Saturday, October 1, 2011

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAZINDUA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU.

  
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda akitoa hotuba ya kuzindua rasmi wiki ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea vipaumbele vitakavyozingatiwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kuwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii,  Kuimarisha huduma za Afya ya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka 5 ikiwa ni pamoja na kuimarisha udhibiti wa magonjwa yanayoammbikiza na yasiyoambukiza pamoja na yale yaliyosahaulika.Pia ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupima Bure Afya zao na kipindi chote cha wiki ya maadhimisho hayo itakayomalizika tarehe 2, Oktoba, 2011.

 Pichani juu na chini; Baadhi ya Wakurugenzi, Viongozi wa Wizara na Serikali, Wadau wa Sekta ya Afya na Watoa huduma za Afya.
 Mwanamuziki Mkongwe nchini Kassim Mapili (katikati) akiwa na wanamuziki wenzake wa bendi ya Mjomba wakitoa burudani katika sherehe za maadhimisho hayo.

 Mgeni rasmi Mh Dkt. Mponda akisakata Rhumba baada ya kukunwa na muziki uliokuwa ukiporomoshwa na Mzee Kassim Mapili.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akizungumza  na  baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria sherehe hizo

No comments: