Ule wakati wa kuicheki ile muvi iliyopata kuwa gumzo ndani na nje ya Tanzania ilipokuwa ikiandaliwa, Tears on Valentine Day sasa umewadia, iko tayari, muda wowote kuanzia sasa itadondoka kitaani.
Kwa mujibu wa msemaji kutoka Tollywood ambao ndiyo waandaaji wa filamu hiyo, ni kwamba mzigo wote umeshawasili kutoka China ambako ulikuwa ukifanyiwa kazi kwa mara ya mwisho baada ya zoezi la upigaji picha lililofanyika Bongo kukamilika.
“Filamu hiyo ambayo imewashirikisha baadhi ya mastaa na wasanii wapya wanaokuja juu kunako tasnia ya muvi nchini ilienda kufanyiwa marekebisho ya mwisho China ikiwemo kutoa kopi za DVD na VCD, ndiyo maana imechukua muda mrefu. Kwakuwa sisi ni kampuni kubwa ya kuaanda filamu Bongo, Tollywood hatujashangazwa na muda huo kwakuwa tunahitaji kufanya kitu bora zaidi na siyo bora filamu,” ilisema taarifa kutoka Tollywood.
Aidha, waandaaji hao wamesema baada ya mzigo kuwasili nchini kinachofuata ni kupanga tarehe maalum ambayo wataudondosha sokoni ili kila mpenzi wa muvi za Kibongo ajipatie kopi yake na kushuhudia mapinduzi katika tasnia hiyo ambayo hivi sasa iko juu ndani na nje ya Tanzania. Kaa tayari kwa muvi hiyo ya kijanja.
***************************************************************
Wote walizaliwa Januari 1981, umri wao ni miaka 29. Tofauti ni kwamba Mashonda alianza kuliona jua kabla ya mwenzake, alichomoka kwenye plasenta Januari 9 wakati Alicia zamu yake ilikuwa Januari 25.
Kuhusu kipaji, wote wapo sawa. Wanakubalika na wanauza ingawa anapotafutwa nani anayeng’ara sokoni kati yao, Alicia anabaki nafasi ya kwanza.
Mashonda hapingi hilo, anakubali kwamba Alicia yupo juu na anafafanua kwamba alikuwa shabiki wake lakini kitendo cha kumchukulia mume wake, kimemuudhi na kumuachia majeraha moyoni.
Anaamini Alicia ni mwanzo wa kusambaratika kwa familia yake. Mwanaye mwenye umri wa miaka mitatu, Kasseem Jr amekosa malezi bora ya baba na mama kwa sababu ya mwanamuziki mwenzake.
Kimsingi, Mashonda na Alicia walianza vita tangu mwaka jana na mpaka leo hakuna kinachoweza kuwafanya wapatane kwani kila mmoja anamponda mwenzake kwa staili anayoweza, madongo mengi wanatumiana kupitia kurasa zao za Twiter.
MADAI YA MSINGI
Mashonda anamtuhumu Alicia kwamba akijua yeye ni mke halali wa Prodyuza Swizz Beatz, alianzisha uhusiano naye wa kimapenzi, hivyo kusababisha atengane naye.
Mashonda anasema: “Nilikuwa shabiki wa AK (Alicia Keys), wote tuliingia mkataba na Lebo ya J Records na nikawa nafuatilia mradi wake. Niliimba nyimbo zake na ilivutiwa na ubunifu wake katika nyimbo za Superwoman na Karma, sikuwahi kumpinga wala kukataa kipaji chake.
“Nilimuamini mpaka nilipogundua kwamba kuna uwezekano mkubwa akawa amefanya mapenzi na mume wangu. Uhusiano wao ulikataliwa mpaka mwishoni ndiyo wakakubali kuweka wazi.
“Kuna watu nimewasikia wakiniponda, wanamtetea AK kwamba hakuna mtu mwenye uwezo wa kumshawishi mtu amuache mke wake, eti huwezi kuvunja kitu kilichovunjika. Already I can.
“Sawa ndoa yangu haikuwa imevunjika kabla ya AK. Ninachojua mimi tulikuwa tunafurahi kuzaliwa kwa mtoto wetu, pia tukawa tayari kusherehekea miaka mitano ya ndoa yetu.
“Namlaumu AK kwa sababu mimi na mume wangu tulikuwa tumemaliza tofauti zetu na tukawa kwenye maelewano mazuri. Nimekubali matokeo na namshukuru Mungu.”
BARUA YA WAZI YA MASHONDA KWA AK
Aliandika: Kilichopo kwangu kuhusu AK, siyo ukweli kwamba amesababisha kuiharibu familia lakini amefanya kitu kibaya mno, kwa ubinafsi akalazimisha kuwa na mtu wakati anajua ni mume wa mtu mwingine.
Kama unasoma hii Alicia, acha nianze kwa kukwambia kwamba unajua kile ulichokifanya. Unajua ulivyohusika na unajua ulivyochangia ndoa yangu kuvunjika.
Unajua niliwahi kukwambia ukae mbali na Swizz na uniache nilee familia yangu na matatizo ambayo ulichangia kutokea. Sijasema kila kitu muda wote kilikuwa sawa ila nataka nikwambie kuwa hakuna uhusiano uliokamilika. Ukamchukua mume wangu kwa lipi? Au ndiyo tafsiri ya wimbo wako wa Superwoman ambao niliupenda na kuuimba mara kwa mara?
AK NAYE AMPAKA MASHONDA
Katika ukurasa wa Twiter, AK alitoa mada kwa mashabiki wake waweze kuijadili. Ilihusu mapenzi na moja ikaonekana alilenga kumchana Mashonda.
Mada ilisema: “Katika mapenzi ni bora kwenda kwa chaguo bora au kwa chaguo lililochakaa?”
Mashonda alipoona hiyo na jinsi wachangiaji walivyotoa maoni yao, ilionekana amelengwa yeye ndiyo maana aliandika barua ya wazi kwenda kwa AK.
SWIZZ AMTUNDIKA MIMBA AK
Kwa sasa AK ni mjamzito na katika intavyuu ya hivi karibuni, Mashonda ameamua kukubali yaishe.
“Nikikutana na Swizz, hapo nakuwa nataka tuzungumze matunzo ya mtoto, siyo vinginevyo. Sihitaji mwanangu awe na mtu yeyote, kwa hiyo nahitaji kuketi faragha na Swizz kwa ajili ya mtoto.
“AK mwenyewe ana mimba, ataona hilo ila hata kwake anahitaji faragha. Upendo na amani.”
“Namtakia mafanikio makubwa, mimba yenye afya hapa duniani. Mtoto wake atakuwa ndugu wa mwanangu, dada au kaka na hiyo ndiyo pekee ya kuangalia.”
EBWANA DAH!
Kwa mujibu wa ‘site’ ya kijanja inayoangalia uhusiano wa mastaa pande za mbele, Swizz Beatz ndiyo mwanaume pekee wa Mashonda. Alicia, yeye anahusishwa kutoka kimapenzi na wanaume wawili, Crucial Keys kati ya mwaka 1994 hadi 2008 kabla ya kudondokea kwa Swizz Beatz ambaye tangu mwaka 2008, anaendelea naye mpaka sasa.
Wasifu wa kimapenzi wa Swizz Beatz, unamuonesha Mashonda kwamba ndiye mwanamke wake wa kwanza kisha Alicia, baada ya hapa hana mwingine anayejulikana.
Kundi la muziki wa dansi la Mapacha watatu linaloundwa na Junior Hamza ‘Kalala Junior, ’Joseph Michael ‘Jose Mara’ na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’ hivi karibuni litasimama kwenye steji moja na Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’ pale watakapokutana katika jukwaa moja.
Mpango mzima utakuwa Oktoba 15, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo mapacha hao watazindua albamu yao ya kwanza inayoitwa Jasho la Mtu yenye nyimbo kama vile Private case, Kipaji Changu, Shika Ushikacho, Mhudumu, Nyumba ndogo na Imebaki stori.
Akipiga stori na safu hii meneja wa shughuli hiyo, Hamis Dakota alisema kuwa taratibu zinakwenda vizuri na kinachosubiriwa ni siku hiyo ifike ili vijana hao waweze kutoa kile ambacho mashabiki wao wanakitarajia.
“Itakuwa ni mara ya kwanza kundi hili kufanya shoo ya pamoja na Twanga hivyo tunatarajia burudani ya aina yake, siyo shoo ya kukosa,” alisema Dakota.
Aliongeza kuwa, mbali na Twanga pia atakuwepo Mzee Yusuf wa Kundi la Jahazi Modern Taarab ambaye atanogesha uzinduzi huo.
Msemaji wa ‘event’ hiyo Tayana Amri aliiambia safu hii kuwa, kutakuwa na ratiba ya kila taifa kuonesha filamu tatu kila siku kuanzia siku ya kwanza ya tamasha hilo Oktoba 14, ndani ya Ukumbi wa New World Cinema Mwenge huku pia likifanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar kwa siku za wikiendi. Tayana alizitaja baadhi ya filamu zinazotarajiwa kung’ara kuwa ni Sunshine Barry & The Disco Worms, Flame & Citron na The Commitments za nchini Denmark.
Kutoka Tanzania filamu za Yatima wa Roho, Vita na Unsung Heroines inayohusu maisha ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro zitaoneshwa.
Mataifa mengine yanayotarajiwa kushiriki katika tamasha hilo ni Ubelgiji, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Norway, Urusi, Sweden, Uswisi, Uingereza, Uholanzi na Hispania.
compiled by mc george/wikienda
No comments:
Post a Comment