Vodacom yawezesha upatikanaji taarifa
za mahusiano kupitia simu za mkononi
Dar es
salaam, Desemba 1, 2011 Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania imezindua huduma ya
Young Africa Live itakayowawezesha wateja wake kupata taarifa sahihi za afya,
mahusiano na ngono kuanzia Desemba Mosi mwaka huu.
Kupitia huduma hiyo ya kwanza nchini
wateja wa Vodacom watapata fursa ya kuunganishwa moja kwa moja na wadau wa masuala
ya afya na mahusiano ya jinsia ikiwa ni pamoja na kujibiwa maswali watakayokuwa
wakiuliza kupitia simu zao mkononi.
Young Africa Live ni huduma
inayowaunganisha wanajamii kihabari kupitia simu za mkononi na kutoa burudani
na fursa ya mazungumzo na kubadilishana taarifa
na uzoefu katika mada za mapenzi, ngono, mahusiano, jinsia na afya ya
uzazi
“Tunaimani kwamba huduma hii
itasaidia jamii hususan vijana ambapo kupitia taarifa za kiafya wataweza kuwa
na mahusiano yenye tija na kujikinga na maambuzkizi ya virusi vya Ukimwi na
Ukimwi”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza
“Kila juhudi ni muhimu katika vita ya
kupunguza athari za virusi vya Ukimwi na Ukimwi, matatizo ya afya ya uzazi
katika jamii ikiwemo vifo. Taarifa sahihi ni nyenzo muhimu katika mapambano
haya, hivyo huduma hii ni wazi itapunguza pengo la ukosaji wa habari muhimu za afya
kwa wanajamii.”Ameongeza Rene.
Ili mteja wa Vodacom aweze kunufaika
na huduma hii ya kwanza nchini kutoka Vodacom anapaswa kuwa na huduma ya
Intaneti kwenye simu yake na kupitia Portal ya
Young Africa Live ataunganishwa na wanajamii wengine na wadau wa afya
kwa urahisi.
Gharama
ndogo itatozwa kwa wateja wa Vodacom wa malipo ya kabla.
“Tunategemea
vijana wengi kutumia fursa hii kujifunza, kubadilishana mawazo na uzoefu juu ya
masuala ya afya na mahusiano na hatimae kuwa chachu ya mabadiliko ya tabia.”Alisema
Rene
Huduma ya
Young Africa Live imefanya vizuri nchini Afrika Kusini na kuwa tegemeo la chanzo
cha habari kwa vijana ambao kupitia mazungumzo ya pamoja yamesaidia kubadili
mitazamo ya vijana katika mapenzi, ngono na masuala ya afya ya uzazi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment