Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk Alberic Kacou
(kushoto), leo akihutubia Jukwaa la Wahariri aliwashakuru wahariri
nchini kwa kazi kubwa wanayofanya katika utoaji wa taarifa za umoja huo.
Amesema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la taarifa zinazotolewa na
vyombo vya habari kuhusiana na shughuli za Umoja wa Mataifa ambalo pia
limeenda sambamba maoni na taarifa zinazotolewa kuwa sahihi.
Dk. Kacou pia amesema kwa upande wa Umoja wa Mataifa, jitihada
zimefanyika kuhakikisha kuwa masuala kutoka kwa waandishi yanapatiwa
majibu kwa uharaka na urahisi. Moja ya jitihada hizo ni pamoja na
uboreshwaji wa tovuti ya Umoja wa Mataifa Tanzania ambayo kwa sasa ina
sehemu ya vyombo vya habari ambayo ni maalumu kwa kuhudumia mahitaji ya
waandishi hapa nchini.
Mratibu huyo pia alilishukuru jukwaa la wahariri kwa
kuonyesha nia ya kutaka kufahamu zaidi na kushirikiana na ofisi ya Umoja
wa Mataifa katika mipango yao ya ushirikiano na serikali ya Tanzania,
bara na visiwani. Katikati ni Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke
Jensen na Kulia ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot.
Mwakalishi wa UNESCO Tanzania
Bi. Vibeke Jensen (wa pili kulia) amepongeza mafanikio katika kupanua
elimu ya sekondari nchini na kusema kwamba mpango wa kuwa na angalau
shule moja ya sekondari katika kila kata umefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Pia amepongeza mafanikio katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wengi zaidi
wanajiunga na masomo ya sekondari na kwamba kumekuwa na usawa wa
kijinsia katika uandishikaji wanafunzi shule za msingi.
Hata hivyo, Jensen, ameelezea masikitiko yake kwamba kadri
wanafunzi wanavyoendelea na masomo ya juu sekondari usawa wa kijinsia
umekuwa ukipungua. Amesema pia tatizo kubwa sio uandikishwaji wa
wanafunzi mashuleni lakini ni kitu gani wanachojifunza.
Ameelezea kusikitishwa na kiwango cha elimu kinachotolewa
nchini na kusema kwamba sio tu hakitoi uwezo wa kujiajiri kwa
wanaomaliza sekondari, bali pia kinatoa fursa chache kwa wanafunzi
kuendelea na masomo ya juu.
|
Thursday, May 3, 2012
Screen WAKUU WA TAASISI ZA UMOJA WA MATAIFA (UN) WAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment