Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo
akiwakaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiq (katikati)
na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala JerrySlaa (wa pili kulia) katika
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar ambapo kampuni hiyo ambayo imeshinda
zabuni ya kufanya usafi katika Manispaa ya Ilala.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiq akizungumza na vyombo vya
habari ambapo ameipongeza Manispaa ya Ilala kwa kufanikiwa kuingia
mkataba na kampuni hiyo wa kufanya usafi katika kata tatu za Manispaa
hiyo kwa kuwa Green Waste Pro Ltd ina vifaa na magari ya kisasa, ambayo
anaamini yatafanikisha lengo la kuweka jiji kuwa safi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo
akizungumza na Mo Blog ambapo amesema wamekuja viwanja vya Mnazi Mmoja
kuonyesha magari waliyonayo likiwemo gari la kisasa la kusafisha
barabara, kunyonya mchanga na hata kusafisha barabara kwa maji.
Amesema
lengo la kampuni yao ni kuhakikisha Manispaa ya Ilala inakuwa safi
akiamini kuwa baada ya miezi michache wananchi wataanza kuona utofauti.
Amefafanua kuwa kwa sasa kampuni ya Green Waste Pro Ltd itaanza kazi ya usafi katika kata za Kivukoni, Mchafukoge na Kisutu.
Afisa
usafishaji wa Manispaa ya Ilala Samweli Bubegwa (kulia) akitoa
maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (katikati) jinsi Manispaa
hiyo ilivyodhamiria kufanya usafi na kuwa mfano wa kuigwa miongoni mwa
wilaya za mkoa huu na jinsi kampuni ya Green West Pro. Ltd ilivyoweza
kushinda Zabuni ya kufanya usafi katika Manispaa ya Ilala.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Sadiq akikata utepe kuzindua rasmi
kampuni ya Green West Pro Ltd ambayo imedhamiria kutakatisha Manispaa ya
Ilala kwa kuwa ndio kitovu cha jiji la Dar es Salaam. Anyeshuhudia
tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (kushoto).
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Afisa Usafishaji Manispaa ya Ilala na
Mkurugenzi Mkuu wa Green Waste Pro Ltd wakishauriana jambo katika
viwanja vya Mnazi Mmoja.
Bw. Said Mecky Sadiq akielekea kukagua magari hayo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam akitazama gari la kisasa la kampuni ya Green
Waste Pro Ltd lenye uwezo wa kusafisha na kufagia barabara mpaka sehemu
za watembea kwa miguu, kunyonya mchanga na pia kusafisha barabara kwa
kutumia maji ambalo ni la kwanza na aina yake Afrika Mashariki.
Pichani
Juu na Chini ni Muonekano wa magari yatakayotumika katika kampeni ya
kusafisha kata tatu za Manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na Kampuni ya
Green Waste Pro Ltd.
Bw.
Sadiq akitazama moja ya Bajaji zitakazotumiwa na kampuni hiyo kuzoa
taka katika maeneo ya pembezoni ambapo magari makubwa hayawezi kufika.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiweka saini katika kitabu cha
wageni mara baada ya kukaguaa vifaa na magari ya kisasa ya kufanya usafi
ya Kmapuni ya Green Waste Pro Ltd. iliyoshinda Zabbuni ya kufanya usafi
katika Manispaa ya Ilala. Katikati ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Ilala Jerry Slaa na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste
Pro Ltd Bw. Anthony Mark Shayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Jerry Slaa naye alishiriki kuweka saini katika kitabu hicho.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Raymond Mushi (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Green Waste Pro Ltd.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam katika picha ya pamoja na baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd na Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni hiyo.
Meneja Fedha Hillary John Aridai (kushoto) na Meneja Uhusiano Vidah Fammie Joseph wa Kampuni wa Green Waste Pro Ltd pamoja na baadhi ya madereva kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment