Friday, September 10, 2010

MVUA YA MAWE MAKUBWA YANYESHA SAUDIA




Imeripotiwa kunyesha mvua ya mawe makubwa katika mji wa Bardia, nchini SAUDI ARABIA mapema mwezi huu. Mawe yaliyokuwa yakidondoka kwenye mvua hiyo yalikuwa makubwa kiasi cha kuvunja vioo vya magari na kutanda barabarani. Wanasayansi, naomba mtujuze mvua ya mawe husababishwa na nini, au nayo ni miongozi mwa miujiza ya Mungu?

'P. DIDDY' AZIKWA, MAJONZI YATAWALA!


Ben Kinyaiya akitoa heshima zake za mwisho kwa majonzi mbele ya jeneza la P. Diddy
Ben Kinyaiya akilia kwa uchungu huku akitulizwa na rafiki yake

...majonzi matupu

Mkurugenzi mwenzie na marehemu, Judith Mosha, akilia kwa uchungu
Msanii wa filamu, JB (kulia) akiongea na mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Kalala Junior
Mwanamuziki wa FM Academia Nyoshi (kulia) akiwa na jamaa zake msibani
Jack Pemba (kulia) akiwa na Jerry Muro msibaniBen akiwa katika dimbwi la majonzi
'Kimwana Manywele' (kulia) na mwenzie akiwa katika majonzi
...wakiwa wamepoteza fahamu
....Aunty Ezeckiel....akilia na warembo wenzie (chini)
Dansa wa Twanga Pepeta, Super Nyamwela, akimfariji mwenzie msibaniMUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI - AMEEN!

IJUMAA SHOWBIZ!

Kala aibuka na viatu rangi mbili, ajifananisha na Kriss Kross!
Kutokana na ushindani uliyopo kunako sanaa mbalimbali ikiwemo game ya muziki wa Bongo Fleva unawafanya wasanii wengi kuwa wabunifu ili kuwavutia mashabiki wao, kitu ambacho kimewafanya baadhi yao kufanikiwa.

Kala Jeremiah ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Fleva ambaye ameibuka na kali ya mwaka kwa kuvaa viatu vyenye rangi mbili tofauti (chekundu na cheusi) ikiwa ni staili yake mpya ya uvaaji baada ya kupotelea Uganda kwa kipindi fulani kabla ya kurudi Bongo na ngoma kadhaa.

“Kaka nimeamua kuja kivingine kama walivyokuwa Kriss Kross, siunajua tena mambo ya ubunifu, lazima kwenye game uwe mjanja,” alisema Kala ambaye wiki iliyopita ameachia ngoma yake mpya yenye jina la Miss Uganda itakayofuatiwa na video yake ambayo pia imepigwa pande hizo za UG.



Rihanna Ashitua na ‘Tattoo’ ya bastola!
Staa wa muziki ambaye chati yake bado iko juu, Rihanna Fenty amebadilisha tattoo aliyokuwa nayo kwenye paja na kuweka mpya yenye mchoro wa bastola ambayo imeonesha kuwashitua wengi huku baadhi yao wakidhani huenda akawa na hisia za kuwa mjeshi hapo baadaye.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22- ambaye anatamba na ngoma yake, ‘Te AMO’ mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa katika fukwe za Hawaii alionesha mwili wake ukiwa katika hali mpya hasa baada ya kubadilisha tattoo hiyo ya bastola.
Kwa mujibu wa Gazeti la ‘The Sun,’ Rihanaa (kama anavyoonekana pichani), alionesha mwili wake alipokuwa amevalia vazi la ufukweni ‘bikini’.

Hata hivyo, mashabiki wa staa huyo wametakiwa kutomhofia kuhusu tatoo hiyo kwani ametumia hina kuchora na huenda ikawa ni ya muda tu.
Lakini pia wapo waliosema kwamba, huenda tattoo hiyo ameichora kwa sababu ya filamu yake mpya, ‘Battleship’ ambayo ipo katika maandalizi ya nguvu.

FM Academia Kumtambulisha Hafsa Kazinja Idd Mosi
Msanii Hafsa Kazinja anatarajia kutambulishwa rasmi siku ya Idd Mosi wakati Bendi ya muziki wa dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ itakapokuwa inazindua albamu yao ya pili, Vuta Nikuvute Mathematics Mayemba ndani ya Ukumbi wa Diamond jubilee.

Akipiga stori na ShowBiz juzi pande za Mwanayamala katika kambi yao ‘Prezidaa’ wa Ngwasuma, Nyoshi El- Saadat alisema kwamba kupitia uzinduzi wa albamu hiyo wamepania kuweka historia isiyofutika kwa mashabiki wote watakaohudhuria shoo hiyo kutokana na maandalizi ya kufa mtu waliyoyafanya.

“Tutamtambulisha malkia mpya wa Ngwasuma, Hafsa Kazinja ambaye ataziba nafasi ya muimbaji wetu wa kike aliyeachana na shughuli za muziki na kujikita zaidi kwenye masuala ya kulea familia zaidi. Kutoka Kenya msanii David Mathenge ‘Nameless’ atakuwepo kwa ajili ya kutusapoti,” alisema Nyoshi.

compiled by mc george/ijumaa

Tuesday, September 7, 2010

UTAJUAJE UNA UPUNGUFU WA MAJI MWILINI?


Umeshawahi kwenda hospitali kumlalamikia daktari kuwa mwili wako hauna nguvu na unajisikia kuchokachoka sana na baada ya kukuchunguza, akakwambia huna tatizo lolote isipokuwa una upungufu wa maji mwilini tu?

Mwili kuishiwa nguvu huwa ni miongoni mwa dalili za upungufu wa maji mwilini na chanzo kikiwa ni wewe mwenyewe kutopenda kunywa maji. Ni kawaida kwa baadhi ya watu kutokunywa maji hadi pale wanaposikia kiu.

Katika makala ya leo, nitakujuza dalili za mwili kuishiwa maji ambazo hujitokeza na kukuhimiza kunywa maji hata kabla hujasikia kiu. Uonapo dalili hizo, hupaswi kuzipuuzia bali kunywa maji kwa wingi tena haraka.

UPUNGUFU WA MAJI MWILINI NI NINI?
Pale mwili unapopoteza kiasi kingi cha maji kwa njia mbalimbali, ikiwemo jasho na mkojo, mwili hupungukiwa maji na hivyo mtu huyo huambiwa ana upungufu wa maji. Tunaelezwa kuwa karibu theluthi mbili ya miili yetu imejaa maji.

Ili mwili uweze kufanya kazi yake vizuri, kiwango cha maji mwilini hakipaswi kupungua hata kidogo, hivyo kila mtu ana wajibu wa kunywa maji ya kutosha kila siku ili kulinda kiwago chake cha maji kisipungue na kinapopungua ndipo hapo mwili huanza kuonesha dalili za kukaukiwa maji (dehydration).

NINI HUSABABISHA?
Sababu zinazosabababisha mwili kukaukiwa maji huweza kuwa nyingi, lakini zinazojulikana zaidi ni pamoja na:
Kuacha kunywa maji
Kukaa kwenye joto kwa muda mrefu
Kunywa kiwango kikubwa cha pombe,
Ungonjwa wa kisukari ambao husababisha mtu kukojoa mara kwa mara
Kutokwa na jasho jingi, kwa sababu ya ama kufanya kazi ngumu au mazoezi. Hivyo inashauriwa mtu anayetokwa jasho jingi kunywa maji mara kwa mara wakati akiendelea na shughuli inayomtoa jasho.
Kama ukiugua au ukipatwa na homa kali, huweza kupungukiwa na maji mwilini
Kutapika na kuharisha nako huweza kupoteza maji mwilini.

DALILI ZA KUKAUKIWA MAJI KWA WATOTO
Kwa kawaida, dalili za upungufu wa maji mwilini hujitokeza zaidi kwa watoto wadogo kuliko watu wazima au wazee. Dalili za upungufu wa maji mwilini kwa watoto huweza kusabababishwa ama na kuharisha, kutapika, kutokunywa maji au vimiminika vingine vya kutosha.
Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji huweza kuonesha dalili zifutazo:

Kukojoa mara chache sana
Mtoto kutokuwa mchangamfu
Macho, tumbo au mashavu kubonyea
Mdomo na ulimi kukauka
Mtoto kulia mara kwa mara na anapolia machozi hayatoki.

DALILI ZA UPUNGUFU WA MAJI KWA WAZEE
Dalili za upungufu wa maji kwa wazee ni tofauti na watu wazima. Wazee wa umri zaidi ya miaka 60 huwa na ngozi iliyosinyaa na hata ukiiminya, hubaki katika hali hiyo kwa muda na unapoikwaruza alama hubaki.

Halikadhalika, wazee hukosa haja ndogo kwa muda mrefu, hupungukiwa uzito kwa kiasi kikubwa na hupatwa na homa.

DALILI ZA UPUNGUFU WA MAJI KWA WAJA WAZITO
Upungufu wa maji mwilini kwa waja wazito ni hatari kwa mama pamoja na mtoto. Dalili zinazoweza kujitokeza kwa waja wazito ni pamoja na:

Kukojoa mkojo wa njano nyeusi
Kuumwa na kichwa
Mwili kukosa nguvu
Kichefuchefu na kutapika
Kukaukwa na mdomo
Ili kujiepusha na matatizo ya upungufu wa maji na hatimaye kujikuta unakumbwa na dalili kadhaa zilizoelezewa hapo, ambazo ziko pia kwa watu wazima wengine, ni kuwa na mazoea ya kunywa maji ya kutosha kila siku. Hata utakapozidiwa na kukimbizwa hospitali, hakuna dawa nyingine utakayopewa zaidi ya maji (re-hydrating solution). Kwa nini usubiri hali hiyo ikutokee wakati unaweza kuizuia kwa kunywa maji tu?

MASIKINI MWISHO!



Tanzania
’s Mwisho and Zambia ’s Paloma up for eviction this week on M-Net’s Big Brother All Stars after Monday’s (6 September) nominations. For the first time in five consecutive weeks, Munya is not in danger of leaving the Big Brother All Stars House this weekend – while Paloma finds herself up for eviction for the first time since week one, when all the housemates stood the chance of leaving.

Once all the nominations were in, Big Brother told the Housemates that Head of House Meryl and her beau Mwisho had received the most nods from the Housemates. Summoned to the Diary Room to make her Head of House decision, Meryl hovered outside the door and asked to go to the toilet before heading inside. Once she was in the Diary Room, she was clearly distressed at having to choose between herself and ‘boyfriend’ Mwisho. She asked Big Brother for a moment after declaring “I can’t do this!”. After much hand-wringing, she decided to save herself and put Paloma up in her place.

· Earlier in the day, Munya had changed his mind after nominating Uti and Mwisho, and put Meryl in Mwisho’s place. Munya has been using the same strategy at nomination since week one, nominating the Housemates who come from the countries furthest from Zimbabwe . At first he said he was nominating Meryl because she was one of the Housemates that came from a country furthest from Zimbabwe but Big Brother would not accept that reason. He then said that his instinct was that “In the best interest of the game, if people I want to stay are to stay then I should nominate her,” he said.

· Meryl later nominated Munya, calling him “The Diamond Boy”, citing no specific reason for nominating him. She also named Kaone, who she said she had to nominate for the purposes of her alliance. Mwisho also nominated Munya and Kaone, saying that he did not like “nominating chicks”. Noting the coincidence between his and Meryl’s nominations, Big Brother asked him if he had discussed his nomination with anyone else in the House or if anyone else was nominating the same people, to which he responded in the negative. Asked why he hadn’t nominated Uti, Mwisho replied that Uti was his friend.

· Jennifer nominated Munya and Mwisho because they were the only two people she did not feel close to. Though she calls Mwisho as her “Dad”, Jennifer told big Brother that she wasn't close to him. Paloma nominated Meryl because she could save herself as Head of House – or save Mwisho if need be.

· Kaone nominated Meryl for the same reason, along with Uti because of their “relationship”. When Big Brother questioned the status of the relationship, Kaone was reluctant to spill the beans. He told Big Brother that Uti was his brother but it was time for them to start nominating each other, adding that he felt that he finally had the freedom to nominate Uti. Big Brother refused to accept that reason, forcing Kaone to refer to his nomination session as an interrogation. Uti didn’t nominate Kaone, instead choosing Jennifer and Paloma because neither had faced eviction before.

· Sheila and Lerato both declared that they would like to see Paloma in The Barn. Lerato also nominated Jennifer to see if she would survive being up for eviction, saying that she was too complacent and comfortable in the House. Sheila also nominated Jennifer, saying that she didn’t trust the Mozambican.

· Code said he felt Mwisho was getting too comfortable in the House, while Tatiana nominated Mwisho and Uti because she’d rather keep the people that she’d been close to while she was still in the House, in the game. Code also nominated Meryl because she was the Head of House.

· Hannington nominated Meryl for the same reason before naming Kaone as his other choice. He had no reason for putting Kaone up but it was just the first name that came into his head. When Big Brother dug deeper, Hannington said it would be interesting to see Kaone in the Barn.


Big Brother All Stars is broadcast live 24/7 for the next 41 days on DStv Channel 198, with edited highlights shows every day of the week on M-Net and later on AfricaMagic. Big Brother All Stars is also available on DStv Mobile in Ghana , Kenya , Namibia and Nigeria .

You can vote to keep a nominated housemate in the house in three different ways:

1. Via the website, or the WAPsite on your mobile phone.

2. By sending an SMS

3. Using MXit

To vote on the website: Cast your vote by clicking on the housemate who you want to keep in the house.
(You can vote once per hour per registered email address.)

To vote via SMS: send the word VOTE followed by the housemate's name to the number for your country (displayed below). For example if you are voting from Botswana send Vote Thato to 15626. SMSes are charged per specified network tariffs in the various countries. VAS rates apply. Free minutes do not apply.
(You can vote 100 times by SMS per mobile number during each voting period.)

Tanzania

Vodacom 15726 Tsh 600

Celtel 15726 Tsh 600

Tigo 15726 Tsh 600

Zantel 15726 Tsh 600

SASATEL 15726 Tsh 600

To vote using MXit: open the browser on your WAP-enabled mobile phone, and type in www.mxit.com/wap to download MXit for free. Then locate MXit on your phone in the applications or games section and register. Once in MXit, go to Tradepost -> Voting -> Big Brother Africa . (Voting on MXit is free and you can vote up to 10 times on MXit per voting period.)

To vote using WAP [www.mnetafrica.com/bigbrother]: Register on the Big Brother network. (Vote on the website or wapsite for free, once per hour during the voting period.)

Voting begins immediately after the Nomination show has been screened at 21:30 on Monday nights (M-Net East and West). Voting closes at 07:00 on the following Sunday morning.

Find out who has received the least number of Votes and will be evicted by watching the Eviction Show on Sunday nights.

Monday, September 6, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Marichuy Kajiachia na midume hawa
Kutoka ndani ya tamthiliya maarufu ya Cuicado el An Angel inayofahamika zaidi kama Marichuy inayoendelea hivi sasa kunako Kituo cha Telivisheni cha CAPITAL, Ebwana Dah ilidondoshewa maombi kibao na wasomaji wakitaka kufahamu staa wake wa kike, Maite Perroni a.k.a Marichuy amewahi kutoka na wanaume wangapi.


Sisi kama wadau namba moja wa burudani, leo tunashuka na mwanadada huyo mrembo bila kusahau idadi ya wanaume aliyowahi kuangusha nao gari on bed. Wa kwanza kabisa kufungua pazi na Maite ni Guido Laris, ambaye alijikabidhi kwa mrembo huyo wa Mexico kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2005 hadi 2008.


Baada ya hapo kijiti kikachukuliwa na William Levy a.k.a Juan Miguel aliyedumu naye kwa miezi kadhaa kabla ya mwaka 2009 Eugenio Siller kuchukua usukani, ingawa naye kama ilivyokuwa kwa William, alikaa naye kwa miezi michache na kuachia ngazi.
Carlos De la mota ndiye anayemmiliki mlimbwende huyo mpaka sasa, tangu alipomtwaa mwaka jana kutoka kwa Eugenio Siller. Ni hayo tu wakubwa!!!
**************************************
Kabago Kumrudisha Farida kideoni
Kutoka pande za Rock City (Mwanza) aliyekuwa memba wa Kundi la BWV, Philibert Kabago amesema na Abby Cool & MC George over the weekend kwamba, siku kadhaa zijazo anatarajia kumrudisha mwanadada aliyepotea kwenye game kitambo, Farida.

Akipiga stori na safu hii juzi kati, kwa njia ya simu Kabago alisema kwamba atarudi na binti huyo kupitia video ya ngoma yake, Wivu ambayo ilitoka miezi kadhaa iliyopita ikimshirikisha msanii huyo ambaye hivi sasa ni mama wa mtoto mmoja.

“Tayari video hiyo imeshakamilika, siku chache zijazo nitaiachia hewani ili kuipa sapoti albamu yangu mpya ambayo pia iko tayari. Vilevile kwa upande wa audio nimetoa ngoma mpya yenye jina la Wameshikika ambayo ilifanyika pande za Uganda, kitakachofuata bada ya hapo ni jiwe juu ya jiwe kwa sababu sitaki kuwaangusha mashabiki wangu kwa kukaa kimya muda mrefu bila kuwadondoshea kazi mpya,” alisema Kabago.
*******************************************
Kwenye dansi kuna wakongwe, vipi Bongo Fleva?
Imekuwa kawaida kwa wanamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi kutambulishwa kwa title zao, lakini hali ni tofauti sana kwa wakongwe katika game ya Bongo Fleva, Abby Cool & MC George over the weekend wanakuwekea mambo sawa.

Ni rahisi sana kusikia Maalim Ngurumo, King Kikii, Shaban Dede, Hamza Kalala, Hassan Rehani Bichuka na wakali wengine wa muziki wa dansi, wakiitwa kwa sifa zao za ukongwe, lakini tumesahau kwamba, hata kwenye Bongo Fleva tuna wakongwe!

Ni heshima na fahari kubwa kuwaenzi wakongwe wa Bongo Fleva. Wasanii kama Solo Thang, Profesa Jay, Afande Sele, Mabaga Flesh, Uswahili Matola, Juma Nature, Balozi, Mchizi Mox, Mr. II ‘Sugu’, Dudubaya na wengineo, wanatakiwa kupewa heshima yao kama wakongwe.

Kiukweli haipendezi tukiwaita wanamuziki wa Bongo Fleva wakati wao ni miongoni mwa waasisi wa muziki huo, inakuwa tamu hata kuandika; “Mkongwe katika game ya Bongo Fleva Soggy Dog...” kuliko kuandika bila kumpa title yake.

Haiwezekani utambulisho wa msanii kama Diamond aliyetoka juzi kati, uwe sawa na wakongwe kama Mr. Paul, Mez B, Caz T, Mike T na wengine wakali walioanza game kitambo.

Meseji hii iende moja kwa moja kwa watangazaji wa redio na runinga, waandishi wa habari na wadau wote wa muziki wa kizazi kipya. Tuwape heshima zao wakongwe pale inapotakiwa kufanya hivyo.
*******************************************
K-Sher aibuka na mapya kuhusu kusimamishawa Tip Top
Mtiti ndani ya Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, bado unaendelea na stori kubwa ni juu ya First Lady wa Kundi hilo, Khadija Shaban a.k.a K – Sher amejitoa au amefukuzwa na hapa Keisha ameibuka na kumwaga mapya manne.

Akigonga interview na Abby Cool & Mc George Over The Week end, juzi kati kwa njia ya simu, K – Sher amesema Kiongozi wa Kundi hilo Babu Tale anatakiwa aongee ukweli, kwani anaficha-ficha mambo, lakini alifafanua mambo muhimu manne.

“Kwanza siwezi kufukuzwa Tip Top kwa sababu uwezo wangu unajulikana, ukweli ni kwamba nikitoka, basi kundi litayumba sana, coz nina mchango mkubwa kimuziki. Mimi nimejitoa mwenyewe na sababu kubwa ni kwamba sina imani na uongozi.

“Babu Tale asiongee uongo na kama wanahitaji nirudi, sharti la kwanza kabla ya mazungumzo mengine, Babu Tale anilipe pesa zangu 480,000 ambazo ni madeni ya pesa alizokuwa akinisainia baada ya shoo na kuniletea pungufu, mwisho siwizekulumbana nao kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya kuongeza uchumi wa taifa letu,” alisema K- Sher.

Kwa upande wake Babu Tale alikuwa na haya ya kusema: “Kaka nina mambo mengi sana ya kufanya, nipo ‘bize’ na maandalizi ya uzinduzi wa albamu mpya ya Tip Top, utakaofanyika Idi Mosi, kwahiyo muda wa kulumbana sina kabisa.”
*******************
MKALI wa miondoko ya TAKEU Bongo, Hamisi Baba a.k.a H- Baba, ameibuka na kutambulisha staili mpya ya muziki, ambayo amesema anaamini itafunika ile mbaya na kumfanya aendelee kuwa kileleni.

H Baba, alitambulisha staili hiyo Ijumaa iliyopita katika Kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha EATV kila Ijumaa, ambapo aliitaja kwa jina la Poteza Dansi Bongo Fleva.

“Hapa watu watanikoma, maana haiigiki mzazi...ni mauno mwanzo mwisho, nani ataweza? Watu wasubiri kidogo waone ujio wangu mpya,” alisema H Baba.

Mbali na muziki, H Baba pia anacheza filamu na sasa yupo njiani kushusha mzigo mpya uitwao Promota, ambao umeongozwa na Director aliyejizolea heshima tele kwenye field hiyo anayekwenda kwa jina la Jully taxi.
*************************************
Twanga kugonga zote kali Idd Mosi na Pili
Bendi ya muziki wa Dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ a.k.a Vijana wa Kizazi Kipya, wataporomosha burudani ya kufa mtu ndani ya Ukumbi wa Mango Garden katika kusherehekea Sikukuu ya Idd Mosi na Pili.

Akistorisha na safu hii Meneja wa Bendi hiyo, Abuu Semhando ‘Baba Diana’ alisema kuwa siku hiyo mchana kuanzia majira ya saa 8 kutakuwa na pati ya watoto ambao watapata fursa ya kuburudika kwa kiingilio cha shilingi 1,000 tu na usiku ni zamu ya wakubwa kwa kiingilio cha shilingi 8,000.

“Itakuwa ni shoo ya aina yake ambayo kila mpenda burudani hastahili kuikosa. Siku hiyo tutatambulisha staili zetu mpya pamoja na nyimbo zetu kali ambazo tunaamini zitakonga nyoyo za mashabiki wetu,” alisema Baba Diana.

compiled by mc george/wikienda


Sunday, September 5, 2010

HAPPY NA LIVINGSTONE WAMEOANA!

SIKU LIVINGSTONE NA HAPPY WALIPOOANA PALE TAMAL HOTEL ILIKUWA NI HOI HOI NA VIFIJO...CHEKI HAPA: http://harusini.blogspot.com/