Monday, September 6, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Marichuy Kajiachia na midume hawa
Kutoka ndani ya tamthiliya maarufu ya Cuicado el An Angel inayofahamika zaidi kama Marichuy inayoendelea hivi sasa kunako Kituo cha Telivisheni cha CAPITAL, Ebwana Dah ilidondoshewa maombi kibao na wasomaji wakitaka kufahamu staa wake wa kike, Maite Perroni a.k.a Marichuy amewahi kutoka na wanaume wangapi.


Sisi kama wadau namba moja wa burudani, leo tunashuka na mwanadada huyo mrembo bila kusahau idadi ya wanaume aliyowahi kuangusha nao gari on bed. Wa kwanza kabisa kufungua pazi na Maite ni Guido Laris, ambaye alijikabidhi kwa mrembo huyo wa Mexico kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2005 hadi 2008.


Baada ya hapo kijiti kikachukuliwa na William Levy a.k.a Juan Miguel aliyedumu naye kwa miezi kadhaa kabla ya mwaka 2009 Eugenio Siller kuchukua usukani, ingawa naye kama ilivyokuwa kwa William, alikaa naye kwa miezi michache na kuachia ngazi.
Carlos De la mota ndiye anayemmiliki mlimbwende huyo mpaka sasa, tangu alipomtwaa mwaka jana kutoka kwa Eugenio Siller. Ni hayo tu wakubwa!!!
**************************************
Kabago Kumrudisha Farida kideoni
Kutoka pande za Rock City (Mwanza) aliyekuwa memba wa Kundi la BWV, Philibert Kabago amesema na Abby Cool & MC George over the weekend kwamba, siku kadhaa zijazo anatarajia kumrudisha mwanadada aliyepotea kwenye game kitambo, Farida.

Akipiga stori na safu hii juzi kati, kwa njia ya simu Kabago alisema kwamba atarudi na binti huyo kupitia video ya ngoma yake, Wivu ambayo ilitoka miezi kadhaa iliyopita ikimshirikisha msanii huyo ambaye hivi sasa ni mama wa mtoto mmoja.

“Tayari video hiyo imeshakamilika, siku chache zijazo nitaiachia hewani ili kuipa sapoti albamu yangu mpya ambayo pia iko tayari. Vilevile kwa upande wa audio nimetoa ngoma mpya yenye jina la Wameshikika ambayo ilifanyika pande za Uganda, kitakachofuata bada ya hapo ni jiwe juu ya jiwe kwa sababu sitaki kuwaangusha mashabiki wangu kwa kukaa kimya muda mrefu bila kuwadondoshea kazi mpya,” alisema Kabago.
*******************************************
Kwenye dansi kuna wakongwe, vipi Bongo Fleva?
Imekuwa kawaida kwa wanamuziki wakongwe wa Muziki wa Dansi kutambulishwa kwa title zao, lakini hali ni tofauti sana kwa wakongwe katika game ya Bongo Fleva, Abby Cool & MC George over the weekend wanakuwekea mambo sawa.

Ni rahisi sana kusikia Maalim Ngurumo, King Kikii, Shaban Dede, Hamza Kalala, Hassan Rehani Bichuka na wakali wengine wa muziki wa dansi, wakiitwa kwa sifa zao za ukongwe, lakini tumesahau kwamba, hata kwenye Bongo Fleva tuna wakongwe!

Ni heshima na fahari kubwa kuwaenzi wakongwe wa Bongo Fleva. Wasanii kama Solo Thang, Profesa Jay, Afande Sele, Mabaga Flesh, Uswahili Matola, Juma Nature, Balozi, Mchizi Mox, Mr. II ‘Sugu’, Dudubaya na wengineo, wanatakiwa kupewa heshima yao kama wakongwe.

Kiukweli haipendezi tukiwaita wanamuziki wa Bongo Fleva wakati wao ni miongoni mwa waasisi wa muziki huo, inakuwa tamu hata kuandika; “Mkongwe katika game ya Bongo Fleva Soggy Dog...” kuliko kuandika bila kumpa title yake.

Haiwezekani utambulisho wa msanii kama Diamond aliyetoka juzi kati, uwe sawa na wakongwe kama Mr. Paul, Mez B, Caz T, Mike T na wengine wakali walioanza game kitambo.

Meseji hii iende moja kwa moja kwa watangazaji wa redio na runinga, waandishi wa habari na wadau wote wa muziki wa kizazi kipya. Tuwape heshima zao wakongwe pale inapotakiwa kufanya hivyo.
*******************************************
K-Sher aibuka na mapya kuhusu kusimamishawa Tip Top
Mtiti ndani ya Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam, bado unaendelea na stori kubwa ni juu ya First Lady wa Kundi hilo, Khadija Shaban a.k.a K – Sher amejitoa au amefukuzwa na hapa Keisha ameibuka na kumwaga mapya manne.

Akigonga interview na Abby Cool & Mc George Over The Week end, juzi kati kwa njia ya simu, K – Sher amesema Kiongozi wa Kundi hilo Babu Tale anatakiwa aongee ukweli, kwani anaficha-ficha mambo, lakini alifafanua mambo muhimu manne.

“Kwanza siwezi kufukuzwa Tip Top kwa sababu uwezo wangu unajulikana, ukweli ni kwamba nikitoka, basi kundi litayumba sana, coz nina mchango mkubwa kimuziki. Mimi nimejitoa mwenyewe na sababu kubwa ni kwamba sina imani na uongozi.

“Babu Tale asiongee uongo na kama wanahitaji nirudi, sharti la kwanza kabla ya mazungumzo mengine, Babu Tale anilipe pesa zangu 480,000 ambazo ni madeni ya pesa alizokuwa akinisainia baada ya shoo na kuniletea pungufu, mwisho siwizekulumbana nao kwa sababu nina mambo mengi ya kufanya kwa ajili ya kuongeza uchumi wa taifa letu,” alisema K- Sher.

Kwa upande wake Babu Tale alikuwa na haya ya kusema: “Kaka nina mambo mengi sana ya kufanya, nipo ‘bize’ na maandalizi ya uzinduzi wa albamu mpya ya Tip Top, utakaofanyika Idi Mosi, kwahiyo muda wa kulumbana sina kabisa.”
*******************
MKALI wa miondoko ya TAKEU Bongo, Hamisi Baba a.k.a H- Baba, ameibuka na kutambulisha staili mpya ya muziki, ambayo amesema anaamini itafunika ile mbaya na kumfanya aendelee kuwa kileleni.

H Baba, alitambulisha staili hiyo Ijumaa iliyopita katika Kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha EATV kila Ijumaa, ambapo aliitaja kwa jina la Poteza Dansi Bongo Fleva.

“Hapa watu watanikoma, maana haiigiki mzazi...ni mauno mwanzo mwisho, nani ataweza? Watu wasubiri kidogo waone ujio wangu mpya,” alisema H Baba.

Mbali na muziki, H Baba pia anacheza filamu na sasa yupo njiani kushusha mzigo mpya uitwao Promota, ambao umeongozwa na Director aliyejizolea heshima tele kwenye field hiyo anayekwenda kwa jina la Jully taxi.
*************************************
Twanga kugonga zote kali Idd Mosi na Pili
Bendi ya muziki wa Dansi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ a.k.a Vijana wa Kizazi Kipya, wataporomosha burudani ya kufa mtu ndani ya Ukumbi wa Mango Garden katika kusherehekea Sikukuu ya Idd Mosi na Pili.

Akistorisha na safu hii Meneja wa Bendi hiyo, Abuu Semhando ‘Baba Diana’ alisema kuwa siku hiyo mchana kuanzia majira ya saa 8 kutakuwa na pati ya watoto ambao watapata fursa ya kuburudika kwa kiingilio cha shilingi 1,000 tu na usiku ni zamu ya wakubwa kwa kiingilio cha shilingi 8,000.

“Itakuwa ni shoo ya aina yake ambayo kila mpenda burudani hastahili kuikosa. Siku hiyo tutatambulisha staili zetu mpya pamoja na nyimbo zetu kali ambazo tunaamini zitakonga nyoyo za mashabiki wetu,” alisema Baba Diana.

compiled by mc george/wikienda


No comments: