Tuesday, September 11, 2012

WAMAREKANI WAIKUMBUKA SEPTEMBER 11

 
Mwanamama Rosario Tejada wa Columbia (kulia) akitafuta jina la mpwa wake aliyefariki katika tukio la kigaidi Septemba 11, 2001 leo katika Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTO) jijini New York .
 
Maria Rodriguez akiwa na picha za marehemu mkwe wake, Emilio Ortiz aliyefariki katika tukio la ugaidi la Septemba 11, jijini New York leo.
Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTO) kikiwaka moto baada ya kulipuliwa Septemba 11, 2001.

MAMIA ya Wamarekani leo wameungana tena katika maadhimisho ya kumbukumbu za tukio la ugaidi lililotekea Septemba 11, 2001 katika majiji ya New York na Washington nchini Marekani.
Umati huo ulikusanyika katika maeneo ya Kituo cha Kimataifa cha Biashara (WTO) jijini New York na Makao Makuu ya Kijeshi ya Marekani, Pentagon kusoma majina ya watu zaidi ya 3,000 waliouawawa katika mashambulizi hayo.
(Picha zote na AP)

No comments: