Thursday, September 13, 2012

DKT. BILAL AZINDUA MKUTANO WA 14 WA MAWAZIRI WA MAZINGIRA BARANI AFRIKA JIJINI ARUSHA.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Vipaji maalum ya Ilboru wakipata maelezo jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake 21 yanavyofanya kazi, Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa maelezo hayo.
Wanafunzi wa sekondari ya Ilboru wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwenye banda la maonyesho wakati wa mkutano wa 14 wa Mazingira jijini Arusha. Kulia ni Mtaalam wa Mawasiliano wa UN Sangita Khadka Bista, Harriet Macha kutoka Kitengo cha Habari cha UN (UNIC) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu.
Meneja Mkuu wa Uwezeshaji wa Shirika la Manedeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Ishmael Dodoo akimwongoza Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (wa tatu kulia) alipowasili katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano (AICC) kuhuduria mkutano wa 14 wa Mazingira na Uzinduzi wa mtandao wa Mazingira unaosimamiwa na NEMC.
Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kulia) akisikiliza Wafanyakazi wa UN Harriet Macha na Katibu wa klabu za Umoja wa Mataifa mkoa wa Kilimanjaro Angaja Fundisha wakitoa maelezo kwa wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Arusha.

No comments: