) mimi na wanangu tutakuwa Ukerewe na kupiga shoo katika Ukumbi wa Kondeni Beach kabla ya kuelekea Misungwi siku inayofuata (kesho). Katika shoo hizo nitakuwa na wasanii kama Phillbet Kabago, Mr. Hill na ‘kru’ nzima ya Michano Time kutoka Passion FM,” alisema Dudu.
********************************

Bamiza Top 20 ZA MAGIC FM 92.9 FM
1. Teja - Lady JD (1ST WEEK ON NO.1)
2. Mama ntilie - Jerry/Ray c/AT (2 WEEKS ON NO.1)
3. Karibu tena - Joh Makini
4. Bado tunapanda – Tip Top connection (3 WEEKS ON NO.1)
5. Chembambament - Noorah/Ngweair
6. Salasala - Godzila
7. Unikimbie - Amini
8. Ngosha the swaga Don - Fid Q
9. Sina raha - Sam
10. Nauza kura yangu - Bonta
11. Shoga - Shaa (3WEEKS ON NO.1)
12. Tamaa mbaya – 20%
13. Kisiwa cha ma lovidavi – Z-Anto
14. Iveta - Sajna
15. Demu wangu - Jaffaray/TID (2 WEEKS ON NO.1)
16. Mtoto mtundu - Juma Nature
17. Mechi za ugenini – Roma
18. Budget – LWP
19. Mkono mmoja - Chege,Temba ft Wahuu (3WEEKS ON NO.1)
20. Hello – Hussein Machozi & Maunda (NEW)

Compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: