Katibu wa Chama cha wanawake UK (TAWA UK) Mariam Mungula akiwaeleza waheshimiwa machahceh kuhusu chama hicho
Afisa wa Bunge Mrs Justina Shauri, Mhe. Esther Matiku, Mhe. Beatrice
Shelukindo na Mama Balozi Joyce Kallaghe wakiwa wanamsikiliza mhe.
Balozi akitoa ukaribisho
Mwenyekiti wa TAWA Uk Mariam Kilumanga, Afisa ubalozi mambo ya
utawala Mrs. Rose Kiondo na Deputy Chairman wa TANZUK Ma Nelly wakiwa
katika pich aya pamoja na Mhe.Al-Shaymaa J. Kwegyir
Picha ya pamoja na waheshimiwa baada ya chakula cha jioni
Wageni
hao 12 wakiwemo Wabunge 11 na Afisa wa Bunge 1 waliotokea nyumbani
Tanzania na kuja UK kwa Mualiko wa Commonwealth parliamentarians Group
(CPA) walikaribisha chakula cha jioni na Mama Joyce Kallaghe Mke wa
Balozi wa Uingereza akiwa na Viongozi wa Chama cha TA na TAWA nyumbani
kwake Tanzania hao
Wabunge
hao 11 wote wanawake na ambao miongoni mwao ni Viongozi wa wajumbe wa
Tanzania Women Parliamentarians Group (TWPG) ,waliongozwa na Mwenyekiti
wa TWPG Mheshimiwa Mama Anna Abdalla MP, na wakiwemo Mh.Susan Lyimo MP,
Mh. Magdalena h. Sakaya (MP) , Mh. Angela Kairuki (MP), Mh. Esther
matiko (MP, Mh. Beatrice Shelukindo (MP), Mh. Riziki Omari Juma (MP),
Mh. Namalek Sokoine (MP), Mh . Faharia Hamisi (MP) ,Mh. Al-Shaymaa J.
Kwegyir (MP), Mh. Agripina Z Buyogera (MP) na Afisa wa Bunge Mrs Justina
Shauri.
Wageni
walikaribishwa na Balozi Mheshimiwa Peter Kallaghe na Mama Balozi Joyce
Kallaghe , Mheshimiwa Balozi aliongea machache ya Ukaribisho na kumpa
nafasi Mh.Mama Anna Abdalla ambae alishukuru kwa mualiko huo na kuelezea
kuhusu Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG) ambao kila Mbunge Mwanamke wa
Bunge la Tanzania ni mwanachama wake na jinsi gani TWPG inavyofanya
kazi kwa pamoja bila ya kujali itikadi za vyama vya kisiasa vya
Waheshimiwa hao. Usiku huo iliweza dhihirika kwa jinsi waheshiwa hao
walivyokuja kujitambulisha kila mmoja alisimama na kujitambulisha na
walilotilia msingi katika utambulisho wao ni kamati zao tofauti za Bunge
ambazo wanahusika nazo na kuwa wnachama wa kikundi cha TWPG. Wageni
waliokuwa pale walishuhudia zaidi ya nusu ya hawa wabunge waliongia na
furaha bila ya kujali kuwa bado wana uchovu wa safari kutoka nyumbani
wakisahau kutaja vyama vyao vya kisiasa. Mheshimiwa Mama Anna Abdalla
alisisitiza kwamba ingawa vyama vya siasa ndio vilivyowapeleka wote
bungeni lakini wakishaingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano
,wanawake bungeni hawaangalii vyama vyao vya siasa bali huwa wakiwa
Bungeni kabla ya sera yeyote kupita Wanawake huwa wote kwa Umoja
wanaangalia hii itamnufaisha vipi Mwanamke na Mtoto wa Kitanzania.
Maneno
haya ya Mheshimiwa Mama Abdalla yalidhihirishwa na jinsi Waheshiwa wote
walipokaa katika meza moja na kuongea na kucheka kwa pamoja na kwa
furaha huku wakila chakula kitamu cha jioni bila ya kujali pale kwenye
ile meza kuna CCM, NCCR, CUF wala CHADEMA. Kitendo hiki kiliwavutia sana
viongozi wa wanawake London ambao walikuwepo katika shuguli hii Bi.
Nelly Msemwa (TA Taifa Deputy chair anaeshughulikia mambo ya wanwake
),Bi. Mariam Kilumanga(TAWA Chair ), BI Mariam Mungula (TAWA Secretary)
, Bi Rose Kiondo (Afisa Ubalozi) na Bi Jestina George (TA London na
Blogger), kiasi ambacho walipopewa nafasi ya kuongeza machache walimpa
nafasi hii Bi Mariam Mungula ambae aliwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge
wa kitendo hicho na somo walilompa la kuwa hata Wakiwa Bungeni yeye
akifikiri hakuna mashirikiano kati ya vyama tofauti kumbe sivyo kabisa
wakiwa ndani na nje ya Bunge wanaweka wote ni kitu kimoja. BI Mariam
Mungula vilevile alielezea kaazi za kikundi wa kina mama cha hapa UK
ambacho yeye ni mmjoa wa viongozi wake Tanzania Women Association
(TAWA) na kumalizia kwa kuwaomba waheshimiwa wabunge kupitia TWPG
wasihau kuwa kuna wanawake wengine wa kitanzania hata kama ni nje ya
nchi na ambao wako tayari kushirikiana nao kwa lolote katika
kumuendeleza MWanamke wa KItanzania.
Kikundi
hichi cha Waheshimwa kimekuja Uingereza kwa Mualiko wa CPA kwa siku
chache katika majukumu yao ya kila siku ya kumpingania Mtanzania.
Mungu Ibariki Tanzania.
Picha na Habari Jestina George
No comments:
Post a Comment