Ally Tall ‘AT’ akiwa amekaa chini baada ya raha kumkolea wakati wa makamuzi.
...Akikamua na mmoja wa wanenguaji wake.
Msanii anayetamba na ‘Hakunaga’, Ismaili Thabit ‘Suma Lee’, akiwajibika.
...Suma Lee akiserebuka na mkali wa miondoko ya kwaito.
Mkurugenzi wa kundi la Mashauzi Classic Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, akiwajibika.
...Akijinafasi jukwaani.
Extra Bongo chini ya Ally Choki (wa pili kushoto), wakiwajibika.
Wanenguaji wa Extra Bongo wakifanya kazi jukwaani.
Nyota wa bendi ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ akikamua na wanenguaji wake.
Wasanii wa kundi la Sliders wakionyesha uwezo wao.
Baadhi ya watoto walioingia ukumbini wakicheza na sungura-mtu.
Wakali Dancers wakipagawawisha.
Ali Choki (kulia), akiteta jambo na Chaz Baba.
Ofisa
Utawala wa Global Publishers Ltd, Soud Kivea (wa pili kulia),
akikabidhi jezi na mpira vyenye thamani ya sh. 380,000 kutoka Dar Live
kwa meneja wa timu ya Vita FC ya Mbagala Zakhem, Ernest Nyanda (wa
kwanza kushoto), akishuhudiwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo na
viongozi wa Dar Live.
Mmoja wa watoto waliofika ukumbini hapo akiwa kwenye pozi baada ya kuchora usoni kwake.
Watoto wakicheza na Bodaboda zilizomo ukumbini hapo.
…..Wakichorwa mapambo usoni.
…..Wakilishwa keki na kipande cha nyama wakati wa kutoka ukumbini humu ikiwa ishara ya upendo wa uongozi wa ukumbi huo.
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia shoo zilizokuwa ukumbi hapo.
Umati uliyofurika ukumbini hapo.
WASANII
wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Ismaili Thabit ‘Suma Lee’, Ally Tall
‘AT’, Mashauzi Classic, Extra Bongo ‘Next Level, na Bendi ya Mashujaa
usiku wa kuamkia leo walipata nafasi ya kufanya makamuzi ndani ya ukumbi
wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.Wasanii hao waliwapagawisha mashabiki wa pande hizo na wakausifia Dar Live wakisema kuwepo kwake kulikuwa mwanzo wa wao kufanya shoo za kimataifa huko Mbagala.
Miongoni mwa wasanii hao waliotumbuiza hapo kwa mara ya kwanza tangu ufunguliwe Januari Mosi mwaka huu, waliahidi kupiga shoo zaidi pindi wanapoalikwa.
Shoo hiyo pia ilisindikizwa na kundi la wanenguaji la Sliders kutoka Kinondoni jijini Dar na Wakali Dancers la Temeke ambao pia walifanya makamuzi ya kufa mtu na kusifia mandhari ya ukumbi huo.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.
No comments:
Post a Comment