Mhe. Rais JK akimkabidhi zawadi na cheti maalum Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dr. John Magufuli
Dr. Dau (kati) akiwa na wageni wengine
Dr. Dau (kulia) akionesha cheti chake
Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja
Na Alfred Ngotezi
Rais Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu uliojumlisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi alitoa zawadi hiyo kwa niaba ya Bodi ya Wakondrasi.
Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza tarehe 5 na utakwisha tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe walitoka Afrika Kusini, Zambia, Kenya na Malawi.
Akiongea kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam, Rais aliwapongeza Wahandisi, Wabunifu Majengo, Wakadiriaji na Makondrasi walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge pamoja ili waweze kupata uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
Katika siku za karibuni NSSF imekuwa na miradi mikubwa ya ujenzi. Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, nyumba za Polisi Dar es Salaam na Zanzibar na nyumba za Jeshi huko Monduli Arusha. Hivi karibuni NSSF itaanza kujenga Daraja la Kigamboni.

No comments:
Post a Comment