Thursday, April 14, 2011

CHAMA CHA WAPISHI KIMATAIFA BONGO CHAJA


Picha hii inamuonesha Chef Issa akiwa na Tunzo katika mashindano ya Junior chefs katika utengenezaji wa Chocolate ktk kitongoji cha Interlaken Switzerland na kuibuka mshindi wa tatu.

CHAMA CHA KITAALAMU CHA WAPISHI TANZANIA KUANZISHWA! Active chefs Association of Tanzania (acat 2011) BAADA YA MAFANIKIO MAKUBWA YA BLOG YA ACTIVECHEF SASA NIMEAMUA KUANZISHA CHAMA CHA KITAALAMU CHA WAPISHI TANZANIA.

CHAMA HIKI NI CHAMA KISICHO CHA KIBIASHARA.
NATOA WITO KWA NDUGU ZANGU WATANZANIA WAPISHI WA HAPA NYUMBANI NA WALIOKO NJE YA NCHI TUUNGANE NA TUJENGE CHAMA CHENYE NGUVU TUWEZE TAMBULIKA KATIKA ULIMWENGU WA MAPISHI DUNIANI.

KWASASA TAYARI WAMESHAPATIKANA WANACHAMA KUMI WATANZANIA TOKA SAUDI ARABIA, AMERICA, SWISS NA UK. NAWAKARIBISHA WOTE MJIUNGE NI BURE HAKUNA ADA YEYOTE. FOMU ZA KUJIUNGA TUMA EMAIL issakesu@gmail.com KISHA NITAKUATUMIA HARAKA NAWE UNAJAZ ANA KUSCAN KISHA UNANITUMIA.

KUANZIA MWEZI UJAO TUTAKUA NA WEBSITE YA CHAMA NA EMAIL YA CHAMA IPO KATIKA MATENGENEZO.
NAWAOMBA SANA NDUGU ZANGU WATANZANIA MUITIKIE WITO ILI TUWEZE KUFAIDI MATUNDA YA TAALUMA HII PIA TUWEZE ANDIKA HISTORIA DUNIANI.

MALENGO BAADA YA KUANZISHA CHAMA KWA MAFANIKIO YA MIAKA 2 KISHA TUTAJIUNGA NA CHAMA CHA WAPISHI DUNIANI ( wacs) World Association of Chefs Societies. KWA KUJIUNGA KATIKA CHAMA HIKI TUTAWEZA PATA WASAHA WA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAPISHI DUNIANI, KUSHIRIKI MAFUNZO NA MIKUTANO PAMOJA NA WAPISHI WALIOBOBEA DUNIANI NA MWISHO NI KUTAMBULIKA KOTE DUNIANI.


PIA TUNATEGEMEA KUJIUNGA NA CHAMA CHA World Master Chefs Society HAPA WAPISHI WENYE NGAZI ZA EXECUTIVE WATAPANDA DARAJA NA KUA MASTER CHEF BAADA YA KUA WANACHAMA NA KUPATA MAFUNZO MAALUM.
VYAMA VYOTE HIVI VIKUBWA DUNIANI HUWEZI JIUNGA MPAKA UWE UMEJIUNGA KATIKA CHAMA NDANI YA NCHI YAKO HAWAKUBALI KUSAJILI MTU BINAFSI.

KWASASA WANACHAMA WA VYAMA VYOTE HIVI NI NCHI 5 TU KWA AFRICA !! South Africa, Namibia, Egypt, Mauritius na Ghana. TUNAWEZA KABISA KUANDIKA HISTORIA YA MAFANIKIO IKIWA TUTAUNGANA NA KUA KITU KIMPOJA.


CHAMA CHETU KIKIWA THABITI TUTAWEZA KUTETEA HAKI YA MPISHI NA KURUDHISHA HADHI NA HESHIMA YA TAALUMA HII ADIMU NA ADHIMU DUNIANI.
UNAWEZA TEMBELEA SITE HIZI ZA VYAMA HIVI VIKUBWA DUNIANI www.worldmasterchefs.com/ NA http://www.wacs2000.org/ MWEZI WA 5 KUANZIA TAR 1 NITAKUA DAR ES SALAAM KISHA NITAKWENDA ARUSHA NAIMANI UTAKUA WASAHA MAALUMU KUWEZA KUKUTANA NA WAPISHI WENZANGU TUKAZUNGUMZA KWA UNDANI ZAIDI NA NIKAWEZA JIBU MASWALI YENU KUMBUKENI HAKUNA MAFANIKIO BILA JUHUDI, MIPANGO NA MAARIFA. PIA UMOJA NI NGUVU.

KILA MTU ANAWEZA AKIPEWA NAFASI NA WASAHA. SASA NI ZAMU YA WAPISHI WA KITANZANIA KUFAHAMIKA DUNIANI NA KUJIWEKEA HESHIMA NA MAISHA BORA. KARIBUNI SANA SANA FOMU NI BURE.

CHEF ISSA

http://activechef.blogspot.com/

No comments: