Wednesday, October 20, 2010

ALIKIBA KWENDA USA

Christine Mosha 'Seven' (kushoto) akiongea na wanahabari kuhusu safari ya Ali Kiba (kulia)
Mwanamuziki bora wa Kitanzania Ali Kiba anatarajiwa kwenda Chicago nchini Marekani kuungana na wanamuziki wengine maarufu wa Afrika kuunda kundi bora la muziki la Afrika linalojulikana kama ONE8 linalojiandaa kurekodi na mwanamuziki bora wa R&B Duniani.

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwa wanamuziki wa Afrika kuungana kama ilivyotokea hivi.Ushirikiano huu wa nyimbo pamoja na Video umeonyesha ushirikiano mzuri wa Afrika na Nchi za Nje.Kundi la ONE8 ndiyo mshiriki mkuu katika mpango huu na wanashirikiana kwa karibu zaidi na kwa usawa na mwanamuziki bora wa R &B wa marekani mwenye makazi yake jijini Chicago akiwa na timu yake ambao wamefurahishwa sana kufanya kazi na wasaanii hawa kutoka Afrika.

Ali Kiba ni mfalme wa Bongo Flava na ni msanii bora kabisa nchini Tanzania.Japokuwa Ali Kiba alitoa Albam yake ya kwanza mwaka 2008 amefanikiwa kuwa mmoja wa wanamuziki bora barani Afrika, pamoja na nchi nyingi za barani Ulaya na Marekani.Kwa mauzo Ali Kiba albam yake ya kwanza Ali kiba ilipata mafanikio makubwa Afrika mashariki kwa kuwa ndio albam iliyoongoza kwa mauzo katika ukanda huu.Ali Kiba anatarajiwa kuwa nguzo muhimu katika kundi la ONE8.

Wakati wanamuziki wote 8 kutoka Afrika wakiondoka kwenda nchini Marekani, mashabiki wa muziki duniani kote wataunganishwa nao kupitia mitandao mbalimbali kama vile Facebook, Twitter, Flicker na Youtube.

Wanamuziki wengine kutoka Afrika wanaounda kundi la ONE8 ni Amani kutoka Kenya, Navio-Uganda, Fally Ipupa-RDC, 2 Face-Nigeria, JK-Zambia, 4 x 4-Ghana na Movaizhaleine kutoka nchini Gabon.

Picha/story: Fullshangwe blog

No comments: