Dar es salaam, Disemba, 20, 2012.
Kuzinduliwa
kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-PESA kuweka na
kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali
popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la
benki ya CRDB..
Huduma hii ya ushirikiano kati ya
Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-PESA ni ya kwanza
nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-PESA wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la
Benki.
“Tunapoitambulisha huduma hii mpya
inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na
huduma ya Vodacom M-PESA.Mteja wa M-PESA kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka
akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya
kujivunia kuwa mteja wa Vodacom”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene
Meza.
Huduma ya Vodacom M-PESA ya kwanza
sokoni kutoka Vodacom mtandando unaoongoza nchini ni kielelezo makini cha
ubunifu na namna ambavyo Vodacom imedhamiria kubadili maisha ya watu kupitia
teknolojia ya simu za mkononi.
Ikiwa na mawakala zaidi 20,000 nchi
nzima M-PESA inabakia kuwa huduma salama zaidi, ya haraka, uhakika na yenye
kuaminika kwa ajli ya kuweka na kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma na
manunuzi mbalimbali, kulipia kodi, kuchangia pensheni pamoja na kupokea fedha
kutoka nchi zaidi ya sabini na tano ulimwenguni.
“Hakuna mteja wa Vodacom M-pesa
atakaesimama kwenye foleni au kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata tawi la
benki yake ya CRDB, sasa wataweka na kutoa fedha wakati wowte na mahali popote
bila kuathiri shughuli nyengine za kijamii na kimaendeleo ni wazi maisha
yamekuwa rahisi zaidi.”Aliongeza Bw. Rene
Tangu ilipoanzishwa mwaka 2007,
huduma ya Vodacom M-PESA imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa
huduma yenye usalam zaidi, yenye mtandao mpana wa mawakala mijini na vijijini
na hivyo kuchangia maendeleo ya jamii na biashara nchini kwa kuinua vipato vya
wananachi kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.
Kuweka fedha katika akaunti ya CRDB
kutoka akaunti ya M-PESA,hatua ni kama ifuatavyo
I.
Piga
*150#
II.
Chagua
kulipia bili
III.
Ingiza namabri ya biashara
ambayo ni 900500
IV.
Ingiza nambari ya
kumbukumbu ambayo ni namabri ya akaunti ya benki.
V.
Weka kiasi cha fedha mteja
anachotaka kutoa katika akaunti ya M-PESA kwenda akaunti ya benki
VI.
Ingiza
nambari ya siri.
VII.
Bonyeza
1 kuthibitisha au 2 kubatilisha muamala.
Baada ya hatua hizi mteja atapokea
mara moja ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA kuthibitisha muamala na
baada ya dakika 8 atapokea ujumbe kutoka benki ya CRDB.
Kuhamisha
fedha kutoka akaunti ya Benki ya CRDB kwenda M-PESA hatua ni kama ifuatavyo
I.
Piga
*150*03#
II.
Ingzia
nambari ya siri
III.
Chagua
nambari 3 (Hamisha fedha)
IV.
Chagua
nambari 3 (M-PESA)
V.
Chagua nambari ya akaunti yako ya Benki
VI.
Thibitisha
nambari yako ya simu
VII.
Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuhamisha
VIII.
Thibitisha au batilisha. Na baada ya hapo utapokea
ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA na pia Benki ya CRDB unaothibitisha zoezi hili.
Ili kuwa na
uwezo wa kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda M-PESA ni LAZIMA kwanza mteja wa M-PESA ajisajili CRDB.
Usajili huo
hufanyika MARA MOJA TU na kwamba
unaweza kufanyika kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*03# na maelezo ya
namna ya kujisajili yatatotekea ambayo mteja atapaswa kuyafuata.
No comments:
Post a Comment