Taarifa kwa Vyombo
vya Habari.
Tantrade yatangaza
viingilio vya Saba Saba.
·
Watu wazima kulipa
2500/- kwa siku na watoto 500/-
·
Tiketi za kupaki
magari madogo kwa siku ni 4000/- ma maroli ni 40000/-
Dar es salaam 26 juni
2012,
Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio
vipya vya watu na magari katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF)
yatakayoanza tarehe 28 ya mwezi Juni hadi tarehe 8 mwezi ujao.
Katika taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mdhamini rasmi wa mawasiliano wa maonyesho
hayo Vodacom Tanzania, Tantrade imetangaza malipo ya Shilingi elfu 2500 kwa
watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya
tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto
shilingi 1000.
Kwa watakao hudhuria
maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000,
kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine
zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma
nyingine.
Malipo
ya ada binafsi.
1.
Kwa siku - watu wazima (siku za
kawaida) – 2,500/-
2.
Kwa siku- watoto (siku za kawaida) –
500/-
3.
Kwa siku – watu wazima (siku ya
SabaSaba) – 3,000/-
4.
kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) –
1,000/-
5.
malipo kwa kipindi chote cha maonyesho
- Beji kwa wahusika wa maonyesho - 20,000/-
6.
Beji kwa wahusika wa maonyesho
(maeneo) – 3,000/-
Tiketi za uegeshaji magari.
1.
Kwa siku (magari madogo) -
4,000/-
2.
kwa kipindi chote cha maonyesho –
30,000/-
3.
Malipo kwa pamoja – 200,000/-
4.
Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
5.
Maroli na magari makubwa – 500,000/-
6.
Malipo ya kuegesha magari nje ya
viwanja vya saba saba – 1,500/-
Maonyesho ya
kimataifa ya Dar es salaam ni maonyesho pekee yanayoongoza katika huduma za
masoko Tanzania, maonyesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji
zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na
wanaohudhuria kupata nafasi ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa
kadha wa kadha.
Mwisho...//
Regards
Matina G. Nkurlu
Manager: Public Relations
Location: Mlimani City Building 1. 1st Floor
Group: Executive, Vodacom
Tanzania Limited
Office: +255769700755484800
Ext: 6932; Extension: 0755484800 Ext: 6932
Mobile: +255754710099
C1: FOR PUBLIC/UNRESTRICTED
[This Information
is for public use and no need for control of distribution]
1 comment:
Saba saba imefika, duuh, kweli siku zinakwenda , sasa hivi shule zinafunguliwa, nadaiwa ada za watoto, ....bei za vitu juu,...kodi ya nyumba, na ooh,.....mbona kazi!
Post a Comment