Nasikitika kuwafahamisha kuwa baba mzazi Mzee Philemon  Chahali amepata ajali mbaya asubuhi hii huko Ifakara.Amegongwa na  pikipiki ambazo ndio usafiri mkuu wa huko.Kwa mujibu wa habari  nilizonazo hadi muda huu,hali yake ni mbaya,ambapo licha ya kuvunjika  mguu pia ameumia kichwani.Kibaya zaidi ni kwamba umri wake ni kwenye  miaka ya 80 kwa hiyo mshtuko tu wa ajli unaweza kumwathiri sana.
Basi  naomba kutumia fursa hii kuomba sala zenu.Sie Wakristo tunaamini kuwa  wanapojumuka wengi kufanya sala basi Mungu naye anakuwepo.Natumaini kwa  sala zenu na za familia yetu Mungu atamjalia baba apone na kurejea  katika hali yake ya kawaida.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.Asanteni
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment