Tuesday, June 21, 2011

BAUCHA RECORDS YASAKA WENYE VIPAJI

Studio ya Baucha Records inasaka vijana wenye vipaji kwa ajili ya kuigiza filamu na tamthiliya mbalimbali, Edna Titus anaripoti.
Prodyuza wa studio hiyo, Ally Baucha aliiambia safu hii kuwa, hii ni nafasi ya pekee kwa wale wenye vipaji.
“Ni program maalum ya kusaka wale wenye vipaji ambao tutawatumia katika filamu na tamthiliya mbalimbali tutakazondaa, kwa mawasiliano zaidi, mtu anayehitaji nafasi hiyo atupigie kupitia simu namba 0715 994 995, 0767 994 995,” alisema Baucha.

No comments: