JUDICA STEPHANO TERI
22.06.1946 hadi
08.03.2012
Alitwaliwa kwa amani baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu Judica Stephano Teri alikuwa mume mpendwa
sana wa Jane (Mwl Teri), baba
mpendwa wa Joan, Linda, Davis &
Hillary na kaka mpendwa wa Mony P. Sisi
wote pamoja na ndugu wengine na wakwe (Aliko,
Leonard & Tina), wajukuu (Tumpe,
Lusako & Evan-Tumaini Alex) na marafiki wake wengi, tutamepatwa na
pengo kubwa ambalo halitazibika.
Wote kwa pamoja, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watu wote waliohusika kwa namna
moja au nyingine kwa njia ya maombi, kadi, simu, barua pepe, michango ya hiari
na kufika katika kipindi cha kuandaa na kumpumzisha mpendwa wetu Judica Teri. Tulifarijika
sana kwa jinsi mlivyoshirikiana nasi kwa upendo mkubwa. Tunawashukuru sana.
Ijapokuwa tungependa tumtaje kila mmoja, lakini
mtatuwia radhi kuwa sio rahisi kufanya hivyo. Tunaomba kila mmoja apokee
shukrani hizi kama zake binafsi. Kipekee tunaomba kuwataja wachungaji wote kwa
huduma za kiroho pamoja na ndugu wa karibu Dkt. Godbless Mlay na mkewe
kwa jinsi walivyomhudumia marehemu kwa kipindi chote alipokuwa amelazwa
hospitalini KCMC, Moshi. Tunawashukuru sana Ukoo wa Teri kwa maandalizi mazuri sana “aikeny mnu moose piu”,
ndugu wengine, marafiki wote na wanakijiji cha Mamba Kusini kwa kuwepo kwa wingi sana kiasi cha kufanya
mazishi kuwa ya heshima kubwa. Tulifarijika sana kwa wingi wa watu wote waliofika
kutoka mbali sana na karibu katika siku ya kumpumzisha mpendwa wetu Judica Teri.
MUNGU
AWALINDE, AWAONGOZE KWA KILA JAMBO NA KUWABARIKI SANA!
YOHANA
MT. 11:25 “Yeye aniaminiye mimi (Yesu),
ajapokufa, atakuwa anaishi….!
No comments:
Post a Comment