Sunday, November 6, 2011

VODACOM TANGA CYCLE CHALLENGE 2011

Baadhi ya washiriki wa mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilometa 140 wakichuana vikali hapo jana.
Mshindi wa  kwanza  wa Kilomita 140 wa mbio za  baiskeli za “Vodacom Tanga cycle Challenge “  Hassan Sharif akimaliza mbio hizo kwa kwa kutumia masaa 4.13.07 .ambapo mbio hizo zilianzia katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga  hadi Hale na kurudi katika uwanja huo  hapo jana.    
waandaaji wa Mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge Sophy Wakati akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  kushoto kabla ya mbio hizo kuanza,wa pili kutoka kushoto Buruhani Yakub ambae ni  Mwandishi wa Habari wa Mwananchi Communication na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Washiriki mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa walemavu wakimaliza mbio hizo hapo jana mjini Tanga. 
Washindi wa kwanza na wapili wa mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa kilometa 80 wakimaliza mbio hizo,ambapo Kudushi Nkandi  kushoto aliibuka mshindi na Mohamed Bundala akawa mshindi wa pili.
 Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu ,afya na uchumi,  Seleboss Mustafa, (kushoto)akimkabidhi  shilingi 75,000.mshindi wa  tatu wa mbio za Vodacom Tanga cycle  Challenge kwa upande wa Kilomita 140 Revocatus Sebastian, aliyetumia  Masaa 4: 15.52 mashindano hayo yaliyoanzia katika uwanja wa Mkwakwani  mjini Tanga  hadi Hale na kurudi katika uwanja huo ,wanaoshuhudia wapili kutoka kushoto ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude,Michael Kasun ambae ni msimamizi wa mawakala wa Vodacom kanda ya Kaskazini.
HASSAN Shariff ametwaa ubingwa wa mashindano ya Mbio za baiskeli ya
(Vodacom Tanga Cycle Challenge 2011)baada ya kumaliza mwendo wa umbali
wa kilomita 140 akiwa mbele ya washiriki wengine.
 
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Wakati Sports Promoter
na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania  yalishirikisha makundi matatu ambayo ni ya
baiskeli zilizotengenezwa maalumu kwa michuano ambapo washiriki
walipita Wilaya za Muheza na Korogwe na kurejea Tanga mjini umbali wa
kilomita 140.
 
Sharrif alitwaa ubingwa huo akiwa katika kundi la baiskeli maalumu za
mbio hizo ambapo alimaliza michuano hiyo akiwa amekimbia kwa saa 4.13.07 na
kufuatiwa na Juma Kashinde aliyetumia muda wa saa 4.14.52 wakati
mshindi wa tatu alikuwa Revecatus Sebastian aliyemaliza akiwa
amekimbia kwa saa 4.15.30.
 
Nafasi ya nne ilikwenda kwa Hamis Milikioni aliyekimbia kwa saa
4.28.08, Mathew Alberto alimaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.35.06 huku
Athumani Muya akikimbia kwa saa 4.38.07.
 
Kundi la baiskeli za kawaida lilianzia Tanga mjini kupitia Tanganyika Wilaya
ya Muheza umbali wa kilomita 80 ambapo Kadushi Nkandi aliongoza kwa
kutumia muda wa saa 1.56.00,Issa Kashinde alishika nafasi ya pili kwa
kumaliza akiwa ametumia muda wa saa 1.57.12 huku Mohamed Bundala
alitumia saa 2.15.13.
 
Baiskeli za miguu mitatu zilikuwa za kulizunguka jiji la Tanga
ambapo aliyeongoza ni Jackson Kinyusa aliyekimbia kwa dakika 30.20
akifuatiwa na Mohamed Balozi dakika 32.16 huku Medrin Sabuni akishika
ushindi wa tatu kwa kukimbia kwa dakika 45.02.
 
Mgeni rasmi ,Mohamed Mustapher ambaye pia ni diwani wa Kata ya
Nguvumali na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya
Tanga,aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuukumbuka mchezo wa baiskeli
na kuwaomba kuboresha zaidi mwakani kwani Tanga ni mkoa wenye vipaji
vingi.
 
Mgeni huyo ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Tanga alimkabidhi
Shariff kiasi cha sh 150,000, Kashinde sh 100,000,Revocatus sh 75,000
wakati washindi wa kwanza katika makundi ya baiskeli za miguu mitatu
na za kawaida walizawadiwa sh 100.000,wa pili sh 75,000 wa tatu sh
50,000 huku washiriki wengine wakipewa kifuta jasho cha sh. 10,000 kwa
kila mmoja.
 
Afisa Udhamini wa Vodacom,Ibrahim Kaunde alisema huu ni mwaka wa pili
kwa Kampuni yake kudhamini mashindano ya baiskeli kwa Mkoa wa Tanga
na Mwanza lengo likiwa ni kuimarisha mchezo huo katika maeneo hayo kwa
kuwa unaonekana kupendwa zaidi.
 
“Kimsingi Vodacom imejikita kudhamini michuano ya baiskeli Tanga na
Mwanza kutokana na ari na mwamko uliopo kama ambavyo tunavyodhamini
riadha mkoani Kilimanjaro”alisema Kaunde.

No comments: