Monday, October 11, 2010

BURIANI ABDALLAH 'ABUU'

baadhi ya wafanyakazi wenzie marehemu wakiwa msibani, mbele ni Mhariri wa Channel ten, Dina Chahali na kulia ni Resty Ngonyani
Mh. Idd Azzan (katikati), naye tulikwa naye
..mtoto wa marehemu, Yunus Abdallah (5)

Kamal Mussa (mwenye fulana no 24) ndiye aliyekuwa na marehemu safarini
mwili ukitolewa msikitini
...waombolezaji katika majonzi
mke wa marehemu akimuaga mpendwa wake...dua ya mwisho ya kumuombe marehemu makaburi.

Aliyekuwa mtangazaji wa Channel Ten na Magic FM, Abdallah Ramadhani, amezikwa jioni hii baada ya kufariki dunia katika ajali ya gari mwishoni mwa wiki iliyopita. Mazishi yake yalihudhuriwa na watu wengi kutoka kada mbalimbali, wakiongozwa na wafanyakazi wenzake. Mungu alitoa na Mungu ametwaa, jina lake lihimidiwe na ailaze roho ya marehemu peponi - ameen!

No comments: