Rais
wa Shindano la Miss Utalii, Gideon Chipungahelo (Katikati) akiongea na wadau wa
Sanaa kuhusu miaka mitano ya shindano hilo kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika
kila wiki makao makuu ya BASATA. Kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa
Miss Utalii Aboubakar Omar na Mkuu wa Kitengo cha Matukio wa BASATA, Omary
Mayanga,
Mkurugenzi
wa Mipango na Maendeleo wa Miss Utalii, Vikas Gupta akielezea mipango mipya ya
shindano la miss utalii kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.Kulia kwake ni Bw.
Aboubakar na Chipungahelo.
Mkurugenzi
wa Matukio, BASATA, Omary Mayanga akitoa ufafanyzu wa masuala mbalimbali
yaliyojitokeza kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii.
Mzee
Mwali Ibrahim ambaye ni mwandishi wa habari za uchumi na utalii wa Business
Times akieleza umuhimu wa shindano la Miss Utalii
Wadau
wa Sanaa wakifuatilia majadiliano kuhusu miaka mitano ya shindano la Miss
Utalii.
Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
limepongezwa na wadau wa Sanaa kwa juhudi zake katika kusimamia na kuratibu
matukio mbalimbali ya Sanaa hapa nchini na kuyafanya kudumu.
Pongezi hizo zimetolewa wiki hii
na wadau wa Sanaa wakati wakichangia mjadala uliohusu miaka mitano ya shindano
la miss utalii na sanaa ya urembo nchini kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika
kwenye Ukumbi wa BASATA uliopo Ilala, Sharif Shamba.
Akizungumza wakati akieleza
historia za shindano hilo, Rais wa Miss Utalii, Gideon Chipungahelo alisema
kuwa, BASATA imekuwa bega kwa bega na shindano hilo katika kuhakikisha miongozo
na kanuni mbalimbali za kuendesha mashindano zinafuatwa na kusisitiza kuwa,
hiyo ndiyo sababu ya shindano hilo kuweza kupata baadhi ya mafanikio ya ndani
na nje ya nchi.
“Naishukuru Serikali na BASATA,
kila mara wamekuwa wakitoa maelekezo na miongozo ambayo imelifanya shindano
hili kufikia mafanikio haya ingawa kumekuwa na changamoto kadhaa hasa za kukosa
wadhamini” alisistiza Chipungahelo.
Aliongeza kuwa, BASATA imekuwa mara
kwa mara ikikutana na kamati ya miss utalii na kuipa maelekezo mbalimbali ikiwa
ni pamoja na kufanya tathimini na wadau wa sanaa ya urembo ambao wamekuwa
wakitoa michango ya kuliboresha shindano hilo.
Awali wadau wa Jukwaa la Sanaa
walipata wasanii wa kutoa maoni na ushauri kuhusu shindano la miss utalii
ambapo walitoa changamoto kadhaa na kushauri jinsi ya kuzitatua na kulifanya
shindano hilo lizidi kusonga mbele.
“Shindano hili ni zuri na ni
kiungo kizuri cha kukuza utalii kama waandaaji watalisimamia vizuri, ni vema
kuwa na kamati maalum ya uendeshaji
inayowajibika na wadhamini waone umuhimu wa kulifadhili shindano hili”
alishauri Mzee Mwali Ibrahim ambaye ni mwandishi wa habari za uchumi wa gazeti
la Majira.
Aliishauri kamati ya miss utalii
kuliunganisha shindano hilo na maendeleo ya sekta ya sanaa nchini.
No comments:
Post a Comment