Tuesday, June 21, 2011

ANZ-UK YAKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA ZA KITANZANIA UK

 wajumbe kutoka ZAWA wakisiliza hoja
SALAM,
Jumuiya ya WaTanzania–UK chini ya Mwenyekiti wake Dr John Lusingu, ilikutana na Viongozi mbali mabali wa Jumuiya  vyama, na Taasisi za KiTanzania katika juhudi ya kutathmini Mkutano wa Diaspora III, na kuweka mikakati ya utekelezaji ya mipango mingine ya Kimaendeleo .

Mwenyekiti wa Tanz-Uk alisisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuunganisha nguvu katika kupanga , kufuatilia na kutekeleza mipango mbali mbali kwa ajili ya WaTanzania walioko UK , pamoja na mikakati ya kushiriki katika maendeleo Tanzania.  “Nguvu za pamoja ni resource imara katika kukabiliana na changamoto ya aina yoyote. Tunatumikia WaTanzania na Taifa moja, tukishirikiana kimawazo na kimkakati, tunahakika ya kufanikisha mambo mengi kwa haraka” alisistiza mwenyekiti Dr John Lusingu.

Viongozi wengi walioitikia mwaliko wa Tanz-UK walioshiriki katika mashauriano hayo, waliipokea hoja hiyo na kuonyesha kufurahishwa na mkakati wa “nguvu ya pamoja”, na kushauri kuwa kuwe na majadiliano zaidi kuufanya mpango huo uwe madhubuti zaidi.
Mkutano huu ulifanyika Jumamosi tarehe 18.02.11 katika ofisi zetu za Ubalozi jijini London
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE
Afisa wa Ubalozi ambaye pia ni mhasibu wa Ubalozi David akichangia hoja wakati wa mkutano
 Frank Kutoka Urban Pulse akiwa mzigoni
 kushoto Bwana Hussein kutoka tawi la TA Reading, Susan katibu mkuu wa CCM Uk na Allan kalinga Mipango, Uchumi na Fedha CCM Uk wakifuatilia agenda ya mkutano
 Mjumbe wa Tanz Uk tawi la London Jestina akitoa hoja
 Mr Otieno (katikati) akiteta jambo na wajumbe wa TA Magabe (kushoto) na Evans (kulia)
 Mwenyekiti wa kikao Afisa wa Ubalozi Amosi Msanjila akitoa mwongozo kulia Mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu na kushoto Said Sururu Kutoka Tawi la Tanz Uk London
 Mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu akitoa mada JPG
 Picha ya pamoja baad ya mkutano

No comments: